Hadithi ya Uumbaji (sehemu ya 1 kati ya 2)

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Hadithi kuu ya asili ya uumbaji kutoka kwa mtazamo wa Kosmolojia ya Kiislamu, kukiri kwamba Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Nakala hii pia inazungumza kuhusu Kiti Kizuri cha Enzi, Kiti cha Chini, na Kalamu.

  • Na Imam Mufti (© 2016 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 08 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 6,320 (wastani wa kila siku: 6)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Mungu Aliumba Kila Kitu

Story_of_Creation_(Part_1_of_2)._001.jpgKwa hivyo yote yalianzaje? Mungu. Hakuna kingine. Mtume wa Uislamu, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, aliuliza, "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, alikuwa wapi Mola wetu kabla hajaumba viumbe vyake?" Akasema: "Hapana kilicho kuwepo ila Yeye tu, kisicho chini Yake wala kilicho juu Yake."[1]

Fikiria jinsi ilivyo ya kushangaza, kimsingi, inatuambia kwamba hakuna chochote ila Mungu anayestahili kweli; uumbaji unamhitaji Mungu na si kitu kingine maana hapo mwanzo alikuwepo Mungu bila kingine.

Mwenyezi Mungu anasema katika Kurani:

"Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu, na Yeye ndiye Mlinzi juu ya kila kitu." (Kurani 39:62)

Kwa hivyo kila kitu isipokuwa Mwenyezi Mungu kiliumbwa Naye, kiko chini ya himaya Yake na uhifadhi Wake, na Akakifanya kiwepo.

Jubayr, aliyeishi zama za Mtume Muhammad anajieleza, akisema, “Nilikuwa mmoja wa maadui wakubwa wa Mtume na akasema, “Nilimchukia kuliko binadamu yeyote juu ya uso wa dunia hii,” lakini baadaye kuna kitu cha ajabu ilitokea. "Wakati mmoja niliingia msikitini na nikamsikia Mtume akisoma aya kutoka Sura ya at-Toor (Kurani 52:35-36), ‘Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana na yakini!’"

Jubayr anasema kwamba wakati Mtume alivyosema ivyo, ingawa hakukubali Uislamu rasmi hadi baadaye katika maisha yake, "imani iliingia moyoni mwangu. Nilijua wakati huo kwamba hakuna uwezekano kabisa kwamba hakuna Mungu.!"

Ukikaa mwenyewe na ukapitia mchakato wa kuondoa uwezekano wa jinsi sisi na kila kitu kinacho tuzunguka tuko hapa, utagundua kuwa hakuna njia nyingine ya kuelezea isipokuwa ni Mungu.

Uumbaji wa Maji, Kiti cha Enzi (Arsh) na Kiti cha Miguu (Kursi)

Mtume Muhammad amesema: "Hakukuwa na chochote ila Yeye, kisichokuwa chini Yake na chochote juu Yake. Kisha Akaumba kiti Chake cha enzi juu ya maji."[2]

Mtume anatuambia kwamba kulikuwa na Mungu kwanza na hakuna kitu kingine. Kisha, Mungu akaumba maji na Kiti cha enzi (Arsh). Viliumbwa bila ya Malaika yeyote na viliumbwa kabla ya kuumbwa kwa mbingu na ardhi. Mtume Muhammad alisema: "Kulikuwa na Mungu, na hakuna kitu kingine zaidi yake, na kiti Chake cha enzi kilikuwa juu ya maji. Aliandika kila kitu katika Kitabu (mbinguni) na aliumba mbingu na ardhi."[3]

Mwenyezi Mungu ametaja mara nyingi ndani ya Kurani kwamba Yeye ni Mola wa Kiti cha enzi, kwa sababu ni moja ya vitu vya kwanza kabisa alivyoviumba na adhimu zaidi.

Kursi ni Kiti cha chini ambacho ni kama ngazi ya kiti cha enzi na Mungu yuko juu ya kiti cha enzi, lakini hakuna kinachofichika Kwake. Katika aya kubwa kabisa ya Kurani, inayojulikana kwa Kiarabu kama Ayah al-Kursi, au "Aya ya Kiti cha chini" kabla Mungu hajataja Kiti Chake cha chini, Anataja ujuzi Wake." (Kurani 2:255).

Kursi chake, Kiti cha chini, ni peke yake ndiye ana mbingu na ardhi chini yake (Kurani 2:255). Mtume Muhammad alisema, "uhusiano wa Kiti cha chini na Kiti cha enzi si zaidi ya pete ya chuma iliyotupwa kwenye jangwa la wazi duniani."[4] Pia, Ibn Abbas alisema kwamba kama Kursi, Kiti cha chini, kinazunguka mbingu na ardhi yote, basi vipi kuhusu Kiti cha Enzi? Hatuna dalili ya ukubwa wa Kiti cha Enzi na ni dhahiri hatuwezi kukadiria ukuu wa Mungu Mwenyewe.

Mungu hayuko mbali; Anasisitiza katika Kurani yote kwamba Yuko pamoja nasi popote pale tulipo. Katika Sura ya al-Hadid (Sura ya 57), mara tu baada ya Mwenyezi Mungu kutuambia kwamba alinyanyuka juu ya Kiti Chake cha enzi, anatuambia kwamba Anajua kila kitu kinachoingia na kutoka katika ardhi, kila kinachoteremka kutoka mbinguni na kinachopanda humo. Kwa kifupi, Yeye anajua undani wa kila kitu (Kurani 57:4). Tunajua kuwa Mwenyezi Mungu yuko juu ya Kiti chake cha Enzi, lakini Yeye ni Muweza wa kila kitu, na ujuzi Wake umezunguka kila kitu.

Zaidi ya hayo, Mungu anazungumza kuhusu malaika wakuu wanaobeba Kiti cha Enzi. Ni viumbe wakubwa wa ajabu kutoka kwa malaika bora wa Mungu. Siku ya Hukumu, Mungu anatuambia kutakuwa na Malaika wanane watakao beba Kiti chake che Enzi (Kurani 69:17). Mtume akasema: “Nimeruhusiwa kusema kuhusu mmoja wa Malaika wa Mungu, Mwenyezi, Mwenye Nguvu, ambaye ni miongoni mwa wabeba Kiti cha Enzi na (kukwambia) umbali uliopo baina ya sikio lake na bega lake ni safari ya miaka mia saba." (Abu Dawud) Pia imepokewa kwa maneno haya, "Umbali ni (kama) ndege anayeruka miaka mia saba." (Ibn Abi 'Asim)

Malaika hao wanafanya nini?

Mungu anatuambia kua wale wanao beba Kiti chake cha Enzi, na wanao kizunguka, wanamsabihi na kumhimidi Mola wao Mlezi, na wanamuamini, na wanawaombea msamaha walio amini kwa kusema: "Mola wetu Mlezi! Umekienea kila kitu kwa rehema na ujuzi. Basi wasamehe walio tubu na wakaifuata Njia yako, na waepushe na adhabu ya Jahannamu." (Kurani 40:7)

Wanamtakasa Mwenyezi Mungu na kutangaza ukamilifu wa Mwenyezi Mungu ili kuonyesha kwamba Mwenyezi Mungu hategemei Kiti cha Enzi na hategemei wanaobeba Kiti cha Enzi. Mungu hahitaji Kiti cha Enzi; Mwenyezi Mungu hawahitaji wanaobeba Kiti cha Enzi.

Kalamu

Baada ya kuumba maji na Kiti cha Enzi, Mungu aliumba Kalamu. Mtume anaposema kuwa Mwenyezi Mungu ameumba Kalamu, anasema kwamba Kiti chake cha Enzi kiliwekwa juu ya maji, kwamba kulikuwa na safu ya maji chini ya Kiti cha Enzi cha Mungu.

"Mwenyezi Mungu alipanga vipimo vya uumbaji miaka elfu hamsini kabla ya kuumba mbingu na ardhi huku Kiti chake cha Enzi kikiwa juu ya maji."[5]

Vipi ni vipimo vya kalamu? Je, inaonekanaje? Hatuna wazo kabisa.

Mtume akasema, “Mwenyezi Mungu aliiambia Kalamu: ‘Andika.’ Ikasema: ‘Ewe Mola, niandike nini?’ Akasema: ‘Andika hukumu za kila kitu mpaka Saa ianze.'"[6]



Rejeleo la maelezo:

[1] Tirmidhi, Abu Daud. Imeorodheshwa kama Sahih ya Tabari na hasan ya Tirmidhi, Dhahabi, na Ibn Taimiyyah.

[2] Tirmidhi, Ibn Majah

[3] Saheeh Al-Bukhari

[4] Tafsir Tabari

[5] Saheeh Muslim

[6] Abu Dawud

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.