Uislam, katika Jamii ya Kisasa (sehemu ya 2 kati ya 2): Kauli Zaidi

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Kauli za wasomi mbali mbali wasio Waislamu kuhusu ukuu wa dini ya Uislamu kama jamii. Sehemu ya 2: Kauli zaidi.

  • Na iiie.net
  • Iliyochapishwa mnamo 01 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 4,489 (wastani wa kila siku: 4)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

A.J. Toynbee, Civilization on Trial, New York, 1948, uk. 205:

“Kutoweka kwa ufahamu wa asili kati ya Waislamu ni moja wapo ya mafanikio bora ya Uislamu na ulimwengu wa sasa. Kuna, kama inavyotokea, hitaji la muhimu la uenezaji wa fadhila hii ya Kiislam.”

A.M.L. Stoddard, aliyenukuliwa katika Islam – The Religion of All Prophets, Begum Bawani Waqf, Karachi, Pakistan, uk. 56:

“Kukuwa kwa Uislamu labda ni tukio la kushangaza zaidi katika historia ya mwanadamu. Kuibuka kutoka kwenye ardhi na watu ambao hawakudhaniwa, Uislamu ulienea kipndi cha karne zaidi ya nusu ya dunia, ukivunja falme kubwa, ukipindua dini zilizodumu kwa muda mrefu, ukirudisha roho za jamii, na kujenga ulimwengu mpya - ulimwengu wa Uislamu.

“Kadri tunavyochunguza maendeleo haya ndivyo inavyoonekana ya kushangaza zaidi. Dini zingine kubwa zilishinda polepole, kwa mapambano ya maumivu na mwisho zilishinda kwa msaada wa wafalme wenye nguvu waliobadilishwa kuwa na imani mpya. Ukristo ulikuwa na Konstantino wake, Ubudha Asoka wake, na Zoroastrianism ilikuwa na Koreshi, kila mmoja aliangukia kwenye ibada yake iliyolazimishwa katika utawala wake. Sio hivyo kwenye Uislamu. uliinuka katika ardhi ya jangwa lililokaliwa kidogo na jamii za kuhamahama ambazo hapo awali hazikujulikana katika historia za wanadamu, Uislam ulisafiri kwenda mbele kwenye ukubwa na uungwaji mkono wa kibinadamu dhidi ya mpingo wa nyenzo. Ila Uislamu ulishinda kwa urahisi na kunaonekana kuwa muujiza, na vizazi kadhaa viliona Mwezi Mwandamo wa Moto ukishinda kutoka Pyrenees hadi Himalaya na kutoka jangwa la Asia ya Kati hadi majangwa ya Afrika ya Kati.”

Edward Montet, "La Propaganda Chretienne it Adversaries Musulmans", Paris, 1890, iliyonukuliwa na T.W. Arnold katika kitabu cha The Preaching of Islam, London, 1913, uk. 413-414:

“Uislamu ni dini ambayo kimsingi ni ya kimantiki kwa maana pana zaidi ya neno hili inazingatiwa kietimolojia na kihistoria. Ufafanuzi wa kimantiki kama mfumo ambao wenye kutegemea imani ya kidini katika kanuni zilizowekwa na kwa sababu hiyo hutumika kwake hasa... Haiwezi kukataliwa kuwa mafundisho mengi na mifumo ya theolojia na mapokezi mengi, kutoka kwenye ibada ya watakatifu hadi utumiaji wa rozari na hirizi, zimepandikizwa kwenye shina kuu la imani ya Waislamu. Lakini licha ya maendeleo mengi, kwa kila maana ya neno, la mafundisho ya mtume, Kurani imekaa mahali pake kama msingi wa kuanzia, na mafundisho ya umoja wa Mungu yametangazwa humo ndani juu ya ukuu , utukufu, usafi usiobadilika na kwa kumbukumbu ya uhakika, ambayo ni ngumu kuipata kwa kupita nje ya rangi ya Uislamu. Uaminifu huu wa mafundisho ya msingi wa dini, msingi rahisi wa kanuni ambayo imetaja, uthibitisho ulioupata kutoka kwenye imani thabiti ya wahubiri waliyoieneza, kuna sababu nyingi sana za kuelezea mafanikio ya juhudi za uhubiri wa Muhammad. Imani iliyo sahihi sana, iliyovuliwa magumu yote ya kitheolojia na kwa hivyo kupatikana katika uelewa wa kawaida inaweza kutarajiwa kuwa nayo na hakika inamiliki nguvu ya kushangaza ya kushinda kwenye njia zake katika dhamiri za wanadamu.”

W. Montgomery Watt, Islam and Christianity Today, London, 1983, uk. 6:

“Mimi sio Muisllam kwa maana ya kawaida, ingawa ninatumahi kuwa mimi ni "Muislam" kama "mtu aliyejisalimisha kwa Mungu", lakini naamini kwamba yaliyomo ndani ya Kurani na maelezo mengine ya maono ya Uislam ni duka kubwa la ukweli wa kimungu ambao Mimi na Wamagharibi mengine bado tuna mengi ya kujifunza, na 'Uislamu hakika ni mshindani mkubwa wa kusambaza mfumo wa kimsingi wa dini moja ya baadaye.’”

Paul Varo Martinson (editor), ISLAM, An Introduction for Christians, Augsburg, Minneapolis, 1994, uk. 205:

“Uislamu ni imani halisi inayotengeneza mawazo ya majirani zetu Waislamu na huamua mtazamo wao maishani. Na pia imani ya Uislam kwa ujumla inahusu tamaduni zaidi kuliko sura ya sasa ya Magharibi katika imani ya Kikristo, ambayo inahusu maisha ya kawaida zaidi ya dini. Ila tutakuwa tupo sawa kwa jamii ya kiislam pindi tutakapo waelewa kutokana na msingi wao wa kidini na kuwaheshimu kama jamii ya imani. Waislamu wamekuwa washirika muhimu katika mazungumzo ya imani.”

John Alden Williams (mhariri), ISLAM, George Braziller, New York, 1962, ndani ya kifuniko cha vumbi:

“Uislamu ni zaidi ya dini: ni njia muhimu ya maisha. Katika njia nyingi ni suala la kuamua zaidi katika uzoefu wa wafuasi wake kuliko dini nyingine yoyote ya ulimwengu. Muislam ("Mwenye Kujisalimisha") anaishi ana kwa ana na Mungu wakati wote na hataanzisha utengano kati ya maisha yake na dini yake, siasa zake na imani yake. Kwa msisitizo wake mkubwa juu ya udugu wa wanadamu wanaoshirikiana kutimiza mapenzi ya Mungu, Uislamu umekuwa moja ya dini zenye ushawishi mkubwa ulimwengu wa leo.”

John L. Esposito, ISLAM, The Straight Path, Oxford University Press, New York, 1988, uk. 3-4:

“Uislamu unasimama katika mstari mrefu wa Wasemiti, mila za tabiri za kidini ambazo zinawakilisha imani ya Mungu mmoja, na imani katika ufunuo wa Mungu, manabii wake, uwajibikaji wa kimaadili na majukumu, na Siku ya Hukumu. Hakika, Waislam, kama Wakristo na Wayahudi, ni watoto wa Ibrahimu, kwani wote wanarudi katika uzao wa jamii yake. Uhusiano wa kihistoria wa kidini na kisiasa wa Uislamu na Jumuiya ya Wakristo na Uyahudi umebaki imara katika historia. Mwingiliano huu umekuwa chanzo cha manufaa na kuazimana pia na kutokuelewana na mizozo.”

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.