Uovu wa Uongo

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Sababu za kusema uwongo ambazo kwa majuto zimekuwa "kitambaa cha maisha ya jamii."

  • Na Imam Mufti
  • Iliyochapishwa mnamo 11 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 3,004 (wastani wa kila siku: 3)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

The_Malice_of_Lying_001.jpgUongo ni sehemu ya kawaida ya uhusiano wa kibinadamu. Watu husema uwongo kwa sababu mbalimbali. Wanaweza kusema uwongo kama sehemu ya uwasilishaji wa kibinafsi, ili kuwasilisha picha nzuri zaidi kwa wengine. Watu wanaweza pia kusema uwongo ili kupunguza mizozo, kwa sababu kusema uwongo kunaweza kufanya kutokubaliana kuwa kidogo. Ingawa kusema uwongo kunaweza kufanya kazi muhimu katika mambo haya, inaweza pia kuharibu uhusiano. Uongo uliogundulika hudhoofisha uaminifu na hupandisha tuhuma, kwa sababu mtu aliyedanganywa ana uwezekano wa kutomwamini mtu aliyesema uwongo siku za mbeleni. [1] Watu wengine hata husema uwongo kwa sababu ya tabia za kimsukumo. 'Uongo wa kila siku ni sehemu ya maisha ya kijamii,' anasema Bella DePaulo, mtaalamu wa saikolojia na mtaalam wa uwongo katika Chuo Kikuu cha Virginia. Utafiti wake unaonyesha wanaume na wanawake hudanganya kwa takribani ya mara tano ya mazungumzo yao ya kijamii yanayodumu kwa dakika 10 au zaidi; kwa kipindi cha wiki moja huwadanganya karibu ya asilimia 30 ya wale ambao wanashirikiana nao moja kwa moja. Cha kuongezea, aina zingine za uhusiano, kama zile kati ya wazazi na vijana, ni sumaku halisi za udanganyifu. Kusema uwongo kunachukuliwa kuwa muhimu katika kazi nyingi: tunaona wanasheria wakijenga hoja za nadharia zilizoaminika kwa niaba ya wateja wao au waandishi wa habari wanajiwasilisha vibaya ili kupata habari nzuri.[2]

Kusema uwongo ni uovu mkubwa, umeenea katika jamii zetu. Kuwadanganya wengine kwa kutumia maneno ya kijanja hunaonekana kuwa ni werevu. Takwimu za umma zinasema uwongo. Serikali zinasema uwongo. Tofauti ya umri wetu ni kuwa kusema uwongo hakuweki doa tena kama zamani. Leo kusema uwongo imekuwa taasisi. Ni njia ambayo wengi wetu tunaishi nayo, kutoka juu, kwa sababu tuligundua kuwa ikiwa tunaushawishi vya kutosha, uwongo unafanya kazi. Nchi zinavamiwa na vita vinaanzishwa kutokana na uwongo. "Sisi" kamwe hatusemi uwongo, tunapindisha ukweli kidogo, kunasuka, bila nia ya kupotosha, lakini "wengine" ni waongo. Jamii yetu ni jamii ambayo imekamilisha "sanaa" ya uwongo. Zimepita siku ambapo uwongo uliharibu utu wa mwongo na kumnyima imani yetu.

Uislamu unaona uwongo kama tabia mbaya. Mungu anasema katika Kurani:

"Wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo." (Kurani 17:36)

Mtume, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, alisisitiza umuhimu wa kuwa mkweli kila wakati na uzito wa uwongo, "Ukweli unasababisha uchamungu na uchamungu huongoza Peponi. Mtu anapaswa kuwa mkweli mpaka aandikwe kama mkweli kwa Mungu. Uongo husababisha upotovu na upotovu unaongoza Motoni. Mtu atasema uongo mpaka aandikwe kama mwongo na Mungu. "[3] Ukweli ni kusema kile kinacholingana na ukweli, jinsi mambo yalivyo, na ni kinyume cha uwongo. Uovu wa uwongo umefungamana na unafiki kama ilivyoelezewa na Mtume Muhammad, "Ikiwa mtu yeyote ana sifa nne, yeye ni mnafiki , na ikiwa mtu yeyote ana moja yao, ana hali ya unafiki mpaka atoe: akiaminiwa, anasaliti uaminifu wake; kila anapoongea, anaongea uwongo; akiweka miadi, haitimizi; na anapogombana, anatoka kwenye ukweli kwa kusema uongo.[4] Mafundisho ya Mtume ni kuwa tunajaribu kila tuwezalo kujinasua na unafiki kwa kuweka amana zetu, kusema ukweli, kutimiza ahadi zetu, na sio kusema uwongo.

Kwenye Uislam, uwongo mbaya kabisa ni dhidi ya Mungu, manabii wake, ufunio wake, na kutoa ushahidi wa uwongo. Tunapaswa kuwa waangalifu tusitoe visingizio vya uwongo kama vile 'nilikuwa na shughuli nyingi au nilisahau,' au kuwema maneno ambayo yanaweza kuchukuliwa kama ahadi kwa wengine kama 'nitarudi kesho,' bila nia hiyo. Wakati huo huo, kusema uwongo hakupaswi kuchanganywa na ukosefu wa adabu, ‘kusema kama kilivyo,’ lakini tunapaswa kuwa waangalifu tusiongope juu ya vitu vidogo bila mtu yoyote kuumia. Hili linaweza kufanywa kwa kuchagua kwa uangalifu maneno yetu.

Je! "Usiseme uwongo kamwe!" kanuni kamili ya Uislamu au kuna uchaguzi? Tuseme kuwa kuna mtu muuji anakuja kugonga mlango wako, akimtafuta mtu aliyemkusudia . Je! Jibu sahihi la kimaadili, "Amejificha ghorofani, akitumaini utaondoka"? Wanafalsafa kama Kant waliandika kana kwamba hili lilikuwa jambo sahihi la kimaadili kulifanya, lakini kwa Uislam, uwongo una haki katika mambo kama hayo.



Rejeleo la maelezo:

[1] ‘Haki ya Kufanya Mabaya: Kudanganya Wazazi kati ya Vijana na Watu wazima Wanaoibuka,’ na Jeffrey Jensen Arnett, Elizabeth Cauffman, S. Shirley Feldman, Lene Arnett Jensen; Jarida la Vijana na Ujana, Juz. 33, 2004.

[2] 'Ukweli juu ya kusema uwongo,' na: Allison Kornet. Saikolojia Leo, Tarehe ya Uchapishaji: Mei / Juni 97

[3]Saheeh Al-Bukhari, Saheeh Muslim

[4] Saheeh Al-Bukhari, Saheeh Muslim

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.