Uvumilivu wa Mtume kwa Dini Nyingine (sehemu ya 1 kati ya 2): Kwa Kila Mmoja Dini Yake Mwenyewe.
Maelezo: Wengi wanaamini kimakosa kwamba Uislamu hauvumilii kuwepo kwa dini nyingine zilizopo duniani. Makala hii inazungumzia baadhi ya misingi ambayo Mtume Muhammad mwenyewe aliiweka katika kushughulika na watu wa imani nyingine, kwa mifano ya kivitendo toka enzi za uhai wake. Sehemu ya 1: Mifano ya uvumilivu wa kidini kwa watu wa imani nyingine inayopatikana katika katiba ambayo Mtume aliiweka Madina.
- Na M. Abdulsalam (© 2006 IslamReligion.com)
- Iliyochapishwa mnamo 17 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 31 Aug 2024
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 4,345 (wastani wa kila siku: 4)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Shughuli za Mtume, Mungu ampe baraka, na dini nyingine inaweza kuelezewa vyema zaidi katika aya ya Kurani:
“Kuweni kwenu na dini yenu, kwangu mimi niwe na yangu.”
Peninsula ya Arabia katika zama za Mtume lilikuwa ni eneo ambalo imani mbalimbali zilikuwepo. Kulikuwa na Wakristo, Wayahudi, Wazoroastria, washirikina, na wengine wasiofungamana na dini yoyote. Mtu anapotazama maisha ya Mtume, anaweza kuteka mifano mingi ili kuonyesha uvumilivu wa hali ya juu ulioonyeshwa kwa watu wa imani nyingine.
Ili kuelewa na kuhukumu uvumilivu huu, mtu lazima aangalie katika kipindi ambacho Uislamu ulikuwa dola rasmi, na sheria mahususi zilizo wekwa na Mtume kwa mujibu wa kanuni za dini. Ingawa mtu anaweza kuona mifano mingi ya uvumilivu iliyoonyeshwa na Mtume katika miaka kumi na tatu ya kukaa kwake Makka, mtu anaweza kufikiri kimakosa kwamba ilitokana tu na kutaka kuinua hadhi ya Waislamu na hadhi ya kijamii ya Uislamu na kwa ujumla. Kwa sababu hii, majadiliano yatahusu kipindi ambacho kilianza kwa Mtume kuhama kwenda Madina, na hasa mara tu katiba ilipowekwa.
Swahiyfah
Mfano bora zaidi wa uvumilivu ulioonyeshwa na Mtume kwa dini zingine unaweza kuwa ni katiba yenyewe, inayoitwa ‘Swahiyfah’ na wana historia wa mwanzo.[1] Mtume alipohamia Madina, jukumu lake kama kiongozi wa kidini liliisha; sasa alikuwa kiongozi wa kisiasa wa dola, iliyotawaliwa na kanuni za Uislamu, ambazo zilitaka sheria za utawala ziwekwe wazi ili kuhakikisha maelewano na utulivu katika jamii ambayo hapo awali ilikuwa imefadhaishwa na miongo ya vita, ambayo lazima ihakikishe kuishi pamoja kwa amani Waislamu, Wayahudi, Wakristo na washirikina. Kutokana na hili, Mtume aliweka ‘katiba’ ambayo ilieleza kwa kina majukumu ya pande zote zilizokuwa zikikaa Madina, wajibu wao kwa kila mmoja wao kwa wao, na vikwazo fulani ambavyo viliwekwa kwa kila mmoja. Washiriki wote walipaswa kutii yale yaliyotajwa humo, na uvunjaji wowote wa vipengele vyake ulizingatiwa kuwa ni kitendo cha usaliti.
Nchi Moja
Kifungu cha kwanza cha katiba kilikuwa kwamba wakaaji wote wa Madina, Waislamu na vilevile wale walioingia kwenye mapatano hayo kutoka kwa Wayahudi, Wakristo, na waabudu masanamu, walikuwa “taifa moja bila ya kuwatenga wengine wote.” Wote walichukuliwa kuwa wanachama na raia wa jamii ya Madina bila kujali dini, rangi, au ukoo. Watu wa imani nyingine walilindwa dhidi ya madhara kama vile Waislamu, kama ilivyoelezwa katika makala nyingine, “Kwa Wayahudi wanaotufuata wanapata msaada na usawa. Hatadhurika wala adui zake hawatasaidiwa.” Hapo awali, kila kabila lilikuwa na mapatano na maadui ndani na nje ya Madina. Mtume aliyakusanya makabila haya tofauti chini ya mfumo mmoja wa utawala ambao ulishikilia mapatano yaliyokuwepo hapo awali baina ya makabila hayo binafsi. Makabila yote yalipaswa kutenda kwa ujumla bila kujali mapatano ya watu binafsi. Shambulio lolote dhidi ya dini nyingine au kabila lilionekana kuwa ni shambulio dhidi ya serikali na Waislamu pia.
Maisha ya watendaji wa dini nyingine katika jamii ya Kiislamu pia yalipewa hali ya ulinzi. Mtume akasema:
“Mwenye kumuua mtu ambaye ana mapatano na Waislamu hatasikia harufu ya Pepo.” (Saheeh Muslim)
Kwa vile wakubwa walikuwa pamoja na Waislamu, Mtume alionya vikali dhidi ya unyanyasaji wowote wa watu wa imani nyingine. Alisema:
“Jihadhari! Yeyote anayewadhulumu watu wachache wasiokuwa Waislamu, au anawapunguzia haki zao, au akawatwika zaidi ya uwezo wao, au akawanyang'anya chochote kwa hiari yao; Mimi (Mtume Muhammad) nitamlalamikia mtu huyo Siku ya Kiyama.” (Abu Dawud)
Kwa Kila Mmoja Dini Yake
Katika makala nyingine, inasema, “Wayahudi wana dini yao na Waislamu wana dini yao.” Katika hili, ni wazi kwamba jambo lolote lile isipokuwa uvumilivu lisingevumiliwa, na kwamba, ingawa wote walikuwa wanajamii, kila mmoja alikuwa na dini yake tofauti ambayo isingeweza kukiukwa. Kila mmoja aliruhusiwa kutenda imani yake kwa uhuru bila vizuizi vyovyote, na hakuna vitendo vya uchochezi ambavyo vingevumiliwa.
Kuna vifungu vingine vingi vya katiba hii ambavyo vinaweza kujadiliwa, lakini msisitizo utawekwa kwenye kifungu kinachosema, "Iwapo mzozo wowote au mabishano yatatokea, ni lazima yaelekezwe kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake." Kifungu hiki kilisisitiza kwamba wakazi wote wa dola lazima watambue mamlaka ya juu zaidi, na katika mambo yale yanayohusisha makabila na dini mbalimbali, haki isingeweza kutekelezwa na viongozi binafsi; bali ni lazima iamuliwe na kiongozi wa nchi mwenyewe au wawakilishi wake aliowateua. Iliruhusiwa, hata hivyo, kwa makabila ya watu binafsi ambao hawakuwa Waislamu, kurejelea maandiko yao ya kidini na wasomi wao kuhusiana na mambo yao binafsi. Wangeweza, kama wangeamua, kumwomba Mtume atoe hukumu baina yao katika mambo yao. Mwenyezi Mungu anasema katika Kurani:
“…Basi wakikujia, wahukumu baina yao au jipuuze nao....” (Kurani 5:42)
Hapa tunaona kwamba Mtume aliiruhusu kila dini ihukumu katika mambo yao wenyewe kwa mujibu wa maandiko yao wenyewe, ilimradi haikusimama kinyume na ibara za katiba, mapatano ambayo yalizingatia faida kubwa ya ushirikiano wa amani kuwepo kwa jamii.
Rejeleo la maelezo:
[1] Jumuiya ya Madina Wakati wa Mtume, Akram Diya al-Umari, Nyumba ya Kiislamu ya Kimataifa ya Uchapishaji, 1995.
Ongeza maoni