Maelezo ya Kurani kuhusu Kupanuka kwa Ulimwengu na Nadharia ya Mlipuko Mkubwa

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Makala hii inaelezea uwiano kati ya maelezo ya kisayansi yaliyokubaliwa zaidi ya asili na upanuzi wa Ulimwengu, na maelezo ya asili na upanuzi wake kwenye Kurani.

  • Na Sherif Alkassimi (© 2008 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 23 Nov 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 21 Nov 2022
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 2,685 (wastani wa kila siku: 3)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Kanuni ya Hubble

Kwa maelfu ya miaka, wanaastronomia walijadiliana kuhusu maswali ya kimsingi kuhusu ulimwengu. Hadi kufikia mwanzo wa miaka ya 1920, iliaminika kwamba ulimwengu ulikuwepo daima; pia, iliaminika ya kwamba ukubwa wa ulimwengu haubadiliki. Hata hivyo, mnamo mwaka wa 1912, mwanaastronomia wa Marekani, Vesto Slipher, aligundua jambo ambalo lingebadili imani za wanaastronomia kuhusu ulimwengu. Slipher aligundua kwamba makundi ya nyota yalikuwa yakisonga mbali na ardhi kwa kasi kubwa. Uchunguzi huu ulitoa ushahidi wa kwanza unaounga mkono nadharia ya kupanuka kwa ulimwengu.[1]

The_Quran_on_the_expanding_Universe_and_the_Big_Bang_theory_001.jpg

Kabla ya uvumbuzi wa darubini mwaka wa 1608, mwanadamu hakuweza kufanya mengi zaidi ya kustaajabia kuhusu asili ya ulimwengu. (Kwa hisani ya: NASA)

Mwaka wa 1916, Albert Einstein aliunda Nadharia yake ya ujumla ya Uwiano ambayo ilionyesha kwamba ulimwengu lazima uwe unapanuka au kukunjamana. Uthibitisho wa nadharia ya kupanuka kwa ulimwengu hatimaye ulifika mwaka wa 1929 mikononi mwa mwanaastronomia maarufu wa Marekani Edwin Hubble.

Kwa kuchunguza mabadiliko [2] katika mawimbi ya mwanga unaotolewa na makundi ya nyota, Hubble aligundua kwamba makundi hayo hayakudumu kwa nafasi yao; badala yake, yalikuwa yakisonga mbali na ardhi kwa kasi sawia na umbali wao kutoka ardhini (Kanuni ya Hubble). Maelezo pekee ya uchunguzi huu ni kwamba ulimwengu lazima unapanuka. Ugunduzi wa Hubble unajulikana kama mojawapo ya magunduzi makubwa zaidi katika historia ya astronomia. Mnamo Mwaka wa 1929, alichapisha uhusiano kati ya kasi na wakati, ambao ni msingi wa kosmolojia ya kisasa. Katika miaka yaliyofuata, na baada ya uchunguzi zaidi, nadharia ya kupanuka kwa ulimwengu ilikubaliwa na wanasayansi na wanaastronomia wote.

See Explanation.  Clicking on the picture will download  the highest resolution version available.The_Quran_on_the_expanding_Universe_and_the_Big_Bang_theory_003.jpgSee Explanation.  Clicking on the picture will download  the highest resolution version available.

Kwa kutumia darubini-upeo ya Hooker , Hubble aligundua ya kwamba makundi ya nyota yalikuwa yakisonga mbali na ardhi. Juu ni picha ya makundi ya nyota yanayojulikana. (Kwa hisani ya: NASA)

Hata hivyo, cha kushangaza ni kwamba kabla darubini hazijagunduliwa na kabla ya Hubble kuchapisha kanuni yake, Mtume Muhammad, rehema na amani ziwe juu yake, alikuwa akisoma aya ya Kurani kwa wenzake ambayo ilitaja ya kuwa ulimwengu unapanuka.

“Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila shaka ndio twenye uwezo wa kuzitanua (kuzipanua).” (Kurani 51:47)

Kurani ilipokuwa inashuka, neno “anga ya nje” lilikuwa halikujulikani, na watu walitumia neno “mbingu” kuashiria chochote kilicho juu ya ardhi. Kwenye aya iliyotajwa juu, neno “mbingu” linamaanisha anga ya nje na ulimwengu unaojulikana. Aya inaonyesha ya kuwa anga ya nje, na hivyo ulimwengu, unapanuka, kama vile Kanuni ya Hubble ilivyotaja.

Ya kwamba Kurani ilitaja jambo kama hilo katika karne hizo kabla ya uvumbuzi wa darubini ya kwanza, wakati ambapo kulikuwa na elimu chache sana kuhusu sayansi, ni kati ya maajabu ya Kurani. Zaidi ya hayo, kwa kuzingatia ya kwamba, mithili ya watu wengi waliokuwa wakati wake, Mtume Muhammad rehema na amani ziwe juu yake, hakujua kuandika wala kusoma, na hivyo hangeweza kuwa na ufahamu wa mambo kama hayo kivyake. Je, inawezekana kwamba alikuwa amepokea ufunuo kutoka kwa Muumba na Mwanzilishi wa ulimwengu?

Nadharia Ya Mlipuko Mkubwa

Baada ya Hubble kuchapisha nadharia yake, aligundua ya kwamba makundi ya nyota hayakuwa yakisonga mbali na Ardhi pekee, lakini pia kila kundi lilikuwa likisonga mbali na kundi lingine. Hii ilimaanisha ya kwamba ulimwengu ulikuwa ukipanuka kwa kila upande, kama vile puto hupanuka linapojazwa hewa. Ugunduzi huu mpya wa Hubble umekuwa msingi wa nadharia ya Mlipuko Mkubwa.

Nadharia ya Mlipuko Mkubwa inasema ya kwamba takriban miaka bilioni 12-15 iliyopita ulimwengu ulizaliwa kutokana na nukta moja yenye nguvu na joto jingi sana, na kwamba kuna kitu kilisababisha mlipuko wa nukta hii ambayo ilianzisha ulimwengu. Ulimwengu, tangu wakati huo, unapanuka kutoka nukta hii moja.

Baadaye, mwaka wa 1965, wanaastronomia wa redio Arno Penzias na Robert Wilson walifanya ugunduzi ulioshinda Tuzo ya Noble uliothibitisha nadharia ya Mlipuko Mkubwa. Kabla ya ugunduzi wao, nadharia hiyo iliashiria kwamba ikiwa nukta ambayo ulimwengu ulitokana nayo ilikuwa na joto jingi sana, basi mabaki ya joto hili yanapaswa kupatikana. Mabaki hayo ndiyo Penzias na Wilson waliyapata. Mnamo mwaka wa 1965, Penzias na Wilson waligundua nyuzi ya 2.725 ya Kelvin ya Mnururisho wa Vijiwimbi wa Ulimwengu (CMB) inayoenea kote ulimwenguni. Hivyo, ilieleweka kuwa mionzi iliyopatikana ilikuwa mabaki ya hatua za mwanzo za Mlipuko Mkubwa. Kwa sasa, nadharia ya Mlipuko Mkubwa inakubaliwa na wengi kati ya wanasayansi na wataalamu wa astronomia.

Cosmic Background Explorer Data

Ramani ya vijiwimbi ya mabaki ya Mlipuko Mkubwa uliozaa ulimwengu. (Kwa hisani ya: NASA)

Inatajwa katika Kurani:

“Yeye ndiye Muumbaji wa mbingu na ardhi…” (Kurani 6:101)

“Kwani aliye ziumba mbingu na ardhi hawezi kuwaumba mfano wao? Kwani! Naye ndiye Muumbaji Mkuu, Mjuzi. Hakika amri yake anapo taka kitu ni kukiambia tu: 'Kuwa' Na kikawa.” (Kurani 36:81-82)

Aya zilizo juu zinathibitisha kwamba ulimwengu ulikuwa na mwanzo, kwamba Mungu ndiye muumbaji wake, na yote ambayo Mungu anahitaji kufanya ili kuunda ni kusema tu “Kuwa,” na unakuwa. Je, hii inaweza kuwa maelezo ya kilichosababisha mlipuko ulioleta mwanzo wa ulimwengu?

Kurani pia inataja:

“Je, hao waliokufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana, kisha Sisi tukazibandua, na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai? Basi je, hawaamini?” (Kurani 21:30)

Wasomi wa Kiislamu ambao wameelezea aya iliopita wanataja kwamba kuna marambingu na ardhi zilikuwa zimeshikana, halafu Mungu alivifanya vitengane na kuunda mbingu saba na Ardhi. Hata hivyo, kutokana na mapungufu ya sayansi na teknolojia wakati wa kushuka kwa Kurani (na kwa karne nyingi zilizofuata), hakuna msomi aliyeweza kutoa maelezo mengi ya kina kuhusu jinsi mbingu na ardhi zilitengenezwa. Kile wasomi waliweza kukielezea kwa kina kilikuwa ni maana sahihi ya kila neno kwa Kiarabu katika aya, pamoja na maana ya jumla ya aya yenyewe.

Kwa aya iliyotangulia, maneno ya kiarabu ya ratq and fataq yametumika. Neno ratq inaweza kutafsiriwa kuwa “kipengele” “imeshonwa kwa” “yameunganishwa” au “yamefungwa pamoja”. Maana ya tafsiri zote hizi inahusisha kitu kilichochanganywa pamoja na kuwa kila kipengele kina uwepo wake tofauti na kingine. Kitenzi fataq kinatafsiriwa kuwa “Tulitawanya” “Tuliyapasua” “Tulitenganisha” au “Tuliyafungua”. Maana hizi zinadokeza ya kuwa kitu huja kwa kitendocha kutenganisha au kupasua. Kuchipuka kwa mbegu ni mfano bora katika kueleza maana ya kitenzi fataq.

Baada ya kugunduliwa kwa nadharia ya Mlipuko Mkubwa,imekuwa wazi kwa wasomi wa Kiislamu ya kuwa maelezo yaliyotajwa kuhusiana na nadharia hiyo yanaendana na maelezo ya uumbaji wa ulimwengu katika aya ya 30, sura ya 21 ya Kurani. Nadharia inasema ya kwamba ulimwengu ulitokana na nukta moja yenye nguvu na joto jingi; ambayo ililipuka na kuanzisha ulimwengu, na hilo linalingana na kile kinachotajwa katika aya ya kwamba mbingu na Ardhi (na hivyo ulimwengu) zilikuwa zimeungana, na kisha kutawanyika. Kwa mara nyingine tena, maelezo pekee yanayoweza kutolewa ni kwamba Mtume Muhammad, rehema na amani ziwe juu yake, alikuwa amepokea ufunuo kutoka kwa Mungu, Muumba na Mwanzilishi wa ulimwengu.



Vielezi-chini:

[1] Dakika Tatu za Kwanza, Mtazamo wa Kisasa wa Asili ya Ulimwengu, Weinberg.

[2] Wakati nuru ya kitu husonga hadi upande wa nyekundu wa uratibishaji wa mwanga. (http//bjp.org.cn/apod/glossary.htm)

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.