Maswali Saba ya Kawaida kuhusu Uislam (sehemu ya 1 kati ya 2)

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Baadhi ya maswali ya kawaida yanayoulizwa kuhusu Uislamu. Sehemu ya 1: Uislamu ni nini? Waislamu ni wakina nani? Allah ni nani? Muhammad ni nani?

 • Na Daniel Masters, Isma'il Kaka and Robert Squires
 • Iliyochapishwa mnamo 08 Dec 2021
 • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
 • Ilichapishwa: 3
 • Imetazamwa: 8,924 (wastani wa kila siku: 10)
 • Ukadiriaji: bado hakuna
 • Imekadiriwa na: 0
 • Imetumwa kwa barua pepe: 0
 • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

1. Uislamu ni nini?

Seven_Common_Questions_about_Islam_(part_1_of_2)_001.jpgUislamu ni jina la dini, au kiufasaha zaidi ni ‘njia ya maisha’, ambayo Mungu (Allah) aliifunua na ilifanywa na Manabii na Mitume wa Mungu ambao aliituma kwa wanadamu. Hata jina lake lipo juu na la kipekee miongoni mwa dini zingine kwa kumaanisha hali ya kuwa; haimuhusishi mtu flani, kama vile Ukristo, Ubudha au Uzoroasta; kabila kama la Mayahudi; au nchi kama Uhindu. Ni mzizi wa neno la Kiarabu Islam kwa kuchukua maana ya amani, usalama, heshima, ulinzi, kutokuwa na lawama, uzuri, kujitoa, kukubali, kujisalimisha, na wokovu. Hususani Uislamu una maana kuwa katika hali ya kujisalimisha kwa Mungu, kumwabudu Yeye peke Yake, na kukubali na kutii Sheria Yake. Kwa kujisalimisha, amani, ulinzi, na maisha yote yakifanya hivyo maana yake itatimia. Hivyo, Muslim au Muslimah ni mtu (mwanume au mwanamke) wapo ndani ya kujisalimisha huko. Uislamu wa mtu udhoofika kwa dhambi, ujinga, na matendo mabaya, na hutenguka kwa kumshirikisha Mungu au kutokumwamini Yeye.

2. Waislamu ni Akina nani?

Neno la Kiarabu “Muslim” linamaanisha “mtu mwenye kutekeleza mambo ya Uislam (kujisalimisha katika mapenzi na sheria ya Mungu)”. Ujumbe wa Uislamu umemaanishwa kwa ulimwengu wote, na mtu yoyote atakaye ukubali ujumbe huu anakuwa Muislamu. Baadhi ya watu wanaamini vibaya kuwa Uislamu ni dini tu ya Waarabu, Ila ukweli uko mbali sana na hili. Kiuhalisia, zaidi ya 80% ya Waislamu wote duniani siyo Waarabu Japokuwa Waarabu wengi ni Waislamu, kuna Waarabu ambao ni Wakristo, Wayahudi na Wasiokuwa na dini. Kama mtu akiangalia watu mbali mbali wenye kuishi katika dunia ya Waislamu - kuanzia Nigeria hadi Bosnia na kuanzia Morocco hadi Indonesia - ni rahisi kuona Waislamu wanatoka kwenye asili mbalimbali, vikundi vya makabila, tamaduni na uraia. Uislamu umekuwa ujumbe wa kilimwengu kwa watu wote. Hili linaweza kuonekana kwa Maswahaba wa mwanzo wa Mtume Muhammad hawakuwa tu Waarabu, ila pia Waajemi, Waafrika na Waroma wa Byzantine. Kuwa Muislamu kunamaanisha ukubali kikamilifu na utii kikamilifu katika mafundisho ya ufunuo na sheria za Mungu Mkuu. Muislamu ni mtu aliyekubali kwa uhuru akiamini ndani ya imani yake, kuthamini na imani kwa mapenzi ya Mungu Mtukufu. Zamani, japokuwa hauoni sana hivi sasa, neno “Mohammedans” lilitumika kama chapa ya Waislamu. Chapa hii haifai, na ndio matokeo ya labda upotovu wa makusudi au ni ujinga tu. Moja ya sababu ya upotovu huu ni kuwa Wazungu walifundishwa kwa karne kuwa Waislamu wanamuabudu Mtume Muhammad katika njia sawa ya Wakristo wanavyo muabudu Yesu. Hii siyo kweli, Wakati mtu hatachukuliwa kuwa Muislamu kama atamuabudia yoyote au chochote asiyekuwa Mungu Mtukufu.

3. Allah ni nani?

Mara nyinyi mtu anakuwa amesikia neno la Kiarabu la “Allah” likiwa linatumika kwenye maongezi yanayohusu Uislamu. Neno “Allah” ni neno la Kiarabu lenye maana ya Mungu Mtukufu, pia ni neno moja linalotumiwa na wanaoongea Kiarabu Wakristo na Wayahudi. Na kiujumla, neno Allah lilikuwa linatumika zamani sana kabla ya neno God, kwakuwa Kingereza ni lugha mpya. Kama mtu angechukua Biblia iliyo tafsiriwa Kiarabu, mtu angeliona neno “Allah” linatumika ambapo neno “God” linatumika kwa Kingereza. Kwa mfano, Wakristo wanaoongea Kiarabu wanasema Yesu ni, kulingana na dini yao, Mtoto wa Allah. Kwa kuongezea, neno la Kiarabu la Mungu Mtukufu ni, “Allah”, ni neno sawa na God katika lugha nyingine ya Kiyahudi. Kwa mfano, Neno la Kihebrew kwaajili ya Mungu ni “Elah”. Katika sababu mbali mbali, baadhi ya wasiokuwa Waislamu kwa bahati mbaya wanaamini kuwa Waislamu wanamuabudu Mungu mwingine asiye kuwa Mungu wa moses na Abraham na Yesu. Hii siyo kweli, kwakuwa Monotheismu wa kweli wa Uislamu huwaita watu wote kumuabudu Mungu wa Noah, Abraham, Moses, Yesu na Mitume yote mingine, amani iwe juu yako.

4. Muhammad ni nani?

Mwisho na Mtume wa mwisho ambaye ametumwa na Mungu kwa mwanadamu alikuwa Mtume Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake. Katika umri wa miaka arobaini, alipokea ufunuo kwa Mungu. Kisha akatumia muda wake uliobakia kuelezea, na kuishi na kufundisha Uislamu, dini ambayo Mungu amemfunulia. Mtume Muhammad ni mkubwa kuliko wote kwa sababu nyingi, ila kubwa ni kuchaguliwa na Mungu kuwa Mtume wa mwisho - jukumu lake kuwaongoza wanadamu litaendelea hadi Siku ya Mwisho - na kwasababu alitumwa kama rehema kwaajili ya mwanadamu. matokeo ya kazi yake imewaleta watu katika imani ya Mungu Mmoja zaidi ya mtume yoyote. Tangu mwazo wa muda, Mungu ametuma mitume katika dunia, kila mmoja katika nchi mahususi. Mtume Muhammad, hata hivyo, alitumwa kama Mjumbe wa mwisho kwa wanadamu wote.

Japokuwa jamii nyingine za kidini zinadai kumuamini Mungu Mmoja, baada ya muda, mawazo potofu huingia kwenye imani na matendo ikiwapeleka mbali na monotheismu ya mitume. Wengine waliwachukulia manabii na watakatifu wao kuwa waombezi wao kwa Mungu Mtukufu. Wengine hata waliamini mitume yao ni udhihirisho wa Mungu, au “Mungu aliyefanyika mwili” au “Mwana wa Mungu”. Dhana hizi potofu husasabisha ibada ya viumbe vilivyoumbwa badala ya Muumbaji, na kuchangia ibada ya masanamu kuamini kuwa Mungu Mtukufu anaweza kufikiwa kwa makubaliano. Ili kujilinda na uongo huu, Mtume Muhammad alikuwa mara zote anajieleza kuwa yeye ni mwanadamu akiwa na kazi ya kuhubiri na kutii ujumbe wa Mungu. Aliwaambia Waislamu kumchukulia yeye kama “Mjumbe wa Mungu na Mtumwa wake”. Katika maisha yake na mafundisho, Mungu amemfanya Mtume Muhammad kuwa mfano wa watu wote - alikuwa nabii wa mfano, mkuu wa nchi, kiongozi wa jeshi, mtawala, mwalimu, jirani, mume, baba na rafiki. Tofauti na manabii na wajumbe wengine, Mtume Muhammad aliishi kwenye mwanga kamili wa historia,na maneno yake na vitendo vilinakiliwa kwa umakini na kukusanywa. Waislamu hawahitaji kuwa na imani tu kuwa alikuwepo, au kuwa mafundisho yake yamehifadhiwa - wanajua kuwa ni kweli. Mungu amechukua mwenyewe kulinda ujumbe uliofunuliwa kwa Muhammad kutoka kwenye uharibifu au kusahaulika au kupotea. Hii ilikuwa muhimu kwasababu Mungu aliaidi Muhammad kuwa Mjumbe wa mwisho kwa wanadamu. Wajumbe wote wa Mungu walihubiri ujumbe wa Uislamu - mf. kujisalimisha katika sheria za Mungu na kumuabudu Mungu peke yake – ila Muhammad ni mtume wa mwisho wa Uislamu ambaye alileta ujumbe wa mwisho na kamili ambao hautaweza kubadilishwa hadi Siku ya Mwisho.

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

 • (Haitaonyeshwa kwa umma)

 • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

  Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.