Miujiza ya Muhammad (sehemu ya 2 kati ya 3)

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Kugawanywa kwa mwezi, na safari ya Mtume kwenda Yerusalemu na kupaa Mbinguni.

  • Na IslamReligion.com
  • Iliyochapishwa mnamo 10 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 1
  • Imetazamwa: 4,748 (wastani wa kila siku: 5)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Kugawanywa kwa Mwezi

Moja ya nyakati ambapo Mungu alifanya miujiza kwa mkono wa Mtume ilikuwa wakati watu wa Makkah walitaka kuona muujiza kutoka kwa Muhammad ili kuthibitisha ukweli wake. Mungu aliugawanya mwezi katika vipande viwili tofauti na kisha ukaunganisha tena. Kurani iliandika tukio hilo:

“Saa imekaribia, na mwezi umepasuka!” (Kurani 54:1)

Mtume Muhammad alikuwa akisoma aya hizi za Kurani katika makundi makubwa ya sala ya Ijumaa ya kila juma na sala za Idi mara mbili kwa mwaka.[1] Kama tukio hilo lisingetokea, Waislamu wenyewe wangeitilia shaka dini yao na wengi wangeiacha! Watu wa Makkah wangesema, ‘Haya, Nabii wenu ni mwongo, mwezi haukugawanyika, na hatujawahi kuuona ukigawanyika!’ Badala yake, Waumini walikua na nguvu zaidi katika imani yao na maelezo pekee ambayo watu wa Makkah wangeweza kujanayo ni, 'ulikuwa ni uchawi '

“Saa imekaribia, na mwezi umepasuka! Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu uchawi tu unazidi kuendelea.Na wamekanusha na wamefuata matamanio yao. Na kila jambo ni lenye kuthibiti.” (Kurani 54:1-3)

Kugawanywa kwa mwezi kunathibitishwa kupitia ushuhuda wa mashahidi uliyopitishwa kwa wasomiwengi wanaoaminika kiasi kwamba inakuwa haiwezekani kuwa ya uwongo (hadith mutawatir).[2]

Mtu mwenye shaka anaweza kuuliza, je, tuna ushahidi wowote huru wa kihistoria kupendekeza mwezi uliwahi kupasuliwa? Baada ya yote, watu ulimwenguni pote walipaswa kuona tukio hili la ajabu na kulirekodi.

Majibu ya swali hili ni mawili

Moja, watu ulimwenguni kote wasingeweza kuiona kama ingekuwa mchana, usiku wa manane, au asubuhi na mapema katika sehemu nyingi za ulimwengu. Jedwali lifuatalo litampa msomaji wazo la nyakati za dunia zinazolingana na saa 9:00 alasiri saa za Makka:

Nchi

Muda

Makka

9:00 pm

India

11:30 pm

Perth

2:00 am

Reykjavik

6:00 pm

Washington D.C.

2:00 pm

Rio de Janeiro

3:00 pm

Tokyo

3:00 am

Beijing

2:00 am

Pia, sio kawaida kwamba idadi kubwa ya watu katika nchi zilizo karibu wangekuwa wakitazama mwezi kwa wakati uleule. Hawakuwa na sababu. Hata kama mtu fulani aliuona, haimaanishi kwamba watu walimwamini na kuweka rekodi yake, wakati watu wengi wa wakati huo hawakuhifadhi historia yao wenyewe kwa maandishi.

Mbili, hakika tuna uthibitisho huru na wa kushangaza kabisa, wa kihistoria wa tukio kutoka kwa mfalme wa Kihindi wa wakati huo.

Kerala ni jimbo la India. Jimbo hilo lina urefu wa maili 360 (kilomita 580) kando ya Pwani ya Malabar upande wa kusini magharibi mwa rasi ya India.[3] Mfalme Chakrawati Farmas wa Malabar alikuwa mfalme wa Chera, Cheraman perumal wa Kodungallure. Imerekodiwa kuwa aliona mwezi ukigawanyika. Tukio hilo limeandikwa katika andiko lililohifadhiwa katika Maktaba ya Ofisi ya India, London, nambari ya kumbukumbu: Arabic, 2807, 152-173.[4] Kundi la wafanyabiashara Waislamu waliokuwa wakipita Malabar wakielekea Uchina walizungumza na mfalme kuhusu jinsi Mungu alivyomuunga mkono nabii wa Kiarabu kwa muujiza wa kugawanyika kwa mwezi. Yule mfalme alishtuka akasema kuwa ameiona kwa macho yake pia, akampa mwanawe msaidizi, na akaondoka kwenda Uarabuni kukutana na Mtume ana kwa ana. Mfalme wa Malabari alikutana na Mtume, akatoa shuhuda hizo mbili za imani, akajifunza misingi ya imani, lakini alifariki dunia akiwa njiani kurudi na akazikwa katika mji wa bandari wa Zafar, Yemen.[5]

Inasemekana kuwa kikosi hicho kiliongozwa na Mwislamu, Malik ibn Dinar, na kuendelea hadi Kodungallure, mji mkuu wa Chera, na kujenga msikiti wa kwanza, na wa zamani zaidi wa India, katika eneo hilo mnamo 629 BK ambao upo hadi leo.

The_Miracles_of_Muhammad_(part_2_of_3)_001.jpg

Picha ya kabla ya ukarabati wa Msikiti wa Cheraman Juma Masjid, msikiti mkongwe zaidi nchini India ulioanzia 629 BK. Picha kwa hisani ya www.islamicvoice.com.

Habari za kusilimu kwake zilifika Kerala ambapo watu waliukubali Uislamu. Watu wa Lakshadweep na Moplas (Mapillais) kutoka jimbo la Calicut la Kerala waliukubali uislam tangu siku hizo.

The_Miracles_of_Muhammad_(part_2_of_3)_002.jpg

Cheraman Juma Masjid, iliyopewa jina la Muislamu wa kwanza wa India aliyesilimu, Cheraman perumal Chakrawati Farmas, baada ya ukarabati. Picha kwa hisani ya www.indianholiday.com.

Kuonekana India na kukutana kwa mfalme wa India na Mtume Muhammad pia kunaripotiwa na vyanzo vya Kiislamu. Mwanahistoria mashuhuri wa Kiislamu, Ibn Kathir, anataja kugawanyika kwa mwezi kuliripotiwa katika sehemu za India.[6] Pia, vitabu vya Hadith vimeandika kuwasili kwa mfalme wa Kihindi na kukutana kwake na Mtume. Abu Sa’id al-Khudri, sahaba wa Mtume Muhammad, anasema:

“Mfalme wa Kihindi alimpa Mtume zawadi ya mtungi wa tangawizi. Maswahaba wakala kipande kwa kipande. nilitafuna pia.”[7]

Kwa hiyo mfalme alichukuliwa kama ‘sahaba’ – neno linalotumiwa kwa mtu ambaye alikutana na Mtume na akafa kama Muislam– jina lake limeandikwa katika vitabu vingi vya kumbukumbu za masahaba wa Mtume.[8]

Safari ya Usiku na Kupaa Mbinguni

Miezi michache kabla ya kuhama kutoka Makka kwenda Madina, Mungu alimchukua Muhammad kwa usiku mmoja kutoka Msikiti Mkuu wa Makka hadi Msikiti wa al-Aqsa huko Jerusalem, safari ya mwezi ya km 1230 kwa msafara. Kutoka Yerusalemu, alipaa hadi mbinguni, akipita mipaka ya ulimwengu katika uwepo wa Mwenyezi Mungu, kukutana na Mungu, na kushuhudia Ishara Kuu (al-Ayat ul-Kubra). Ukweli wake ulionekana wazi kwa njia mbili. Moja, ‘Mtume alieleza misafara aliyoipita njiani kuelekea nyumbani na akasema mahali ilipo na kuhusu lini wangetarajiwa kufika Makka; na kila mmoja akafika kama ilivyotabiriwa, na maelezo yalikuwa kama alivyoeleza.’[9] Pili, hakuwahi kujulikana kuwa aliwahi kufika Yerusalemu, lakini aliuelezea Msikiti wa al-Aqsa kwa wenye shaka kama shahidi wa kuona.

The_Miracles_of_Muhammad_(part_2_of_3)_003.jpg

Safari ya ajabu imetajwa katika Kurani:

“SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.” (Kurani 17:1)

“Je! Mnabishana naye kwa aliyo yaona? Na akamwona mara nyingine, Penye Mkunazi wa mwisho. Karibu yake ndiyo ipo Bustani inayo kaliwa. Kilipo ufunika huo Mkunazi hicho kilicho ufunuika.Jicho halikuhangaika wala halikuruka mpaka.Kwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake Mlezi.” (Kurani 53:12-18)

Tukio hilo pia linathibitishwa kupitia ushuhuda wa mashahidi wa kuona uliopitishwa katika zama kupitia mlolongo wa uhakika wa wanazuoni(hadith mutawatir).[10]

The_Miracles_of_Muhammad_(part_2_of_3)_004.jpg

Mlango wa Msikiti wa Al-Aqsa ambapo Muhammad alipaa mbinguni. Picha kwa hisani ya Thekra A. Sabri.



Vielezi-chini:

[1] Saheeh Muslim.

[2] AngaliaNadhm al-Mutanathira min al-Hadith al-Mutawatir,’ na al-Kattani p. 215.

[3] “Kerala.” Encyclopædia Britannica kutoka Encyclopædia Britannica Premium Service. (http://www.britannica.com/eb/article-9111226)

[4]Imenukuliwa katika kitabu "Muhammad Rasulullah," na Muhammad Hamidullah: "Kuna hadithi ya zamani sana huko Malabar, Pwani ya Kusini-Magharibi ya India, kwamba Chakrawati Farmas, mmoja wa wafalme wao, aliona kugawanyika kwa mwezi. alisherehekea muujiza wa Mtukufu Mtume pale Makka, na alipopata kujua kwamba kulikuwa na utabiri wa kuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kutoka Uarabuni, alimteua mwanawe kama mtawala na akatoka kwenda kukutana naye. aliukubali uislam kwa mkono wa Mtume, na aliporudi nyumbani, kwa maelekezo ya Mtume, alifariki kwenye bandari ya Zafar, Yemen, ambapo kaburi la “mfalme wa Kihindi” lilitembelewa kwa uchamungu kwa karne nyingi.

[5]Zafar: Sephar ya kibiblia, Safa ya zamani, au sehemu ya Uarabuni ya kale ya Saphar iliyoko kusini-magharibi mwa Yarim kusini mwa Yemeni. Ulikuwa mji mkuu wa Wahiyariti, kabila lililotawala sehemu kubwa ya Uarabuni ya kusini kuanzia mwaka wa 115 KK hadi karibu BK 525. Hadi kufikia utekaji wa Waajemi (c. AD 575), Zafar ilikuwa mojawapo ya miji muhimu na iliyosherehekewa sana kusini mwa Uarabuni. -jambo ambalo limethibitishwa si tu na wanajiografia na wanahistoria Waarabu bali pia na waandishi wa Kigiriki na Waroma. Baada ya kutoweka kwa ufalme wa Himyar na kuinuka kwa Uislamu, Zafar taratibu ilianguka kwenye kugawanyika.’ “Zafar.” Encyclopædia Britannica kutoka Encyclopædia Britannica Premium Service. (http://www.britannica.com/eb/article-9078191)

[6]Al-Bidaya wal-Nihaya,’ na Ibn Kathir, vol 3, uk. 130.

[7]Imeripotiwa na Hakim ndani ya‘Mustadrik’ vol 4, uk. 150. Hakim anasema, ‘sijakariri ripoti nyingine yoyote inayosema mtume alikula tangawizi’

[8]Al-Isaba’ na Ibn Hajr, vol 3. p. 279 na‘Lisan ul-Mizan’ na Imam al-Dhahabi, juzuu ya 3 uk. 10 chini ya jina la ‘Sarbanak,’ jina ambalo waarabu walimjua.

[9]‘Muhammad: Maisha yake kulingana na vyanzo vya mwanzo Martin Lings, uk. 103.

[10] Masahaba arobaini na watano wa Mtume waliwasilisha taarifa za Safari yake ya Usiku na Kupaa Mbinguni. Tazama kazi za masomi wa hadithi: ‘Azhar al-Mutanathira fi al-Ahadith al-Mutawatira’ cha al-Suyuti uk. 263 na ‘Nadhm al-Mutanathira min al-Hadith al-Mutawatir,’ cha al-Kattani uk. 207.

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.