Brandon Toropov, Mkristo wa Zamani, Marekani (sehemu ya 1 kati ya 2)
Maelezo: Jitihada za mtu binafsi za kujifunza mistari halisi zaidi ya Biblia, mistari ya Q, zinamwongoza kwa Uislamu. Sehemu ya kwanza: Tatizo la Ukristo wa kisasa.
- Na Brandon Toropov
- Iliyochapishwa mnamo 14 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 2,630 (wastani wa kila siku: 3)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Wimbi la Waongofu
Kama wewe ni Mkristo, wazo la kwamba Yesu, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, alikuwa na dini ambayo vyombo vya habari vya leo vinaituhumu kuwa imeleta matatizo mengi ya dunia, inaweza kuonekana kuwa madai yasiyo na msingi. Mimi pia niliyaona hivyo mara ya kwanza nilipokutana nayo, kabla sijasoma Injili zote kwa kina. Hata hivyo unapaswa kujua kwamba Wakristo wengi wa kisasa wamechukua uamuzi wao binafsi uliobadilisha maisha yao kuhusu ujumbe wa Injili na uhusiano wake na Uislamu.
“Kuna uthibitisho wa kuaminika unaoashiria kuongezeka kwa wanaoingia katika Uislamu tangu Septemba 11, si tu katika Uingereza, lakini kote Ulaya na Amerika. Kituo kimoja cha Kiislamu cha Uholanzi kinadai ongezeko la mara kumi, huku Mradi wa Waislamu Mpya, ulio na makao yake Leicester na unaoendeshwa na mama mmoja wa Ireland aliyekuwa Mkatoliki wa zamani, ukiripoti watu wengi wanaojiunga na Waislamu. (London Times, Januari 7, 2002.)
Vyombo Vikuu vya Habari Vinatupuuza
Ni nadra sana kwa Vyombo vya habari vya Magharibi kushiriki na dunia kwa ujumla hadithi za watu hawa wanaoingia katika Uislamu, lakini ninaamini kwamba wengi wa watu hawa -- iwapo wao ni kama mimi -- walijikuta, mwishoni mwa siku, wakiwa na wasiwasi juu ya matokeo ya kumwita Yesu “Bwana” bila kutii maelekezo yake... walijikuta na wasiwasi zaidi kuhusu hilo, kuliko habari yoyote ya vyombo vya habari ya masuala ya kijiografia na kisiasa.
Aina hii ya wasiwasi husababisha watu kubadilisha maisha yao.
Changamoto za Q
Nikijizungumzia mimi binafsi, nilibadilisha maisha yangu mwenyewe kwa sababu sikuweza kupuuza maana ya vifungu halisi vya Injili ambavyo wasomi wakubwa wa leo (wasio Waislamu!) wanaamini kuwa ni vya tarehe ya mbali kabisa kati ya vingine vyote vinavyopatikana.
Maneno haya, ambayo yanaunda maandishi yaliyojengwa upya yanayojulikana kama Q, yanaweza kupatikana yote katika Agano Jipya. Maneno haya ndiyo yaliyo karibu zaidi na maneno halisi ya Yesu, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, kuliko mengine yoyote yanayoweza kupatikana.
Q Inathibitisha Uislamu
Ikiwa ni mara yako ya kwanza kujua Q, unapaswa kujua kile wasomi bora wa Agano Jipya sasa wanajua, yaani kwamba usomi wa leo unatambua kwamba vifungu fulani vya Injili ni muhimu sio tu katika kufundisha, bali ni muhimu zaidi kihistoria kuliko vifungu vingine. Usomi huu umesababisha majadiliano ya kuvutia kati ya wasomi (na wasomaji wachache wa kawaida).
Naamini aya za Q zinathibitisha taswira ya Uislamu ya Yesu ya kuwa alikuwa Nabii wa kibinadamu mwenye ujumbe wa Kiungu, ambao kimsingi hauna tofauti na ule wa Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake.
Nabii Mwanadamu
Sikuendeleza nadharia ya Q. Imekuwa kote kwa miaka sasa. Makasisi wa “Kijadi” wa Kikristo na wanatheolojia kwa ujumla wanaichukia. Wanadai kwamba wanafunzi wa Q kwa namna fulani wanataka kupunguza hadhi ya Yesu, amani iwe juu yake. Kinyume na hiyo, sisi tuna nia ya kujifunza aliyoyasema kihalisi.
Q inawakilisha changamoto kubwa kwa Ukristo wa kisasa, sio tu kwa sababu inaonyesha wazi kwamba taswira ya Uislamu ya Yesu ni sahihi kihistoria. Naamini kwamba ukweli wa kuwa Q kimsingi inathibitisha taswira ya Uislamu ya Yesu kama Nabii mwanadamu haujaonekana vizuri na Wakristo wa leo. Na ni lazima uwe. Kwa sababu mapitio ya makini ya maandiko yanaonyesha kwamba Yesu kwa kweli anawaita watu wake kwa Uislamu.
Yesu alinileta kwa Uislamu!
Nimekuja kwa Uislamu, Alhamdulillah [wa kutukuzwa ni Mwenyezi Mungu] baada ya miongo mitatu ya kutoridhika na Ukristo. Ingawa nimesoma hadithi nyingi za waliokubali uislamu tangu nilipoingia katika Uislamu mwezi Machi mwaka wa 2003, sijaona wengi ambao walitaja Injili kama chanzo chao cha kuingia katika Qurani Tukufu. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwangu.
Nilivutiwa na Injili katika umri mdogo -- kumi na moja -- na nikazisoma kwa bidii peke yangu, licha ya kwamba sikuishi katika nyumba ya Kikristo. Baada ya muda mchache nilijifunza kujiwekea mambo ya kidini kivyangu.
Maswali ya Mapema
Ujanani mwangu nilijifunza maandiko ya Kikristo peke yangu. Bado nina bibilia nyekundu ya King James niliyonunua nikiwa mdogo; andiko langu lililoandikwa kwa hati yangu kwenye ukurasa wa mbele inatangaza Juni 26, 1974, kama tarehe niliyomkubali Yesu kama mwokozi wangu binafsi.
Ninaposema nilisoma maandiko kwa kiasi kikubwa, namaanisha kuwa nilivutiwa na Injili za Matayo, Marko, Luka, na Yohana kama sumaku. Kuna maelezo mengi na maandiko yangu katika Biblia yangu ya zamani katika Zaburi, Mhubiri, na Mithali - lakini maelezo mengi na maandiko yapo katika Injili. Lakini nilihisi, hata nikiwa mdogo, kwamba kulikuwa na matatizo ya ndani kwenye maandiko niliyoyapenda sana.
Ni nani aliyebadilisha Injili?
Naweza kukumbuka vizuri nikisoma habari katika sura ya 22 ya Luka ambapo Yesu aliondoka kutoka kwa wanafunzi, akaomba, akarudi na kuwakuta wakiwa wamelala. Ni nani, nilishangaa, angeweza kumwona akisali... na kisha kulihusisha tukio hilo ili hatimaye liingizwe katika Injili ya Luka? Kuna kifungu kingine katika Injili ambapo Yesu anadhaniwa kuweka maneno “wacha anayesoma aelewe” katika moja ya mazungumzo yake, jambo lililoonekana kuwa lisilo la kawaida kwangu. Na bado kulikuwa na kwingine ambapo mwandishi wa Agano Jipya aliwahakikishia Wakristo wa karne ya kwanza kwamba kizazi chao kingeona ujio wa pili wa Masihi - kifungu ambacho nimeona vigumu kuwiana na mafundisho ya kisasa ya Kikristo. Maswali haya na mengine kuhusu Agano Jipya yalitokea nilipokuwa bado mdogo kabisa, hata kabla sijafikisha miaka kumi na mitano. Je, kuna mtu aliyebadilisha Injili? na iwapo yupo, ni nani? Na kwa nini?
Nilijiwekea maswali yangu ili niyashughulikie baadaye, na kuamua kwamba tatizo halisi ni kwamba sikuwa baadhi ya wanachama cha imani chenye nguvu cha Kikristo.
Mkatoliki
Nilipofikisha umri wa miaka kumi na minane, nilielekea Mashariki ili kujiunga na chuo kikuu na kuingia Kanisa Katoliki la Kirumi. Katika chuo kikuu, nilikutana na msichana mzuri na mwenye huruma ambaye alikuwa mkatoliki; na angekuwa mpenzi na msaidizi wangu mkubwa maishani; hakuwa hasa mtu wa dini, lakini alithamini jinsi mambo haya yalivyokuwa muhimu kwangu, na hivyo aliniunga mkono katika imani zangu. Kwa hakika, Kufupisha mwanzo wa uhusiano wetu katika sentensi chache hapa ni udhalimu mkubwa kwa rasilimali zake zisizokuwa na kikomo za nguvu, msaada, na upendo.
Mkutano na Kuhani
Nilimuuliza kuhani wa chuo kikuu - mtu mzuri na mcha Mungu - kuhusu baadhi ya nyenzo za Injili ambazo zilinipa changamoto, lakini akawa na wasiwasi na kubadilisha maudhui. Katika tukio jingine, nakumbuka nikimwambia kwamba nilikuwa nikisoma kwa kina Injili ya Yohana kwa sababu Injili hiyo ilikuwa (kama nilivyofikiri wakati huo) ni maelezo ya binafsi ya matukio hayo.
Kama awali, alibabaika na kubadilisha maudhui na hakutaka kujadili ubora wa Injili moja juu ya nyingine; alisisitiza tu kwamba zote nne zilikuwa muhimu na kwamba nizisome zote. Haya yalikuwa mazungumzo muhimu, na bainishi, kama nilivyokuja kujua baadaye.
Ukristo au Upaulo?
Hii sio hadithi ya maisha yangu, bali ni maelezo ya wongofu wangu, kwa hivyo nitaruka matukio mengi muhimu. Kuhani huyo mzuri hatimaye alifunganisha ndoa yetu mimi na mpenzi wangu, na tukahamia viunga vya Massachusetts. Kila mmoja wetu alijiendeleza mbele kitaaluma na tukakua. Tulikuwa na watoto watatu wazuri. Na niliendelea kusoma Biblia kila mara. Nilivutiwa na maneno kuhusu taa na jicho, Mwana Mpotevu, Heri, umuhimu wa sala, na mengine mengi - lakini nilikuwa na matatizo makubwa zaidi ya kimantiki na “usanifu” unaozunguka Agano Jipya, hasa kwa Mtume Paulo. Ukweli kwamba Paulo hakuonekana kujenga hoja ya kitheolojia karibu na chochote ambacho Yesu alisema kihakika ulikuwa tatizo kubwa sana kwangu.
Katikati ya miaka ya 1990, mimi na mke wangu sote tulivunjika moyo sana na Kanisa Katoliki, na sababu kubwa ni kutokana na kuhani mmoja mbaya ambaye hakuyapea kipaumbele mahitaji ya kiroho ya jamii yake. Baadaye tulikuja kujua kwamba alikuwa akimsitiri mnyanyasaji wa mtoto!
Mprotestanti
Niliona ni muhimu kujitumbukiza katika jamii ya imani. Nilijiunga, na nikawa mwenye bidii, katika dhehebu la Kiprotestanti, amablo ni Kanisa la Kutaniko.
Kwa hivyo niliongoza madarasa ya Shule ya Jumapili kwa watoto, na kwa kifupi nilifundisha darasa la Injili kuhusu Mifano kwa watu wazima. Katika madarasa ya Shule ya Jumapili kwa watoto nilifuata vizuri mtaala niliopewa; lakini katika darasa la watu wazima, nilijaribu kuwashawishi washiriki kujiuliza maswali kuhusu Mifano fulani moja kwa moja, bila kuchuja kila kitu kupitia Mtume Paulo. Tulikuwa na majadiliano ya kuvutia, lakini nilihisi upinzani fulani, na sikujaribu kufundisha darasa la watu wazima tena. Mke wangu hatimaye alijiunga na kanisa langu. (Yeye ni mwanachama huko leo.)
Kwa hatua hii, nilikuwa nimeathiriwa sana na uwiano ulio dhahiri kati ya mila ya kifumbo ya Kikristo na ile ya Wasufi na Wabudha wa Zen. Hadi nilikuwa nimeandika kuhusu mambo hayo. Lakini hakukuonekana kuwa na mtu yeyote katika kanisa langu ambaye alishiriki bidii yangu kwa masuala haya.
Ongeza maoni