Ukweli ni Mmoja (sehemu ya 2 kati ya 2)
Maelezo: Sehemu ya pili ya hoja yenye mantiki inayothibitisha kwamba ukweli ni kamili na sio tegemezi, kupitia uchunguzi wa mafunzo na maadili katika nyakati na sehemu mbalimbali.
- Na M. Abdulsalam (© 2006 IslamReligion.com)
- Iliyochapishwa mnamo 29 Nov 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 3,122 (wastani wa kila siku: 3)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Wale ambao wanaamini kuwa ukweli ni tegemezi na kwamba imani zote ni sahihi wanadhani kuwa haiwezekani kusema kwamba imani ya mtu ni makosa, kwa sababu dini kwao ni imani ya kibinafsi. Uongo wa taarifa hii ni dhahiri kabisa na hatuhitaji kuichunguza kwa undani ili kuithibitisha. Ikiwa dini moja linaamini kwamba Yesu alikuwa nabii wa uwongo, lingine linashikilia kuwa yeye ni Mungu, na lingine kwamba alikuwa mwanadamu aliyechaguliwa kuwa nabii, je zote zitawezaje kuwa kweli? Yesu, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, lazima awe ni miongoni mwa vitu vitatu vilivyotajwa hapo juu, na taarifa zote tatu haziwezi kuwa sahihi. Kwa hivyo, kwa kuwa ni moja tu ya taarifa hizi inaweza kuwa sahihi, yoyote ambayo imethibitishwa kama ya kweli huamua kwamba zingine lazima zichukuliwe kuwa za uwongo.
Hata hivyo, hii haimaanishi kuwa mtu hana haki ya kuamini kama watakavyo, kwani hii ni haki ambayo Mungu amewekeza kwa wanadamu wote. Lakini wakati huo huo, haimaanishi kwamba mtu lazima achukue hii kwa nguvu na kusema kwamba zote ni sahihi, na kwamba mtu hana haki ya kuunda uamuzi juu yao. Pia, kumpa mtu haki ya kuamini kile anachotaka hailazimishi kwamba wana haki ya kutekeleza au kutangaza imani hizi wazi, kwani sheria zinazotekelezwa katika jamii kila wakati huangalia athari za vitendo katika kiwango kikubwa cha jamii na ikiwa vitendo hivyo ni vya faida au kudhuru jamii kwa ujumla.
Kutokana na yale tuliyojadili, tunaweza kufikia hitimisho kwamba dini zote zinazopatikana leo ulimwenguni ni za uongo, au kwamba kuna moja kati yao ambayo ni ya Ukweli kamili; kwani ingawa dini mbalimbali zina mfanano, pia zina tofauti za kimsingi.
Ikiwa tungesema kwamba hakuna dini yoyote ulimwengu wa leo iliyo sahihi, basi hii itajumuisha kuamini kwamba Mungu hana haki kwa sababu alituacha tuzunguke duniani kwa dhambi na makosa bila kutuonyesha njia sahihi ya kufanya mambo, na hii haiwezekani kwa Mungu wa Haki. Kwa hivyo hitimisho la busara tu ni kwamba kuna Dini Moja ya Kweli, ambayo ina mwongozo katika nyanja zote za maisha, dini, maadili, jamii, na mtu binafsi.
Tunajuaje hii ndo dini moja ya kweli? Ni wajibu wa kila mtu kulichunguza jambo hili. Wanadamu waliumbwa kutimiza kusudi kubwa, sio tu kula, kulala na kwenda kutafuta chakula chao cha kila siku na kutosheleza tamaa zao. Ili kutimiza lengo hili, ni lazima mtu ajaribu kupata kusudi lake ni nini, na hii inaweza tu kufanywa kwa uchunguzi. Ikiwa mtu anaamini kwamba kuna Mungu, na kwamba Mungu lazima hakuwaacha wanadamu wakitangatanga katika upotofu, basi lazima watafute dini na njia ya maisha ambayo Mungu aliifunua. Kwa kuongezea, dini hii isingefichwa au kua ngumu kwa wanadamu kuipata au kuelewa, kwani hiyo ingeshinda kusudi la mwongozo. Pia, dini lazima iwe na ujumbe huo huo kwa wakati wote, kwani tulisema kwamba kila kitu kinarudi kwa ukweli mmoja kamili. Pia, dini hii haiwezi kuwa na uongo wowote au utata wowote, kwani uongo au kupingana katika jambo moja la dini hiyo inathibitisha uongo wa dini kwa ujumla, kwani tungetilia shaka uaminifu wa maandishi yake.
Hakuna dini nyingine inayotimiza masharti yaliyotajwa hapo juu isipokuwa dini ya Kiislamu, dini ambayo inalingana na asili ya mwanadamu, dini ambayo imehubiriwa na manabii wote tangu mwanzo wa mwanadamu. Dini zingine zinazopatikana leo, kama vile Ukristo na Uyahudi, ni mabaki ya dini iliyo letwa na manabii wakati wao, ambayo ilikuwa Uislamu. Walakini, baada ya muda, zimebadilishwa na kupotea, na kilichobaki leo kwa dini hizi ni mchanganyiko wa ukweli na uongo. Dini pekee ambayo imehifadhiwa na kuhubiri ujumbe ule ule ulioletwa na manabii wote ni dini ya Uislamu, dini moja ya kweli, ambayo inatawala nyanja zote za maisha ya wanadamu, dini, siasa, jamii, na mtu binafsi, na ni wajibu wa wanadamu wote kuchunguza dini hii, ili kujua ukweli wake, na kuifuata.
Ongeza maoni