Bruce Paterson, Mkristo wa zamani, Uingereza

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Baada ya kuchoka na maswali yasiyojibiwa katika imani yake, mtafutaji ukweli anatafuta mwanga katika dini za Mashariki, dini za kitamaduni, na hatimaye anaupata katika Uislamu.

 • Na Bruce Paterson
 • Iliyochapishwa mnamo 14 Dec 2021
 • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
 • Ilichapishwa: 0
 • Imetazamwa: 1,078 (wastani wa kila siku: 1)
 • Ukadiriaji: bado hakuna
 • Imekadiriwa na: 0
 • Imetumwa kwa barua pepe: 0
 • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Ningependa kuchukua fursa hii kuwaelezea safari yangu ya kujiunga Uislamu na ninatumai kuwa kwa kuwaelezea kuhusu safari yangu nitaweza kuwasaidia katika safari yenu ya maisha. Sisi sote tunazaliwa katika tamaduni, nchi na dini mbalimbali katika kile kinachoonekana mara nyingi kuwa dunia yenye utata na mchanganyiko. Tunapoangalia ulimwengu unaotuzunguka, tunaweza kuona mchanganyiko wake kwa urahisi: vita, umaskini na uhalifu. Kuna haja ya kuendelea? Hata hivyo tunapotazama malezi yetu wenyewe na elimu yetu, tunawezaje kuhakikisha kwamba mambo yote tuliyoambiwa, ni ya kweli?

Kwa bahati mbaya, watu wengi ulimwenguni wanajaribu kujificha na kuepukana na matatizo ya dunia badala ya kusimama na kuukabili ukweli. Ukweli kwa mara nyingi ndio njia ngumu kabisa kufuata. Swali ni: Je, uko tayari kusimama kwa ajili ya ukweli? Je, una nguvu za kutosha? Au, utatoroka na kujificha kama wengine?

Nilianza kutafuta ukweli miaka kadhaa iliyopita. Nilitaka kujua ukweli kuhusu kuwepo kwetu. Kwa hakika, kuelewa maisha kwa usahihi ndio ufunguo wa kutatua matatizo yote ya kidunia ambayo tunayakabili leo. Nilizaliwa katika familia ya Kikristo na hapa ndipo safari yangu ilipoanza. Nilianza kusoma Biblia na kuuliza maswali. Punde si punde nikawa siridhiki. Kuhani aliniambia, “Unahitaji tu kuwa na imani.” Kutokana na kusoma Biblia nimeona utata na mambo yasiyo sahihi kabisa. Je! Mungu anajipinga mwenyewe? Je! Mwenyezi Mungu anasema uongo? Bila shaka jibu ni la!

Niliwachana na Ukristo, nikifikiri maandiko ya Wayahudi na Wakristo yameharibiwa na kwa hivyo singeweza kutofautisha ukweli na uongo. Nilianza kujua kuhusu Dini za Mashariki na Falsafa zao, hasa Ubuddha. Nilitumia muda mrefu kutafakuri katika mahekalu ya Kibuddhi na kuzungumza na watawa. Kusema kweli, kutafakari huku kulinipa hisia nzuri. Shida ilikuwa kwamba haukujibu maswali yangu yoyote kuhusu lengo halisi la kuwepo kwetu. Badala yake uliyaepuka kiujanja kwa njia ambayo inaifanya hata kuizungumzia ni ujinga.

Nilisafiri kuenda sehemu nyingi za dunia wakati wa jitihada zangu kwa ajili ya kutafuta ukweli. Nilivutiwa sana na dini za kitamaduni na njia ya fikira za kiroho. Niliona kwamba mengi ya yale ambayo dini hizi zilikuwa zikisema zilikuwa na ukweli fulani ndani yake, lakini sikuweza kukubali dini nzima kama ukweli. Hii ilikuwa sawa na pale nilipoanza na Ukristo!

Nilianza kufikiri kwamba kuna ukweli katika kila kitu na haijalishi unachoamini au unachofuata. Kusema kweli hii ni namna moja ya kutoroka. Namaanisha, je, inaweza kueleweka vipi: kuwa kuna ukweli fulani kwa mtu mmoja na ukweli mwingine kwa mtu mwingine? Kunaweza kuwa na ukweli mmoja tu!

Nilihisi nimechanganyikiwa, nilianguka chini kwa sakafu na kuomba, “Tafadhali Mungu, nimechanganyikiwa sana, tafadhali niongoze kwa ukweli.” Hapo ndipo nilipogundua Uislamu.

Bila shaka siku zote nilijua kitu kuhusu Uislamu, lakini nilijua tu kile tunachosikia katika nchi za Magharibi. Nilishangazwa sana lakini na kile nilichokipata. Nilivyosoma Qurani zaidi na kuuliza maswali kuhusu mafundisho ya Uislamu, ndivyo nilivyopokea ukweli. Tofauti ya kushangaza kati ya Uislamu na kila dini nyingine ni kwamba Uislamu ndio dini pekee inayoweka tofauti na mpaka mkali kati ya Muumba na viumbe. Katika Uislamu, tunamwabudu muumba. Rahisi. Hata hivyo utaona kwamba katika kila dini nyingine kuna aina fulani ya ibada inayohusisha viumbe. Kwa mfano, kuwaabudu wanadamu ambao wanaaminika kuwa umwilisho wa Mungu au mawe, ni imani inayopatikana mahali nyingi. Kusema kweli lakini, ikiwa utaabudu chochote, basi muabudu aliye umba vyote. Yule aliyekupa maisha yako na yule atakayeyaondoa tena. Katika Uislamu, dhambi pekee ambayo Mungu hatasamehe ni kuabudu viumbe.

Hata hivyo, ukweli wa Uislamu unaweza kupatikana katika Qurani. Qurani ni kama dalili na mwongozo wa maisha. Katika kitabu hicho utapata majibu ya maswali yote. Kwangu mimi, kila kitu nilichojifunza kuhusu dini zote tofauti, kila kitu nilichojua kuwa kweli, kiliunganishwa pamoja kama vipande vya fumbo. Nilikuwa na vipande vyote pamoja lakini sikujua jinsi ya kuviunganisha pamoja.

Kwa hivyo ningependa kukuhimiza ufikirie kuhusu Uislamu sasa. Uislamu wa kweli kama ulivyoelezwa katika Qur'ani. Sio Uislamu tunayofundishwa huko Magharibi. Unaweza angalau kuwa na uwezo wa kukata kwa nusu safari yako ya kutafuta ukweli wa maisha. Nakuombea mafanikio kivyovyote.

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

 • (Haitaonyeshwa kwa umma)

 • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

  Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.