Je, Tunaweza Kumwona Mungu?

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Swali la iwapo Mungu anaweza kuonekana katika maisha haya kwa Mitume, watakatifu, na watu wa kawaida, na kama Ataonekana Akhera.

  • Na IslamReligion.com
  • Iliyochapishwa mnamo 03 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 3,101 (wastani wa kila siku: 3)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Can_we_see_God_001.jpgAkili ya mwanadamu ni maajabu ya kweli, lakini katika maeneo fulani ina mipaka. Mungu ni tofauti na chochote ambacho akili ya mwanadamu inaweza kufikiria au kuwaza, kwa hivyo akili itachanganyikiwa ikiwa inajaribu kumfananisha Mungu. Hata hivyo, inawezekana kuelewa sifa za Mungu ambazo hazihitaji mtu kujenga picha zozote akilini mwake. Kwa mfano, moja ya majina ya Mungu ni al-Ghaffar, ambayo ina maana kwamba anasamehe dhambi zote. Kila mtu anaweza kuelewa hili kwa urahisi kwa sababu hivyo ndivyo akili ya mwanadamu inavyoweza kumfikiria Mungu. Mafundisho ya Kiyahudi na ya Kikristo kuhusu Mungu yamechanganywa kwa sehemu flani kwa sababu ya uelewa usio sahihi wa suala hili. Torati ya Kiyahudi inafundisha kwamba Mungu ni kama mwanadamu,

“Ndipo Mungu akasema, ‘Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; Mungu akamfanya mtu kwa mfano wake.’” (Genesis 1:26-27)

Zaidi ya hayo, makanisa fulani yana sanamu au picha za mzee mwenye ndevu nyeupe zinazo muonyesha kama Mungu. Baadhi ya hizi zilitolewa na watu kama Michelangelo ambaye alionyesha Uso na mkono wa Mungu - mzee mwenye sura ngumu - katika picha za kuchora.

Kutoa picha za Mungu katika Uislamu ni jambo lisilowezekana, na ni sawa na ukafiri, kama vile Mungu anatuambia katika Kurani kwamba hakuna chochote kinachofanana Naye:

“Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.” (Kurani 42:11)

“Wala hana anaye fanana naye hata mmoja.” (Kurani 112:4)

Ombi la Musa Kumwona Mungu

Macho hayawezi kubeba maono ya Mungu. Anatuambia katika Kurani:

“Macho hayamfikilii bali Yeye anayafikilia macho. Naye ni Mjuzi, Mwenye habari.” (Kurani 6:103)

Musa, ambaye Mungu alizungumza naye na kumpa miujiza mikubwa, alichaguliwa na Mungu kuwa Nabii wake. Inasemekana kwamba alifikiri kwamba, kwa kuwa Mungu alikuwa akizungumza naye, huenda angeweza kumwona Mungu kihalisi. Hadithi hiyo iko kwenye Kurani, ambapo Mwenyezi Mungu anatueleza kilichotokea:

“Na alipo kuja Musa kwenye miadi yetu, na Mola wake Mlezi akamsemeza, alisema: ‘Mola wangu Mlezi! Nionyeshe nikutazame.’ (Mwenyezi Mungu) akasema: ‘Hutoniona. Lakini utazame huo mlima. Ukibaki pahala pake basi utaniona.’ Basi alipo jionyesha Mola Mlezi wake kwa mlima, aliufanya uvurugike, na Musa akaanguka chini amezimia. Alipo zindukana alisema: ‘Subhanaka, Umetakasika! Natubu kwako, na mimi ni wa kwanza wa Waumini.’” (Kurani 7:143)

Mungu aliweka wazi kwamba hakuna mtu yeyote, hata nabii mkuu Musa, anayeweza kustahimili maono ya Mungu, kwa maana Mungu ni mkuu mno kuweza kuonekana na macho ya wanadamu katika maisha haya. Kwa mujibu wa Kurani, Musa alitambua ombi lake lilikuwa na makosa; kwa hivyo, aliomba msamaha kutoka kwa Mungu kwa kuomba.

Je Mtume Muhammad Alimuona Mungu Katika Maisha Haya?

Mtume Muhammad alisafiri katika safari ya ajabu katika mbingu na kukutana na Mungu. Watu walifikiri kwamba kwa vile Mtume Muhammad alizungumza na Mungu katika safari hiyo, huenda alimuona Mungu pia. Mmoja wa maswahaba, Abu Dahrr, alimuuliza kuhusu hilo. Mtume akajibu:

“Kulikuwa na nuru tu, ningewezaje kumwona?” (Saheeh Muslim)

Ni mwanga gani aliouona? Mtume akaeleza:

“Hakika Mwenyezi Mungu halali wala haifai kwake kulala. Yeye ndiye anayeshusha mizani na kuziinua. Amali za usiku hupanda kwake kabla ya amali za mchana na za mchana kabla zile za usiku, na pazia lake ni nuru.”(Saheeh Muslim)

Maono ya Mungu katika Uzoefu wa Kiroho

Baadhi ya watu, ikiwa ni pamoja na wengine wanaodai kuwa Waislamu, wanaripoti matukio ya kiroho ambapo wanadai kuwa wamemwona Mungu. Matukio ya kawaida yaliyoripotiwa pia yanajumuisha kuona mwanga, au mtu mzuri ameketi kwenye kiti cha enzi. Kwa upande wa Waislamu, uzoefu kama huo kwa kawaida huambatana na kuacha desturi za kimsingi za Kiislamu kama vile swala na saumu, chini ya maoni potofu kwamba vitendo hivyo ni vya watu wa kawaida tu ambao hawakuwa na uzoefu wa aina yao.

Kwa hivyo Uislamu unafundisha nini kuhusu hili? Uislamu unatufundisha kwamba ni Shetani anayejifanya kuwa Mungu ili kuwahadaa watu wajinga wanaoamini matukio hayo na kupotea. Moja ya misingi mikuu ya Uislamu ni kwamba sheria iliyoteremshwa kwa Mtume Muhammad haiwezi kubadilishwa au kufutwa. Mungu hajahalalisha kwa baadhi ya watu kwa kile Alichoharamisha kwa wengine, wala hawasilishi Sheria Yake kupitia matukio kama hayo kwa watu. Badala yake, sheria ya kimungu inafichuliwa kupitia njia sahihi ya ufunuo kwa mitume, njia ambayo ilifungwa baada ya ujio wa mtume Muhammad, wa mwisho kati ya manabii wa Mungu.

Kumwona Mungu katika Maisha ya Baadaye

Katika mafundisho ya Kiislamu, Mungu hawezi kuonekana katika maisha haya, lakini waumini watamwona Mungu katika maisha yajayo; hata hivyo, Mungu hataonekana kwa ujumla. Hili limeelezwa kwa uwazi katika Kurani na Sunnah. Mtume akasema,

"Siku ya Kiyama ndiyo siku ya kwanza ambayo jicho lolote litamtazama Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu na Aliyetukuka."[1]

Akielezea matukio ya Siku ya Kiyama, Mwenyezi Mungu anasema katika Kurani:

“Zipo nyuso siku hiyo zitao ng'ara, Zinamwangallia Mola wao Mlezi.” (Kurani 75:22-23)

Mtume aliulizwa iwapo tutamuona Mungu siku ya kiyama. Akajibu, “Je, unaumizwa kwa kuutazama mwezi unapojaa?”[2] ‘Hapana,’ wakajibu. Kisha akasema: “Hakika wewe utamwona vile vile.” Katika hadithi nyingine, Mtume amesema: “Hakika kila mmoja wenu atamuona Mwenyezi Mungu siku mtakayokutana naye, wala hakutakuwa na pazia wala mtafsiri baina yake na nyinyi.[3] Kumwona Mungu kutakuwa ni neema ambayo ni nyongeza ya Pepo kwa watu watakaokaa humo. Kwa hakika, shangwe ya kumwona Mungu kwa mwamini itakuwa kubwa kuliko shangwe zote za Peponi zikiunganishwa pamoja. Makafiri, kwa upande mwingine, watanyimwa kumuona Mungu, na hii itakuwa adhabu kubwa kwao kuliko maumivu na mateso yote ya Jahannamu yakiunganishwa pamoja.



Rejeleo la maelezo:

[1] Darqutni, Darimi

[2] Saheeh Al-Bukhari, Saheeh Muslim

[3] Saheeh Al-Bukhari

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.