Msingi wa Maadili ya Uislamu

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Nguzo itawakilisha umuhimu wa Uislamu: msingi wa imani, vitendo vya dini, Kurani, mafundisho ya Mtume Muhammad, na Shariah. Nakala rahisi amabayo inaunganisha Uislamu kwa ufupi.

  • Na Imam Mufti (© 2013 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 10 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 20 Aug 2023
  • Ilichapishwa: 3
  • Imetazamwa: 5,335 (wastani wa kila siku: 5)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Core_Values_of_Islam._001.jpgNi ngumu kuubana Uislamu wote katika misingi michache ya maadili. Ila, cha umuhimu ni imani na vitendo vya kidini vilivyoelekezwa na Mtume Muhammad mwenyewe. Hivyo, kuna makubaliano ya jumla kwao na kati ya Waislamu wote. Inatoa mlinganisho kwani Wayahudi na Wakristo wa mwanzo kuwa hawana mfumo sawa katika imani. Wakristo, kwa mfano, wana madhehebu mbali mbali[1] na Wayahudi awana dhebebu katika imani. Mayahudi wa zamani wanakubali amri 613 ambazo Maimonides, rabbi wa Kiyahudi kutoka Muislamu wa Hispania, ilinakiliwa na kuonyeshwa ndani ya karne ya 12.

Kwa kuongezea, Wasomi wa Kiislamu, wa zamani na sasa, pia wameonyesha na wakati mwingine kukubaliana na msingi wa mafundisho ya Kurani, ya Mtume Muhammad, neema na baraka za Mungu ziwe juu yake, na ‘umuhimu’ wa sheria ya Kiislamu (Shariah).

Msingi wa Imani ya Uislamu: Nguzo Sita za Imani

Zaidi ya bilioni ya Waislamu wanachangia katika misingi ya imani ambazo zinajulikana kama "Nguzo za Imani." Nguzo hizi za imani zinajenga msingi wa mfumo wa kiimani.

1. Kumwamini Mungu Mmoja: Katika mafunzo muhimu ya Uislamu ni kuwa Mungu pekee ndiye anayepaswa kutumikiwa na kuabudiwa. Pia, dhambi kubwa katika uislamu ni kumwabudu mwingine badala ya Mungu. Pia, Waislamu wanaamini ndiyo dhambi pekee ambayo Mungu haisamei kama mtu atakufa bila kufanya toba yake.

2. Kuwaamini Malaika: Mungu ameumba viumbe visivyoonekana vinaitwa malaika ambao wanafanya kazi bila kuchoka kusimamia Ufalme Wake kwa heshima kubwa. malaika wametuzunguka muda wote, kila mmoja ana kazi; wengine wananakili maneno yetu na vitendo.

3. Kuwaamini Mitume wa Mungu: Waislamu wanaamini Mungu anawasilisha Muongozo wake kwa kupitia mitume wake waliotumwa katika kila taifa. Mitume hii ilianza na Adam na ikiwemo Noah, Abraham, Musa, Yesu and Muhammad, amani iwe juu yao. Ujumbe maalumu wa hawa wote ulikuwa kuna Mungu mmoja tu wa kweli na Yeye pekee ndiye anayepaswa kuombwa na kuabudiwa.

4. Kuamini Vitabu Vilivyofunuliwa na Mungu: Waislamu wanaamini Mungu amefunua hekima Yake na maelekezo kupitia ‘vitabu’ kwa baadhi ya mitume kama Zaburi, Torati, na Injili. Baada ya muda, ila, mafundisho ya asili yanapotoshwa na kupotea. Waislamu wanaamini Kurani ni ufunuo wa mwisho wa Mungu kufunuliwa Muhammad na umehifadhiwa kiuhakika.

5. Kuamini katika Siku ya Hukumu: Maisha ya hii dunia na kila kilichopo kitafikia mwisho katika siku iliyokusudiwa. Katika muda huo, kila mtu atafufuliwa kutoka ufu. Mungu atamhukumu kila mtu peke yake, kulingana na imani yake na matendo yake mazuri na mabaya. Mungu ataonyesha huruma na usawa katika kuhukumu. Kulingana na mafundisho ya Kiislamu, wale ambao wanamuamini Mungu na kufanya vitendo vizuri watazawadiwa pepo ya milele. Wale watakao kataa imani ya Mungu wataadhibiwa milele Jahanamu.

6. Kuamini kwenye Hatma na Nguvu ya Mungu: Waislamu wanaamini kuwa kwakuwa Mungu ndiye mshikiliaji wa maisha yote, hakuna kitu kinatokea bila Ruhusa Yake na kwa utambuzi Wake wote. Kuamini huku akukinzani na wazo la uhuru wa kutenda. Mungu atulazimishi, machaguo yetu yanajulikana na Mungu kabla kwasababu maarifa yake yamekamilika. Utambuzi huu unawasaidia waaminio kipindi cha shida na ugumu.

Msingi wa Matendo ya Dini ya Kiislamu:"Nguzo" Tano za Uislamu

Ndani ya Uislamu, kuabudu ni sehemu ya maisha ya kila siku na sio mila tu. Vitendo rasmi vya ibada vinajulikana kama"nguzo" tano za uislamu. Nguzo tano za Uislamu ni tamko la imani, swala, kufunga, kutoa swadaka, na hijja.

1. Tamko la imani:"Tamko la imani" ni kauli ya, "La ilaha illa Allah wa Muhammad Rasul-ullah", ikimaanisha "Hakuna mola apaswae kuabudiwa kwa haki ila Mungu(Allah), na Muhammad ni mjumbe (mtume) wa Mungu". Tamko la Imani ni zaidi ya tamko tu; inatakiwa ionyeshwe na matendo ya mtu. Kusilimu katika Uislamu , mtu anatakiwa aseme tamko hili.

2. Kuswali Kila Siku: Kuswali ni njia ya Muislamu kuungana na Mungu na kupata nguvu ya kiroho na pumziko la akili. Waislamu wanafanya ibada hii ya kuswali mara tano kwa siku.

3. Zakah: Aina ya sadaka. Waislamu wanatambua kuwa utajiri wote ni baraka kutoka kwa Mungu, na majukumu kadhaa yanahitajika kurudisha. Ndani ya Uislamu, ni jukumu la matajiri kuwasaidia masikini na wenye kuhitaji.

4. Kufunga Ramadan: Mara moja kila mwaka, Waislamu wanalazimishwa kufunga kwa mwezi mzima kuanzia asubuhi hadi jioni. Kipindi cha kujitoa sana kiimani kinajulikana kama Ramadan ambapo chakula, maji na tendo la ndoa haviruhusiwi wakati wa kufunga. Baada ya machweo mtu anaweza kufurahia vitu hivi. Kipindi hiki cha mwezi Waislamu hujizuia na kuzingatia ibada na kutoa. Wakati wa kufunga, Waislamu wanajifunza kuwahurumia wale wenye chakula kidogo ulimwenguni.

5. Hajj safari ya kwenda Makka: Kila Muislamu anajitahidi kusafiri mara moja katika maisha yake katika sehemu takatifu ya kuabudu ya Makka, siku hizi inaitwa Saudi Arabia. ni jambo kubwa la kiroho kwa Muislamu. Kikawaida, watu milioni 2-3 wanafanya hajj kila mwaka.

Msingi wa Kurani: Surah (Sura)al-Fatihah

Wasomi wanafikiria Surah al-Fatihah, sura ya kwanza ya Kurani, kuwa msingi wa Kurani. inasomwa kwenye kila sala katika lugha ya Kiarabu. Tafsiri inayofuata:

"Ninaomba kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Sifa njema (zote) ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe (vyote) . Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu. Mwenye kumiliki Siku ya Malipo. Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada. Tuongoze njia iliyonyooka(ya Uislamu). Njia ya (wale) uliowaneemesha; Siyo ya (wale) waliokasirikiwa wala ya (wale) waliopotea. "

kusikiliza usomaji wa Surah al-Fatiha bonyeza hapa

Msingi wa Mafunzo ya Muhammad

Wasomi wa zamani wa Uislamu wanachukulia mafunzo ya Mtume Muhammad katika hadithi kadhaa. Hadithi hizi za jumla zinagusa kila sehemu ya maisha yetu. Baadhi yake ni:

1)Kitendo kinahukumiwa kwa azimio lililopo nyuma yake.

2) Mungu ni msafi na hakubali kitu chochote labda kiwe safi na na Mungu amewalazimisha waaminio kwa Walicholazimisha mitume.

3)Sehemu ya tabia nzuri ya mtu katika Uislamu ni kuyaacha yasiyo muhusu.

4)Haamini mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake (katika Uislamu) kile anachojipendelea nafsi yake.

5)Mtu hatakiwi kujidhuru au Kuwadhuru wengine.

6)Usiruhusu mawazo yako katika maisha haya yawe kwaajili ya pato la kidunia na Mungu atakupenda. Usijali kwa walichonacho watu, na watakupenda.

Msingi wa Sheria ya kiislamu au Shariah

Msingi wa sheria ya kiislamu ni uhifadhi wa:

1)Dini

2)Maisha

3)Familia

4)Akili

5)Mali

6)Wasomi wa wakati huu wanapendekeza labda haki au uhuru kuwa aina ya sita.

Katika taswira ya Uislamu, zinajulikana kama "Muhimu" kwasababu zinachukuliwa ni muhimu kwa maisha ya binaadamu.

Katika kumalizia, kama mtu atauliza, nini msingi wa uislamu kwa maneno machache, jibu litakuwa, "Lipo kwenye neno Uislamu : kutumikia, kuabudu, na kumtii Mungu kwa kupenda."



Vielezi-chini:

[1] www.creeds.net

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.