Ukweli ni Mmoja (sehemu ya 1 kati ya 2)

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Sehemu ya kwanza ya hoja yenye mantiki inayothibitisha kwamba ukweli ni kamili na sio tegemezi, kupitia uchunguzi wa mafunzo na maadili katika nyakati na sehemu mbalimbali.

  • Na M. Abdulsalam (© 2006 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 29 Nov 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 27 Nov 2022
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 3,022
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

The_Truth_is_One_(part_1_of_2)_001.jpgMara nyingi wakati wa kujadili dini, mtu husikia taarifa kwamba hakuna aliye na haki ya kuhukumu imani ya mtu mwingine, au kwamba dini ni jambo la binafsi la mtu na hatuwezi kusema kuwa ni makosa au ni sawa. Katika historia yote, jamii zimejikita katika sheria na maadili yao juu ya "ukweli kamili" ambao wanaona ni "sawa", na hii inaweza kuwa ni matokeo ya maandishi ya nje yanayoonekana kama makuu, au ya tabia inayopatikana katika asili ya wanadamu ambayo huwafanya waone mambo fulani kuwa mazuri na mengine kuwa mabaya. Kwa kiwango kidogo, wanadamu wanaweza kuona vitu fulani kuwa vizuri na vibaya. Kwa mfano, wanadamu wote, wakiachwa kwa hali yao ya asili bila kupotoshwa kwa akili, wataona kinyesi na mkojo kuwa uchafu. Pia, vitendo vingine, kama kuiba, kuua na kusema uwongo pia hujulikana kuwa vibaya, wakati ukweli, uwazi, na heshima huonekana kuwa ni ya kujivunia. Hii ni matokeo ya tabia ambayo iliundwa kwa wanadamu wote, lakini kama ilivyoelezwa hapo juu, hisia hii ni ndogo.

Ikiwa mtu anasema kwamba hawana haki ya kuhukumu imani au matendo ya wengine, kwa kweli, wanajipinga wenyewe. Ikiwa ungeuliza wengi wa watu hawa ikiwa kuua watoto wachanga au kujiua ni sawa na inakubalika, kwa kawaida watajibu kwamba sio. Lakini tunapoangalia jamii zingine, kama dini zingine zinazopatikana Amerika ya Kati, mauaji ya watoto wachanga yalionekana kuwa njia ya kukaribia miungu yao. Pia leo, katika dini la Kihindu, ni sifa kwa mke kujiua baada ya kifo cha mumewe. Ikiwa wanaamini kweli kuwa dini ni kitu kilichoachwa kwa mtu binafsi na kwamba hakuna aliye na haki ya kuingilia kati au kuwahukumu, basi hii italazimisha kuruhusu kuua watoto wachanga kua ni jambo ambalo ni sawa kwa wale ambao wanaamini ni ya kusifiwa, na kwamba watu hawana haki ya kuwahukumu.

Ikiwa tungeleta suala hili kwa kiwango cha mtu binafsi, tungeona kwamba kila mtu ana maoni yake binafsi ya mema na mabaya, ikiwa mtazamo huu unategemea dini, sheria, utamaduni, au tafakari ya mtu binafsi. Mtu anaweza kuamini kwamba inakubalika kabisa kuzini wakati mwingine anaweza kudhani kuwa ni makosa. Mtu anaweza kuamini kuwa inaruhusiwa kwao kujiingiza katika mihadarati kwani ni miili yao, na wengine wanaweza kuamini kuwa ni jinai. Hakuna atakayeweza kusema kuwa kitu chochote ni sawa au kibaya, na watu wote wangeachwa kuamini kwa njia zao na kutekeleza kile wanachokiona kuwa "sahihi."

Ikiwa tungetekeleza imani hii katika jamii, tungekuwa na jamii inayotokana na machafuko, ambapo sheria hazingeweza kutungwa au kutekelezwa, kwani sheria inategemea kanuni kwamba mambo fulani yanapaswa kuwa ni mema na mengine ni mabaya. Ikiwa mtu angesema kwamba kuna ukweli fulani uliokubaliwa na wanadamu wote ambao unaweza kutumika kutunga sheria, taarifa hii ni ya kweli kwa kikomo fulani, kama tulivyosema kwamba wanadamu wote wana asili ya kujua mema kutoka kwa mabaya kwa hali finyu. Lakini kama inavyoonekana, tabia hii mara nyingi hupotoshwa kupitia mazingira, saikolojia, au sababu za kidini, kwa kuwa vitendo fulani ambavyo wakati mmoja vilionekana kuwa viovu na visivyo na maadili baadaye huonekana kuwa vyema na vinavyokubalika, na mambo mengine ambayo hayapatani na asili ya wanadamu yanaonekana kuwa ndo ufunguo za wokovu. Hii inaweza kuangaliwa katika jamii za kidemokrasia ambazo zinaweka sheria zao kuzingatia wingi. Tunaona kwamba mambo mengi ambayo yalichukuliwa kuwa ya kipuuzi kabisa au yasiyo na maadili sasa yanakubalika kijamii, kwa kiwango ambacho ikiwa mtu ana maoni tofauti kuhusu suala hilo, huonekana kama watengwa.

Kwa sababu hii, wanadamu hawawezi kuachwa kwa matakwa yao ya kutunga sheria kipi ni sahihi na sio sahihi. Hata katika jamii za dini moja ambazo zimeanzisha utengano wa dini na serikali, ingawa wanakubaliana na vitu ambavyo walishikilia kutoka kwa dini yao, wanatofautiana sana kwa kile kinachoonekana kuwa sahihi na sio sahihi katika jamii zao. Kinachochukuliwa kama umri halali wa idhini ya kufanya mapenzi nchini Ufaransa inachukuliwa kuwa ubakaji huko Amerika. Wakati utoaji mimba ni halali katika nchi moja, ni uhalifu katika nchi nyingine, na wakati ushoga unaonekana kama njia halali ya maisha katika jamii moja, inaonekana kama dhambi kubwa katika jamii nyingine.

Kwa hivyo ikiwa sasa tunasema ukweli ni kamili na mmoja na hauhusiani na kila mtu na jamii, basi swali linalofuata ni maadili gani ambayo yanaonyesha ukweli na ni nani wa kuamua? Je! Ni sheria gani ambazo zinapaswa kutekelezwa katika jamii? Je! Zinapaswa kuamuliwa na mawakili na majaji ambao wamefikia kiwango cha "ufahamu wa kisheria", wanasiasa ambao kawaida hufanya maamuzi kwa faida yao au faida ya nchi zao, au wanafalsafa ambao wamejua ukweli wa ulimwengu kupitia tafakari yao wenyewe? Kama ilivyoonekana hapo awali, wanadamu hawawezi kuachwa waamue maswala haya, isije ikawa na matokeo mabaya, kama inavyoonekana leo katika jamii nyingi zilizo na shida nyingi. Yule pekee aliye na haki ya kutunga sheria ya mema na mabaya ni yule ambaye alituumba na anajua ni nini kinachofaa kwetu, na huyo ni Mwenyezi Mungu aliyetukuka. Ni Mungu aliyeumba ulimwengu na ni Mungu aliyeweka mizani ya haki. Ni Mungu ambaye ni mkamilifu na ni Mungu ambaye hana makosa yoyote.

Mijadala yetu mingi imeshughulikia maswala ya imani ambayo yanahusu maadili na matendo, lakini la muhimu zaidi ni imani ambazo zinashughulika na Mungu, na hii itajadiliwa katika nakala ifuatayo.

Mbaya Nzuri zaidi

Ukweli ni Mmoja (sehemu ya 2 kati ya 2)

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Sehemu ya pili ya hoja yenye mantiki inayothibitisha kwamba ukweli ni kamili na sio tegemezi, kupitia uchunguzi wa mafunzo na maadili katika nyakati na sehemu mbalimbali.

  • Na M. Abdulsalam (© 2006 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 29 Nov 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 2,319
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Wale ambao wanaamini kuwa ukweli ni tegemezi na kwamba imani zote ni sahihi wanadhani kuwa haiwezekani kusema kwamba imani ya mtu ni makosa, kwa sababu dini kwao ni imani ya kibinafsi. Uongo wa taarifa hii ni dhahiri kabisa na hatuhitaji kuichunguza kwa undani ili kuithibitisha. Ikiwa dini moja linaamini kwamba Yesu alikuwa nabii wa uwongo, lingine linashikilia kuwa yeye ni Mungu, na lingine kwamba alikuwa mwanadamu aliyechaguliwa kuwa nabii, je zote zitawezaje kuwa kweli? Yesu, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, lazima awe ni miongoni mwa vitu vitatu vilivyotajwa hapo juu, na taarifa zote tatu haziwezi kuwa sahihi. Kwa hivyo, kwa kuwa ni moja tu ya taarifa hizi inaweza kuwa sahihi, yoyote ambayo imethibitishwa kama ya kweli huamua kwamba zingine lazima zichukuliwe kuwa za uwongo.

Hata hivyo, hii haimaanishi kuwa mtu hana haki ya kuamini kama watakavyo, kwani hii ni haki ambayo Mungu amewekeza kwa wanadamu wote. Lakini wakati huo huo, haimaanishi kwamba mtu lazima achukue hii kwa nguvu na kusema kwamba zote ni sahihi, na kwamba mtu hana haki ya kuunda uamuzi juu yao. Pia, kumpa mtu haki ya kuamini kile anachotaka hailazimishi kwamba wana haki ya kutekeleza au kutangaza imani hizi wazi, kwani sheria zinazotekelezwa katika jamii kila wakati huangalia athari za vitendo katika kiwango kikubwa cha jamii na ikiwa vitendo hivyo ni vya faida au kudhuru jamii kwa ujumla.

Kutokana na yale tuliyojadili, tunaweza kufikia hitimisho kwamba dini zote zinazopatikana leo ulimwenguni ni za uongo, au kwamba kuna moja kati yao ambayo ni ya Ukweli kamili; kwani ingawa dini mbalimbali zina mfanano, pia zina tofauti za kimsingi.

Ikiwa tungesema kwamba hakuna dini yoyote ulimwengu wa leo iliyo sahihi, basi hii itajumuisha kuamini kwamba Mungu hana haki kwa sababu alituacha tuzunguke duniani kwa dhambi na makosa bila kutuonyesha njia sahihi ya kufanya mambo, na hii haiwezekani kwa Mungu wa Haki. Kwa hivyo hitimisho la busara tu ni kwamba kuna Dini Moja ya Kweli, ambayo ina mwongozo katika nyanja zote za maisha, dini, maadili, jamii, na mtu binafsi.

Tunajuaje hii ndo dini moja ya kweli? Ni wajibu wa kila mtu kulichunguza jambo hili. Wanadamu waliumbwa kutimiza kusudi kubwa, sio tu kula, kulala na kwenda kutafuta chakula chao cha kila siku na kutosheleza tamaa zao. Ili kutimiza lengo hili, ni lazima mtu ajaribu kupata kusudi lake ni nini, na hii inaweza tu kufanywa kwa uchunguzi. Ikiwa mtu anaamini kwamba kuna Mungu, na kwamba Mungu lazima hakuwaacha wanadamu wakitangatanga katika upotofu, basi lazima watafute dini na njia ya maisha ambayo Mungu aliifunua. Kwa kuongezea, dini hii isingefichwa au kua ngumu kwa wanadamu kuipata au kuelewa, kwani hiyo ingeshinda kusudi la mwongozo. Pia, dini lazima iwe na ujumbe huo huo kwa wakati wote, kwani tulisema kwamba kila kitu kinarudi kwa ukweli mmoja kamili. Pia, dini hii haiwezi kuwa na uongo wowote au utata wowote, kwani uongo au kupingana katika jambo moja la dini hiyo inathibitisha uongo wa dini kwa ujumla, kwani tungetilia shaka uaminifu wa maandishi yake.

Hakuna dini nyingine inayotimiza masharti yaliyotajwa hapo juu isipokuwa dini ya Kiislamu, dini ambayo inalingana na asili ya mwanadamu, dini ambayo imehubiriwa na manabii wote tangu mwanzo wa mwanadamu. Dini zingine zinazopatikana leo, kama vile Ukristo na Uyahudi, ni mabaki ya dini iliyo letwa na manabii wakati wao, ambayo ilikuwa Uislamu. Walakini, baada ya muda, zimebadilishwa na kupotea, na kilichobaki leo kwa dini hizi ni mchanganyiko wa ukweli na uongo. Dini pekee ambayo imehifadhiwa na kuhubiri ujumbe ule ule ulioletwa na manabii wote ni dini ya Uislamu, dini moja ya kweli, ambayo inatawala nyanja zote za maisha ya wanadamu, dini, siasa, jamii, na mtu binafsi, na ni wajibu wa wanadamu wote kuchunguza dini hii, ili kujua ukweli wake, na kuifuata.

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.