Maelezo ya Kurani Kuhusu Giza Chini ya Bahari na Mawimbi ya Ndani

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Maelezo ya Kurani kuhusu maisha katika bahari ya kina, na giza ndani yake, na jinsi inathibitisha matokeo ya kisayansi ya kisasa.

  • Na islam-guide.com
  • Iliyochapishwa mnamo 23 Nov 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 27 Feb 2023
  • Ilichapishwa: 1
  • Imetazamwa: 2,537 (wastani wa kila siku: 3)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Mungu anasema katika Kurani:

“Au (vitendo vya makafiri) ni kama giza katika bahari kuu, iliyo funikiwa na mawimbi juu ya mawimbi, na juu yake yapo mawingu. Giza juu ya giza. Akiutoa mtu mkono wake anakaribia asiuone...” (Kurani 24:40)

The_Quran_on_Deep_Seas_and_Internal_Waves_001.jpg

Aya hii inataja giza linalopatikana katika majimakuu, ambapo mtu akinyosha mkono wake, hawezi kuiona. Giza chini ya bahari huanza karibu na kina cha mita 200 kuenda chini. Kwa kina hiki, takriban hakuna mwanga.(angalia picha ya 1). Chini ya kina cha mita 1000 hakuna mwanga kabisa. [1] Binadamu hawawezi kupiga mbizi zaidi ya mita arobaini bila msaada wa manowari au vifaa maalum. Binadamu hawawezi kuishi bila msaada katika sehemu ya giza ya bahari, kama vile kwa kina cha mita 200.

The_Quran_on_Deep_Seas_and_Internal_Waves_002.jpg

Picha 1: Kati ya asilimia 3 na 30 ya mwanga wa jua hurudishwa kutoka juu ya bahari. Kisha karibu rangi zote saba za wigo wa mwanga hupotea moja kwa moja katika mita 200 za kwanza, isipokuwa mwanga wa buluu. (Bahari, Elder na Pernetta, uk. 27)

Wanasayansi hivi karibuni wamegundua giza hili kwa kutumia vifaa maalum na nyambizi ambazo zimewawezesha kufikia kina cha bahari.

Pia tunaweza kuelewa kutokana na sentensi zifuatazo katika aya iliyopita, “...katika bahari kuu, iliyo funikiwa na mawimbi juu ya mawimbi, na juu yake yapo mawingu....”, kwamba maji ya kina ya bahari yanafunikwa na mawimbi, na juu ya mawimbi haya ni mawimbi mengine. Ni wazi kwamba aina ya pili ya mawimbi ni mawimbi ya juu tunayoyaona, kwa sababu aya inataja kuwa juu ya mawimbi ya aina ya pili kuna mawingu. Lakini mawimbi ya kwanza ni yapi? Wanasayansi hivi karibuni wamegundua kwamba kuna mawimbi ya ndani ambayo “hutokea kwenye mipaka ya wiani kati ya tabaka za wiani tofauti.” [2] (angalia picha ya 2).

The_Quran_on_Deep_Seas_and_Internal_Waves_003.jpg

Picha ya 2: Mawimbi ya ndani katika mpaka kati ya tabaka mbili za maji ya wiani tofauti. Moja ni zito (ya chini), nyingine uzito wake ni ndogo (ya juu). (Uchunguzi wa bahari, Jumla, uk. 204.)

Mawimbi ya ndani yanafunika maji ya kina ya bahari kwa sababu maji ya kina yana wiani mkubwa kuliko maji yaliyo juu yao. Mawimbi ya ndani huwa kama mawimbi ya juu. Yanaweza pia kuvuma, kama mawimbi ya juu. Mawimbi ya ndani hayawezi kuonekana kwa jicho la mwanadamu, lakini yanaweza kugunduliwa kwa kuchambua halijoto au mabadiliko ya kiwango cha chumvi katika mahali fulani.[3]



Rejeo la maelezo:

[1]Bahari, Elder and Pernetta, uk. 27.

[2]Uchunguzi wa bahari, Jumla, uk. 205.

[3]Uchunguzi wa bahari, Jumla, uk. 205.

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.