Je, ni Vigezo gani vya Nabii wa Kweli?

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Kutazama katika aya za Biblia ambazo zimeweka vigezo vya ukweli kwenye madai ya Utume.

 • Na Imam Mufti
 • Iliyochapishwa mnamo 24 Nov 2021
 • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
 • Ilichapishwa: 0
 • Imetazamwa: 2,562 (wastani wa kila siku: 3)
 • Ukadiriaji: bado hakuna
 • Imekadiriwa na: 0
 • Imetumwa kwa barua pepe: 0
 • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Miale kutoka kwenye Taa ile ile

Swali la kawaida la kumwuliza mtu anayemwamini nabii yeyote ni: ‘Ni vipi vigezo vya kumwamini kwako?’ Vigezo vinavyoeleweka vitakuwa:

(i) ushahidi wa madai yake.

(ii) uthabiti katika mafundisho yake (kuhusu Mungu, maisha ya baadaye, na masuala kama hayo ya imani)

(iii) kufanana kwa mafundisho ya manabii wa mwanzo.

(iv) Uadilifu: lazima awe mtu mwenye maadili ya hali ya juu.

Biblia inaunga mkono vigezo vyetu. Agano la Kale linasema hivi juu ya nabii wa uongo:

1. Anajifanya kutumwa na Mungu.[1]

2. Kuonekana mwenye tamaa,[2] mlevi,[3] asiye na maadili na asiye na adabu,[4] kusukumwa na roho za shetani.[5]

3. Utabiri uwongo,[6] anaongea uwongo kwa jina la Mungu,[7] kwa moyo wake,[8] ndani ya jina la miungu ya uwongo.[9]

4. Mara nyingi hufanya uaguzi na uchawi.[10]

5. Huwaongoza watu kwenye makosa,[11] hufanya kusahau jina la Mungu,[12] hufundisha unajisi na dhambi,[13] na kudhulumu[14]

Agano Jipya linasema vigezo vya Yesu vya kutambua manabii wa uongo:

"Jihadharini na manabii wa uongo. Wao huja kwenu wakionekana kama kondoo kwa nje, lakini kwa ndani ni mbwamwitu wakali. Mtawatambua kwa matendo yao. Je, watu huchuma zabibu katika miti ya miiba, au tini katika mbigili? La! Basi, mti mzuri huzaa matunda mazuri, na mti mbaya huzaa matunda mabaya. "[15]

Tunajifunza yafuatayo

(i) utabiri utaendelea baada ya Yesu

(ii) Kuwa makini na manabii wa uwongo

(iii) vigezo vya kumtambua nabii wa uongo ni matunda yake, hiyo ni kazi au matendo yake.[16]

Kama ilivyoelezwa hapo mwanzo, Muhammad alieleza bila shaka, ‘Mimi ni Mtume wa Mungu.’ Mtu akitathmini madai yake kwa vigezo vilivyotajwa hapo juu, ataona yanakidhi vigezo kikamilifu.

Katika mafundisho ya Uislam, manabii wote wanaunda udugu wa kiroho wa ndugu wenye ‘baba’ mmoja, lakini ‘mama' tofauti. ‘Baba’ ni utume na umoja wa Mungu, ‘mama’ ni Sheria tofauti walizozileta. Akisisitiza udugu wa kiroho wa mitume wote, Mtume Muhammad alisema:

"Mimi wa karibu kuliko watu wote kwa mwana wa Maryamu (Yesu). Manabii ni ndugu wa baba, mama zao ni tofauti, lakini dini yao ni moja." (Saheeh Al-Bukhari, Saheeh Muslim)

Manabii wote ni ‘miale’ kutoka kwenye‘Taa’ moja: ujumbe mkuu wa manabii wote katika nyakati zote ulikuwa kufanya ibada kwa Mungu pekee. Ndio maana Uislamu unaona kumkana mtume mmoja ni sawa na kuwakana wote. Kurani inasema:

"Hakika wale wanao mkataa Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wanataka kufarikisha baina ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake, kwa kusema: Wengine tunawaamini na wengine tunawakataa. Na wanataka kushika njia iliyo kati kati ya haya. Hao ndio makafiri kweli. Na tumewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha. Na walio muamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake, wala wasimfarikishe yeyote kati yao, hao atawapa ujira wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, na Mwenye kurehemu." (Kurani 4:150-152)

Kukanusha utume wa Muhammad ni sawa na kuwakana mitume wote. Utume wa Muhammad unajulikana kama utume wa Musa na Yesu unavyojulikana: ripoti nyingi za miujiza yao ambazo zimetufikia. Kitabu kilicholetwa na Muhammad (Kurani) kimehifadhiwa kikamilifu, na Sheria yake ni kamili na inatumika katika ulimwengu wa leo. Musa alileta Sheria na haki, Yesu alileta neema na mabadiliko. Muhammad alichanganya kati ya Sheria ya Musa na neema ya Yesu.

Kama mtu angesema, ‘alikuwa muongo,’ wengine wanafaa zaidi kushtakiwa kwa shtaka hili. Kwa hiyo, kumkana Muhammad ni kuwakana mitume yao wenyewe. Ikiwa mtu mwenye akili timamu anatazama nyota mbili angavu, lazima akiri kwamba zote mbili ni nyota, hawezi kuisema moja, ‘Ndiyo, hii ni nyota angavu,’ alafu aikane nyingine! Kufanya hivyo kutakuwa kukana ukweli na uwongo.

Tengeneza jedwali la manabii wote unaowaamini. Anza kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho unaowaamini. Jibu maswali yafuatayo:

Je, ni ushahidi gani ninaoamini kuwa alikuwa ni nabii wa kweli?

Je, kazi ya nabii ilikuwa ipi kwa maneno yake mwenyewe?

Je, alileta Sheria? Je, Sheria yake inatumika hadi leo?

Alileta andiko gani? Je, maudhui na maana yake ni ipi?

Je, andiko limehifadhiwa katika lugha ya awali ambayo ilifunuliwa nayo? Je, inachukuliwa kuwa na mamlaka ya kifasihi, isiyo na mikanganyiko ya ndani?

Unajua nini kuhusu maadili na uadilifu wake?

Linganisha manabii wote ulioorodhesha kisha ujibu maswali yale yale kuhusu Muhammad. Kisha jiulize, ‘Je, ninaweza kumwondoa Muhammad katika orodha yangu kwa uaminifu kwa sababu hafikii vigezo kama manabii wengine?’ Haitachukua jitihada nyingi sana kugundua kwamba ushahidi wa utume wa Muhammad ni wenye nguvu zaidi na wenye kusadikisha zaidi.

Je, mtu mwenye shaka anahitaji kufikiria jambo lisilo la kawaida kuhusu madai ya Muhammad kuwa nabii? Ni lini Mungu alitangaza mwisho wa kutuma nabii kabla yake? Nani aliamua kuwa hakutakuwa na mawasiliano yoyote ya kimungu na wanadamu? Bila ushahidi wa kuzuia ufunuo wa Mungu, ni kawaida kukubali mwendelezo wa ufunuo:

"Hakika Sisi tumekutuma wewe kwa Haki, kuwa ni mbashiri na mwonyaji. Na hapana umma wowote ila ulipata mwonyaji kati yao." (Kurani 35:24)

"Kisha tukawatuma Mitume wetu, mmoja baada ya mmoja. Kila umma alipo wafikia Mtume wao walimkanusha. Tukawafuatanisha hawa baada ya hawa, na tukawafanya ni hadithi za kusimuliwa. Wakapotelea mbali watu wasio amini!" (Kurani 23:44)

Hii ni kweli hasa pale ukweli ulipopotoshwa na Mayahudi na Wakristo, Wakristo wakidai Yesu ni mwana wa Mungu na Wayahudi wakimwita mwana wa haramu wa Yusufu Seremala. Muhammad alileta ukweli: Yesu alikuwa nabii mtukufu wa Mungu aliyezaliwa kwa kimuujiza na bikira. Matokeo yake ni kwamba Waislamu wanamwamini Yesu na wanampenda, wala hawapiti mipaka kama Wakristo, wala hawamdharau kama Mayahudi.Vieleze-chini:

[1]Yer 23: 17,18,31

[2]Mik 3:11

[3]Isa 28:7

[4]Yer 23:11,14

[5]1Waf 22:21,22

[6]Yer 5:31

[7] Yer 14:14

[8]Yer 23:16,26; Eze 13:2

[9]Yer 2:8

[10]Yer 14:14; Eze 22:28; Act 13:6

[11] Yer 23:13; Mic 3:5

[12] Yer 23:27

[13]Yer 23:14,15

[14]Eze 22:25

[15] Mathayo 7:15-17 (Toleo la King James)

[16]Kulingana na ‘Vine’s Expository Dictionary of New Testament Words.’

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

 • (Haitaonyeshwa kwa umma)

 • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

  Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.