Craig Robertson, Mkatoliki wa zamani, Kanada (sehemu ya 2 kati ya 2): Kujifunza Kukubali

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Baada ya kupata njia yake ya kurudi kwa Ukristo, Craig anasalitiwa na marafiki zake na anapotea tena, hadi anapopatana na Muislamu akiwa kazini.

 • Na Craig Robertson
 • Iliyochapishwa mnamo 14 Dec 2021
 • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
 • Ilichapishwa: 0
 • Imetazamwa: 1,891 (wastani wa kila siku: 3)
 • Ukadiriaji: bado hakuna
 • Imekadiriwa na: 0
 • Imetumwa kwa barua pepe: 0
 • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Bado ninakumbuka hadi leo mkutano wangu wa kwanza na Muislamu. Mmoja wa wavulana alimleta rafiki yake kwenye nyumba ya vijana. Alikuwa mtoto wa Kiislamu ambaye jina lake nimesahau. Ninachokumbuka ni mvulana huyo akisema “Nimemleta rafiki yangu 'fulani', yeye ni Muislamu na nataka kumsaidia awe Mkristo”. Nilishangaa kabisa na mtoto huyu mwenye umri wa miaka 14, alikuwa na utulivu na urafiki! Amini au usiamini, alijitetea mwenyewe NA Uislamu dhidi ya Wakristo kadhaa ambao walikuwa wanamtukana yeye na Uislamu! Tulipokuwa tukiketi pale tukipitia Biblia zetu na kuzidi kukasirika, aliketi pale tu, akitabasamu na kutuambia kuhusu kuabudu wengine badala ya Mungu na jinsi kuna upendo katika Uislamu. Alikuwa kama swara aliyezungukwa na mafisi kadhaa, lakini wakati wote huo, alikuwa na utulivu na heshima. Nilishangazwa sana!

Mtoto huyo wa Kiislamu aliacha nakala ya Qurani kwenye rafu, huenda aliisahau au aliiacha kwa kusudi, sijui, lakini nilianza kuisoma. Hapo hapo nilipandwa na hasira nilipoona kitabu hiki kilikuwa na mantiki inayoeleweka zaidi kuliko Biblia. Nilikitupa juu ya kitanda na kuenda zangu, nikiungua kwa hasira; lakini baada ya kukisoma, nilikuwa na shaka ya kunung'unika katika moyo wangu. Nilijaribu sana kusahau kuhusu mtoto huyo wa Kiislamu na kufurahia muda wangu na marafiki zangu katika nyumba ya vijana. Kikundi cha vijana kilikuwa kikikwenda Makanisa mbalimbali mwishoni mwa wiki kwa ajili ya sala, na usiku wa Jumamosi ulitumika kukaa katika Kanisa moja kubwa badala ya kukaa kwenye baa. Nakumbuka nikiwa katika tukio moja la namna hiyo liitwalo 'Kisima' na nilijisikia nikiwa karibu sana na Mungu na nilitaka kujinyenyekeza na kumwonyesha Muumba wangu upendo wangu kwake. Nilifanya nilichokiona kuwa asili, nilisujudu. Nimesujudu kama Waislamu wanavyofanya katika sala za kila siku, lakini sikujua niliyokuwa nikifanya, yote ninayoyajua ni kwamba nilihisi vizuri sana... nilihisi nilifanya kitu sawa na nzuri kuliko kitu kingine chochote nilichowahi kufanya. Nilijihisi mwema sana na kuendelea katika njia yangu lakini kama kawaida, nilianza kuona mambo yakiteleza tena.

Mchungaji daima alitufundisha kwamba ni lazima tuwasilishe nia yetu kwa Mungu, na sikutaka chochote zaidi ya kufanya hivyo; lakini sikujua ni kwa jinsi gani! Daima niliomba “Tafadhali Mungu, fanya nia yangu iwe yako, nifanye kufuata nia Yako” na kadhalika, lakini hakuna kitu kilichotokea. Nilijihisi nikiteleza na kwenda polepole mbali na Kanisa huku imani yangu ikiyeyuka. Ilikuwa wakati huo ndipo rafiki yangu , yule Mkristo ambaye alikuwa amenisaidia kuja kwa Yesu, pamoja na rafiki yangu mwingine wa karibu, walimbaka mpenzi wangu ambaye nilikuwa naye kwa miaka miwili. Nilikuwa katika chumba kingine nikiwa nimelewa, sijui nini kinatokea na siwezi kuzuia chochote. Wiki kadhaa baadaye, ilijulikana kwamba aliyekuwa akisimamia nyumba ya vijana alikuwa amemlawiti mmoja wa wavulana ambaye alikuwa rafiki yangu.

Ulimwengu wangu ulikuwa umevunjika! Nilikuwa nimesalitiwa na marafiki zangu wengi, watu ambao walidhaniwa kuwa karibu na Mwenyezi Mungu, na wanafanya kazi ya kuelekeza watu Peponi. Sikuwa na chochote zaidi cha kutoa, Nilikuwa mtupu tena. Nilitembea tu kila mahali kama hapo awali, kwa upofu na bila mwelekeo wowote, nikifanya tu kazi na kulala na kuenda sherehe mbalimbali. Mpenzi wangu aliniacha baada ya muda mfupi. Hisia za hatia, hasira na huzuni zimezunguka uhai wangu wote. Muumba wangu angewezaje kuruhusu kitu kama hicho? Ubinafsi wangu ulikuwa mkubwa aje?

Baada ya muda mfupi, meneja wangu wa kazi aliniambia kuwa “Mwislamu” mmoja angekuja kufanya kazi nasi, alikuwa mtu wa dini na kuwa tunapaswa kujaribu kuwa na heshima tukiwa naye. Mwislamu huyo alipokuja tu alianza Da'wah. Hakupoteza muda wowote katika kutuambia kuhusu Uislamu na kila mtu alimwambia kwamba hakutaka kusikia chochote kuhusu Uislamu, isipokuwa mimi! Roho yangu ilikuwa ikilia na hata ukaidi wangu haukuweza kuzuia kilio. Tulianza kufanya kazi pamoja na kujadili imani zetu. Nilikuwa nimepoteza matumaini na Ukristo kabisa, lakini alipoanza kuniuliza maswali, imani yangu iliongezeka na nilihisi kama mpiganaji wa vita vya 'Krusedi' anayetetea Imani kutoka kwa uovu wa “Mwislamu” huyu.

Ukweli wa jambo hilo ni kwamba Mwislamu huyo hakuwa mbaya kama nilivyoambiwa. Kwa kweli, alikuwa bora kuliko mimi. Hakulaani, hakuwahi kukasirika na daima alikuwa na utulivu, mwenye fadhili na mwenye heshima. Nilivutiwa kweli na kuamua kwamba angekuwa Mkristo mzuri. Tulijadiliana na kuulizana mambo kuhusu dini za kila mmoja wetu, lakini baada ya muda nilihisi nikijihami zaidi na zaidi. Wakati mmoja, nilikasirika sana... hapa nilikuwa nikijaribu kumshawishi akubali ukweli wa Ukristo, na nilihisi ni yeye ndiye alikuwa kwa njia ya ukweli! Nilianza kuchanganyikiwa zaidi na zaidi na sikujua cha kufanya. Kile nilichokijua ni kwamba nilifaa kuongeza imani yangu, hivyo nikaruka katika gari langu na kunguruma mbali kueleka 'Kisima'. Niliamini kwamba kama ningeweza kusali tena, ningeweza kurudisha hisia hizo na imani imara na kisha ningeweza kumshawishi Muislamu huyo vizuri. Hatimaye nilifika huko, baada ya kuharakisha kwa njia nzima, na nikapata kumefungwa! Hakuna mtu mwingine alikuwa hapo, nilitazama kote ili angalau nipate tukio lingine linalofanana na la kwanza ili niweze 'kupata nguvu' lakini hakuna kitu kilitokea. Nilirudi nyumbani huku nikiwa nimekata tamaa.

Nilianza kutambua kwamba nilikuwa nikisukumwa katika mwelekeo fulani, kwa hivyo nikaomba tena na tena kwa Muumba wangu ili aelekeze nia yangu Kwake. Nilihisi kwamba dua yangu ilikuwa ikijibiwa; Nilikwenda nyumbani na kulala kitandani na wakati huo nilitambua kwamba nilihitaji kuomba kwa jinsi ambayo sijawahi omba mbeleni. Niliketi kitandani na kulia, 'Yesu, Mungu, Buddha, yeyote uliye, tafadhali, tafadhali niongoze, nakuhitaji Wewe! Nimefanya maovu mengi sana katika maisha yangu na nahitaji msaada wako. Ikiwa Ukristo ndio njia sahihi basi unipe nguvu, na ikiwa ni Uislamu basi nilete kwake!' Niliacha kuomba na machozi yalikwenda, na ndani kwa kiini cha nafsi yangu nilihisi utulivu, nilijua jibu lilikuwa nini. Nilikwenda kazini siku iliyofuata na kumwambia ndugu wa Kiislamu “naweza kukusalimia aje?” Aliniuliza nilimaanisha nini na nikasema, “Nataka kuwa Muislamu”. Aliniangalia na akasema “Allahu Akbar!”. Tulikumbatiana kwa dakika nzima na nikamshukuru kwa kila kitu na nikaanza safari yangu katika Uislamu.

Nikitazama nyuma kwa matukio yote yaliyotokea katika maisha yangu kwa muda wote huo, natambua kwamba nilikuwa natayarishwa kuwa Muislamu. Mungu alinionyesha huruma nyingi. Kati ya yote yaliyotokea katika maisha yangu, kulikuwa na kitu cha kujifunza. Nilijifunza uzuri wa kwa nini Uislamu ulikataza ulevi, zinaa, na haja ya kuvaa Hijab. Hatimaye niko kwa ardhi iliyonyooka, sielekei tena upande mmoja; ninaishi maisha ya wastani, na ninajitahidi kuwa Muislamu mwema.

Kuna changamoto kila wakati, na nina uhakika wengi wenu mmezipitia, kama nilivyozipitia mimi. Lakini kupitia changamoto hizi, kupitia maumivu haya ya kihisia, tunakuwa na nguvu; tunajifunza na ninatumai tutageuka kwa Mungu. Kwa wale miongoni mwetu ambao wamekubali Uislamu wakati fulani maishani mwao, sisi kweli tumepata kheri na bahati. Tumepewa nafasi, nafasi ya kupata rehema kubwa kabisa! Rehema ambayo hatustahili, lakini Mungu bado atatupea siku ya Kiyama. Nimejenga amani na familia yangu na ninatumai kuanza yangu mwenyewe Mungu akipenda. Uislamu kwa kweli ni njia ya maisha, na hata tunapopitia mateso kwa mikono ya Waislamu wenzetu au wasio Waislamu, lazima tukumbuke daima kuwa tunafaa kuwa na subira na kumgeukia Mungu tu.

Ikiwa nimesema kitu kisicho sahihi ni kutoka kwangu, na ikiwa nimesema kitu kilicho sahihi kimetoka kwa Mwenyezi Mungu, Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu amjalie rehema na baraka Mtume wake Muhammad, Amina.

Mungu aongeze Imani yetu na kuifanya iambatane na yale yanayompendeza Yeye na kutupatia Pepo Yake, Amina!

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

 • (Haitaonyeshwa kwa umma)

 • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

  Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

(Soma zaidi...) Ondoa