Kumuweka Mungu kwenye Moyo

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Kumkumbuka Mungu hupelekea amani na furaha katika maisha haya.

  • Na Imam Mufti (© 2012 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 11 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Jun 2023
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 2,123 (wastani wa kila siku: 2)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

KeepingGodintheHeart.jpgMtu lazima aelewe ulimwengu huu katika muktadha wa Monotheizimu (Imani katika Umoja wa Mungu). Ujumbe wa manabii ni rahisi: Watu waliumbwa kuwa watumishi wa Mungu, lakini kuwa hivyo wanahitaji kumjua Mungu. Mungu wa Uisilamu ni Mungu Mpendwa Anayependa (al-Wadud), Mungu mwenye Huruma (ar-Rahman), Mungu wa kibinafsi Anayefanya urafiki (al-Wali), mwenye uhusiano wa karibu na ambaye ana msingi wa kujisalimisha, kukumbuka, kutamani, na kuung'arisha ya moyo.

Mungu haitaji sifa na ibada zetu. Yeye ndiye Muumba wa mbingu na dunia, Mwenye Enzi Kuu, na Mtunzaji wa kila kitu katika ulimwengu wote. Hakika watu wengine wanaomkumbuka Yeye kwenye sayari ya upweke katika anga kubwa isiyo na mwisho iliyojazwa na mabilioni ya galaxi haimfaidishi Yeye kwa njia yoyote ile, wala haitaongeza Ufalme Wake hata kwa uzito wa atomi. Mtume Muhammad, rehema za Mungu ziwe juu yake, anasimulia yafuatayo kwa niaba ya Mungu:

"Enyi waja Wangu, Nimeharamisha udhalimu kwa nafsi yangu na nimefanya ni haramu kati yenu, kwa hivyo msidhulumiane .... Enyi waja wangu, hamtaniudhuru wala hamtanifaidisha. Enyi waja Wangu, wakitokea wa kwanza wenu na wa mwisho wenu, binadamu kutokana na nyinyi na majini kati yenu kuwa wachamungu sana, kwamba hangeweza kuniongezea ufalme Wangu kwa chochote. Enyi Waja Wangu, wakitokea wa kwanza wenu na wa mwisho wenu, binadamu kutokana na nyinyi na majini kati yenu kuwa waovu sana, kwamba hangeweza kunipunguzia ufalme Wangu kwa chochote...."[1]

Mungu ameamuru ukumbusho Wake (unaojulikana kama dhikr) na ibada zingine kwa faida yetu. Aina zote za ukumbusho na ibada, hutumika kutukumbusha juu ya Mungu na kutuweka tukimkumbuka kila wakati. Na ufahamu huu wa Mungu, unatuzuia kutenda dhambi, kufanya dhuluma na uonevu, na kutuhamasisha kutimiza haki zake na haki za uumbaji. Na kwa hivyo kwa kufuata njia zilizowekwa kwa ajili yetu na Mungu, kwa hakika tunajisaidia wenyewe, kwasababu ndiyo njia bora kabisa tunayoweza kuichukua katika jambo lolote na kujua kuwa unafanya jambo linalofaa litakalo sababisha kuridhika, amani, na furaha.

Kama wanadamu wanavyokabiliwa na uvivu na udhalimu, bila kuwa na njia zozote za kumkumbuka au kumwabudu Mungu, itatufanya sisi kuwa tusiojali na kuzama zaidi na zaidi katika makosa na giza mpaka tutamsahau Mungu kabisa, kwa wajibu na majukumu yetu maishani.

"Ole wao wenye nyoyo ngumu zisio mkumbuka Mwenyezi Mungu!" (Kurani 39:22)

"Enyi mlio amini! Yasikusahaulisheni mali yenu, wala watoto wenu, kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Na wenye kufanya hayo ndio walio khasiri. " (Kurani 63:9)

Dhikr imegawanywa katika matawi mawili: dhikr ya ulimi na dhikr moyo wakati moyo unafikiria uzuri na ukuu wa Mungu.

Kama vile kumsahau Mungu kunaleta maumivu ya kusahauliwa na Yeye, vivyo hivyo kumkumbuka Mungu husababisha furaha ya kukumbukwa na Yeye: "Nikumbuke, nami nitakukumbuka" (Kurani 2: 152). Matokeo ya kumkumbuka Mungu sio tu kukumbukwa na Mungu katika ulimwengu ujao, lakini pia kufikia amani ya moyo katika ulimwengu huu. "Sikiza, mioyo hupata amani tu katika kumkumbuka Mungu." (Kurani 13:28). Kumwita Mungu wakati wa kukata tamaa, kunaweza kukupa faraja na amani kwakuwa unamwita Yule aliye na Nguvu zote na ndiye pekee anayeweza kukutoa katika shida.

Dhikri au kumkumbuka Mungu ni njia ya kuunganisha moyo wako na Mungu. Inatoa na mazoea ya kiroho ya kukumbuka na kuungana tena na kile cha maana zaidi katika maisha yetu, Mungu. Waislamu hupata faraja, amani na nguvu katika kurudia mara kwa mara misemo mitakatifu iliyo na Majina ya Mungu na sifa Zake. Iliyo katika njia inayofaa, dhikr ni chakula cha njaa ya kiroho.

Dhikri ni hatua katika njia ya upendo; Pindi mtu anapompenda mtu, anapenda kulirudia jina lake na kumkumbuka kila wakati. Kwa hivyo, moyo ambao umepandikizwa upendo wa Mungu dhikri itakuwa makaoyake kila muda.

Dhikri pia inashauriwa kwa waamini kama njia ya kupata thawabu za mbinguni. Inachukuliwa kuwa ibada na inaongeza matendo mema ya mtu.

Kipengele cha kuvutia zaidi cha dhikr ni kwamba inaruhusiwa mahali popote na wakati wowote; kufanyika kwake hayazuiliwi kuwa ni kwa saa flani za Sala (sala ya ibada) wala mahali maalum. Mungu anaweza kukumbukwa mahali popote. Matendo haya yanapatikana kwa wanawake kama ilivyo kwa wanaume.

Maneno maalum ya dhikr hutumiwa katika madhumuni ya uponyaji pia. Hata leo kisomo cha baadhi ya maombi yaliyofundishwa na Mtume Muhammad na aya kutoka kwenye Kurani Tukufu hutumiwa kutibu wagonjwa.

Kurani inataja umuhimu wa dhikr moja kwa moja na katika njia isiyo ya moja kwa moja katika aya mbali mbali katika Kurani, "dhikr (ukumbusho, ufahamu) wa Mungu ni mkubwa" au "jambo kuu."

Njia bora zaidi ya ukumbusho wa Mungu ni Kurani inayojiita Al-Dhikr, "Kikumbusho" (Kurani 20:99); kwa hivyo, jina lingine la Kurani ni Dhikr-ullah, "ukumbusho wa Mungu." Moja, ni kutambua kwamba kusoma Kurani ni kumkumbuka Mungu. Mbili, sura ya kwanza ya Kurani, Al-Fatiha, ni msingi mkuu wa sala za kila siku za Waislamu. Sio hivyo tu, pia ni kiini cha ujumbe wa Kurani. Tatu, Kurani inatoka kwa Mungu (ni Neno Lake) na hutoa njia za kuishi maisha ambayo yanampendeza Yeye.

Dhikri inapendwa kwa sababu kumkumbuka Mungu ni kumuweka Mungu katikati na kuviweka vitu yote pembeni. Matendo yote ya Kiislamu ya ibada hufanywa kwa ajili ya ukumbusho, kumweka Mungu katikati ya maisha ya kiroho kwa njia hiyo. Kurani inaita sala ya ibada (salah) yenyewe "ukumbusho." Baada ya Kurani, kuna aina ya ukumbusho wa Mungu (dhikr) ambayo ni aina ya upanuzi wa hiari wa sala ya ibada (salah).

Karibu na Kurani, dhikr bora, maneno ambayo Mungu anapenda zaidi, ni taaluma ya imani la ilaha illa Allah (hakuna mungu wa kweli anayestahili kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu), na vile vile maneno ya Subhan-Allah (Mungu yupo mbali na kutokukamilika), Allahu-Akbar (Mungu ndiye Mkuu), na al-Hamdu-lillah (Sifa zote na shukrani ni za Mwenyezi Mungu).



Rejeleo la maelezo:

[1] Saheeh Muslim, Ibn Majah & At Tirmidhi

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.