Raha Za Peponi Kwa Ufupi
Maelezo: Mtazamo wa asili ya Pepo kama ilivyoelezwa katika Kurani na maneno ya Mtume Muhammad.
- Na islam-guide.com
- Iliyochapishwa mnamo 29 Nov 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 2,560 (wastani wa kila siku: 2)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mwenyezi Mungu amesema katika Kurani:
“Na wabashirie walio amini na wakatenda mema kwamba watapata mabustani yapitayo mito kati yake....” (Kurani 2:25)
Mungu pia amesema:
“Kimbilieni msamaha wa Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, iliyo wekewa walio muamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake....” (Kurani 57:21)
Mtume Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, ametuambia kuwa aliye chini kabisa katika daraja miongoni mwa watu wa Peponi atakuwa na mara kumi ya dunia hii,[1] na atapata chochote atakacho tamani na mara kumi kama hiyo.[2] Pia, Mtume Muhammad amesema: “Nafasi katika Pepo inayolingana na ukubwa wa mguu ingekuwa bora kuliko dunia na vilivyomo ndani yake.”[3] Pia alisema: “ huko Peponi kuna vitu ambavyo jicho halijawahi kuona, hakuna sikio lililosikia, na hakuna akili ya mwanadamu iliyo fikiria.”[4] Pia alisema: “Mtu mwenye huzuni zaidi katika ulimwengu wa wale walio kusudiwa kwa ajili ya Pepo atatumbukizwa mara moja katika Pepo. Kisha ataulizwa, ‘Mwana wa Adamu, je! uliwahi kupata taabu yoyote? Je! umewahi kupatwa na magumu yoyote?’ Kwa hiyo atasema, ‘Hapana, Wallahi, Ee Mola! Sikuwahi kukumbana na taabu yoyote, na sikupata shida yoyote.’”[5]
Ukiingia Peponi, utaishi maisha ya furaha sana bila magonjwa, maumivu, huzuni, au kifo; Mungu atakuwa atapendezwa nawe; nawe utaishi huko milele. Mwenyezi Mungu amesema katika Kurani:
“Na wale walio amini na wakatenda mema tutawaingiza katika Pepo zipitazo mito kati yake kwa kudumu humo milele....” (Kurani 4:57)
Rejeleo la maelezo:
[1]Imesimuliwa katika Saheeh Muslim, #186, na Saheeh Al-Bukhari, #6571.
[2]Imesimuliwa katika Saheeh Muslim, #188, na Mosnad Ahmad, #10832.
[3]Imesimuliwa katika Saheeh Al-Bukhari, #6568, na Mosnad Ahmad, #13368.
[4]Imesimuliwa katika in Saheeh Muslim, #2825, na Mosnad Ahmad, #8609.
[5]Imesimuliwa katika Saheeh Muslim, #2807, na Mosnad Ahmad, #12699.
Ongeza maoni