Maryamu, Mamake Yesu (sehemu ya 2 kati ya 2): Kuzaliwa kwa Yesu

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Makala hii inaeleza yale yaliyompata Maryamu baada ya kuwa chini ya ulezi wa Mtume Zakaria. Inasimulia jinsi malaika Gabrieli alivyotangaza kuzaliwa kwa mtoto wa kipekee, jinsi alivyokabiliana na kujifungua mtoto wake, na kusimulia baadhi ya miujiza iliyotukia wakati Yesu alipozaliwa.

  • Na Aisha Stacey (© 2008 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 10 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 2,877 (wastani wa kila siku: 3)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Aliyeheshimiwa na kupendwa na Waislamu wote na anayejulikana kama mwanamke mchamungu na msalihina, Maryamu, mamake Yesu alichaguliwa juu ya wanawake wote. Uislamu unakataa wazo la Kikristo kwamba Yesu ni sehemu ya utatu kuwa yeye ni Mungu, na unakataa kwa dhati kwamba Yesu ama mamake, Maryamu, wanastahili kuabudiwa. Kurani inatamka bayana kwamba hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu.

“Huyo ndiye Allah, Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu, hapana mungu ila Yeye, Muumba wa kila kitu. Basi muabuduni Yeye tu. Naye ni Mtegemewa wa kila kitu...” (Kurani 6:102)

Waislamu wanatakiwa, hata hivyo, kuwaamini na kuwapenda Mitume wote, akiwa ni pamoja na Mtume Yesu, ambaye ana nafasi maalum kwenye kanuni za imani za Kiislamu. Mamake, Maryamu, ana mahali pa heshima. Akiwa msichana, Maryamu alikwenda katika Nyumba ya Maombi huko Yerusalemu, maisha yake yote akiwa alijitolea kwa sala na ibada ya Mungu.

Maryamu Anapashwa Habari za Yesu

Wakati amejitenga na kila mtu, mtu mmoja alijitokeza mbele ya Maryamu. Mwenyezi Mungu alisema:

“Na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea Roho wetu, akajifananisha kwake sawa na mtu..” (Kurani 19:17)

Maryamu aliingiwa na hofu na kujaribu kukimbia. Alimwomba Mwenyezi Mungu akisema:

“(Maryamu) akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa Rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mchamungu..” (Malaika) akasema: Hakika mimi ni mwenye kutumwa na Mola wako Mlezi ili nikubashirie tunu ya mwana aliye takasika..” (Kurani 19:18-19)

Maryamu alistaajabishwa na kutatanishwa na maneno hayo. Hakuwa ameolewa, bali alikuwa bikira aliyejisitiri na kujilinda. Aliuliza kwa mshangao:

“‘Maryamu akasema: Mola wangu Mlezi! Vipi nitampata mwana na hali hajanigusa mwanaadamu? Mwenyezi Mungu akasema: Ndivyo vivyo hivyo, Mwenyezi Mungu huumba apendacho. Anapo hukumu jambo, huliambia: Kuwa! Likawa.” (Kurani 3:47)

Mwenyezi Mungu alimuumba Adam kwa vumbi la ardhi, bila mama wala baba. Alimuumba Hawa kutokana na ubavu wa Adam; na Yesu aliuumbwa bila ya baba, bali alikuwa na mama, Bikira Maryamu mchamungu. Mwenyezi Mungu, ambaye ni kauli ya lazima pindi anaposema ‘kitu Kiwe’ ili kukipatia uhai, alipuliza roho ya Yesu ndani ya tumbo la Maryamu kupitia Malaika Gabrieli.

“na tukampulizia humo[1] aliye linda ubikira wake, kutoka roho yetu, na akayasadiki maneno ya Mola wake Mlezi...” (Kurani 66:12)

Ingawa katika Kurani na Biblia hadithi za Maryamu zina vipengele vingi vinavyofanana, maoni ambayo Maryamu alikuwa ameposwa au kuolewa yanakataliwa kabisa na Uislamu. Muda ulipita, na Maryamu aliogopa kusemwa na watu waliokuwa karibu naye. Aliwaza jinsi ya kwamba watamuamini kuwa hakuna mwanaume aliyemgusa. Wanazuoni wengi katika Uislamu wanakubali kwamba muda wa ujauzito wa Maryamu ulikuwa wa kawaida.[2] Kisha, wakati ulipowadia wa yeye kujifungua, Maryamu aliamua kuondoka Yerusalemu, na kusafiri kuelekea mjini Bethlehemu. Ingawa Maryamu aliyakumbuka maneno ya Mwenyezi Mungu, na kwa kuwa imani yake ilikuwa yenye nguvu na thabiti, msichana huyo alikuwa na hofu na wasiwasi. Lakini malaika JibriliKadhalikaz alimpatia hakikisho:

“Na pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria (mwana) kwa neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa walio karibishwa (kwa Mwenyezi Mungu).” (Kurani 3:45)

Kuzaliwa kwa Yesu

Uchungu wa kujifungua ulimfikisha kwenye mti wa mtende na akalikumbatia shina la mtende na kuendelea kulia kwa uchungu:

“Laiti ningeli kufa kabla ya haya, na nikawa niliye sahaulika kabisa!” (Kurani 19:23)

Maryamu alijifungua mtoto wake papo hapo, chini ya mti wa tende. Alikuwa amechoka baada ya kujifungua, na kujawa na dhiki na hofu, lakini hata hivyo alisikia sauti ikimuita. .

“ Usihuzunike! Hakika Mola wako Mlezi amejaalia chini yako kijito kidogo cha maji; Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu.Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako...” (Kurani 19:24)

Mungu alimpa Maryamu maji, kijito kilitokea ghafla chini ya mahali alipokuwa ameketi. Kadhalika, alimpa chakula; kile alichotakiwa kufanya ni kutikisa shina la mti wa tende. Maryamu aliogopa na alijawa na hofu; alijihisi dhaifu sana baada ya kujifungua, kwa hiyo hakuna na nguvu ya kutikisa shina kubwa la mtende? Lakini Mwenyezi Mungu aliendelea kumpa Maryamu riziki.

Tukio lililofuata kwa hakika lilikuwa la muujiza mwingine, na kama wanadamu tunajifunza somo kubwa kutokana na hili. Maryamu hakuhitaji kutikisa mti wa tende, jambo ambalo lisingewezekana; ilibidi atie juhudi tu. Alipojaribu kufuata amri ya Mwenyezi Mungu, tende mbivu zilianguka kutoka kwenye mti na Mwenyezi Mungu akamwambia Maryamu: “…basi kula, na kunywa, na litue jicho lako.” (Kurani 19:26)

Sasa ilimbidi Maryamu amchukue mtoto wake mchanga na kuikabili familia yake. Bila shaka aliogopa, na Mwenyezi Mungu alijua hili vizuri. Hivyo alimwagiza anyamaze kimya. Haingewezekana kwa Maryamu kueleza jinsi ambavyo ghafla amekuwa mama wa mtoto mchanga. Kwa kuwa alikuwa hajaolewa, watu wake hawakuamini maelezo yake. Mungu alisema:

“Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako. Na pindi ukimwona mtu yeyote basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu.’” (Kurani 19:26)

Maryamu alifika kwa watu wake akiwa amembeba mtoto, na hapo hapo wakaanza kumshutumu; wakasema, “Umefanya aibu gani? Umetoka katika familia nzuri, na wazazi wako walikuwa wachamungu.”

Kama vile Mungu alivyokuwa amemwagiza, Maryamu hakuzungumza, alinyoosha kidole tu kwa mtoto aliyekuwa mikononi mwake. Kisha Yesu, mwana wa Maryamu akasema. Kama mtoto mchanga, Yesu, Mtume wa Mungu alifanya muujiza wake wa kwanza. Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu alisema:

“Akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu, amenipa Kitabu na amenifanya Nabii; Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo, Na ameniusia Swala na Zaka maadamu ni hai, na nimtendee wema mama yangu, wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu. Na amani iko juu yangu siku niliyo zaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai!” (Kurani 19:30-34)

Maryamu ametajwa katika Kurani (5:75) kama siddqa (mkweli) lakini neno la Kiarabu siddiqa linamaanisha maana zaidi ya kusema ukweli . Lina maana ya kwamba mtu amefikia kiwango cha juu sana cha uadilifu. Pia lina maana kwamba mtu ni mkweli, si tu na yeye mwenyewe na wale walio karibu nao, bali pia kwa Mungu. Maryamu alikuwa ni mwanamke aliyetimiza agano lake na Mwenyezi Mungu, ambaye alimuabudu kwa utiifu. Alikuwa mchamungu, aliyejisitiri, na msalihina; mwanamke aliyechaguliwa juu ya wanawake wengine wote kuwa mamake Yesu alikuwa ni Maryamu binti Imran.



Rejeleo la maelezo:

[1] Hili limefafanuliwa vyema katika maelezo wazi kuhusu vazi lake, ingawa aya yenyewe inazungumzia kuhusu "ubikira wake" (yaani kujilinda kutokana na kuingiliana na wanaume wanaoweza kumuoa). Hivyo Mungu akapuliza roho ndani yake hata kama alikuwa amejihifadhi kwa njia ya malaika Jibrili.

[2] Sheikh al Shanqeeti in (Adwaa’ al-Bayaan, 4/264)

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.