Uislam, katika Jamii ya Kisasa (sehemu 1 kati ya 2): Utangulizi

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Kauli za wasomi mbalimbali za wasiokuwa Waislamu juu ya ukuu wa dini ya Uislamu kama Jamii. Sehemu ya 1: Utangulizi.

  • Na iiie.net
  • Iliyochapishwa mnamo 02 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 19 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 3,667
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Islam__a_Profound_Civilization_(part_1_of_2)_001.jpgUislamu ambao ulifunuliwa kwa Muhammad, Mungu ampandishe, ni mwendelezo na hitimisho la dini zote zilizoteremshwa hapo awali, na kwa hivyo ni ya zama zote na watu wote. Hadhi hii ya Uislamu inadumishwa na ukweli dhahiri. Kwanza, hakuna kitabu kingine chochote kati ya vile vilivyofunuliwa ambacho kipo katika muundo na maudhui kama yale yaliyofunuliwa. Pili, hakuna dini nyingine iliyofunuliwa yenye madai yoyote ya kusadikisha yenye kutoa mwongozo katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu kwa zama zote. Lakini Uislamu unashughulikia ubinadamu kwa ujumla na hutoa mwongozo unaohusu shida zote za wanadamu. Kwa kuongezea, imehimili mtihani wa miaka elfu moja na mia nne na ina uwezo wote wa kuanzisha jamii bora kama ilivyokuwa chini ya uongozi wa Mtume wa mwisho Muhammad.

Ilikuwa ni muujiza kwa Nabii Muhammad kuweza kuwaleta hata maadui zake wakubwa kwenye kundi la Uislamu bila kuwa na rasilimali za kutosha. Waabudu sanamu, wafuasi vipofu wa kufuata njia za mababu zao, waendelezaji wa uhasama wa kikabila, na wanyanyasaji wa utu na damu za watu wakawa taifa lenye nidhamu zaidi chini ya uongozi wa Uislamu na Mtume wake. Uislamu ulifungulia mtazamo wa ukubwa wa kiroho na hadhi ya kibinadamu kwa kutangaza haki kama kigezo pekee cha sifa na heshima. Uislamu ulirekebisha maisha yao ya kijamii, kitamaduni, kimaadili na kibiashara kwa sheria na kanuni za msingi ambazo zinaambatana na maumbile ya mwanadamu hivyo kuweza kutumika zama zote kwa kuwa maumbile ya mwanadamu hayabadiliki.

Kwa bahati mbaya Wakristo wa Magharibi badala ya kujaribu kwa dhati kuyaelewa mafanikio mazuri ya Uislamu wakati wa mwanzo, wao waliiona kama dini pinzani. Wakati wa karne za Vita vya Msalaba, mwelekeo huu ulipata nguvu nyingi na msukumo na idadi kubwa ya machapisho yalitolewa ili kuichafua taswira ya Uislamu. Lakini Uislamu umeanza kufunua ukweli wake kwa wasomi wa kisasa ambao uchunguzi wao wa kijasiri na madhubuti juu ya Uislamu kwa kujibu madai yote yaliyowekwa dhidi ya Uislamu na wale wanaojiita wataalamu wa kimashariki wasioegemea upande wowote.

Hapa tunaona maoni juu ya Uislamu kutoka kwa wanazuoni wasio Waislamu wa wakati wa sasa. Ukweli hauitaji utetezi wa kuuombea kwa niaba yake, lakini propaganda mbaya ya muda mrefu dhidi ya Uislamu imesababisha mkanganyiko mkubwa hata katika akili za wanafikra na waoni huru.

Tunatumai ya kwamba uchunguzi ufuatao utachangia katika kuanzisha tathmini yenye lengo ya Uislam.

Canon Taylor, Karatasi iliyosomwa mbele ya Bunge la Kanisa la huko Walverhamton, Oktoba 7, 1887, Imenukuliwa na Arnond katika kitabu cha The Preaching of Islam, uk. 71-72:

“Ni (Uislamu) ulibadilisha unyani na ubinadamu. Ilitoa tumaini kwa mtumwa, udugu kwa wanadamu, na kutambua ukweli wa kimsingi wa asili ya mwanadamu.”

Sarojini Naidu, Mahubuiri juu ya “The Ideals of Islam”, angalia Hotuba na Machapisho ya Sarojini Naidu, Madras, 1918, p. 167:

“Hisia ya haki ni moja wapo ya maoni mazuri ya Uislam, kwa sababu nikiwa nasoma Kurani nilipata kanuni hizo za maisha, sio za mafumbo lakini maadili ya vitendo katika maisha ya kila siku yanayofaa ulimwenguni kote.”

De Lacy O'Leary, Islam at the Crossroads, London, 1923, uk. 8:

“Historia inaweka wazi, kuwa simulizi ya Waislamu shupavu wanaotapakaa ulimwenguni na kuulazimisha Uislamu kwa njia ya upanga kwenye jamii zilizoshindwa ni moja wapo ya simulizi za ajabu sana ambazo wanahistoria wamewahi kuzirudia.”

H.A.R. Gibb, Whither Islam, London, 1932, p. 379:

“Ila Uislamu bado una kazi zaidi ya kujitoa kwa sababu ya wanadamu. Inasimama karibu kabisa na Mashariki kuliko Ulaya, na ina mila nzuri ya uelewa na ushirikiano wa kikabila. Hakuna jamii nyingine iliyo na rekodi kama hiyo ya mafanikio katika kuungana katika usawa wa hadhi, nafasi, na jitihada nyingi na asili mbalimbali za wanadamu ... Uislamu bado una nguvu ya kupatanisha mambo ambayo hayafanani ya asili na tamaduni. Ikiwa upinzani wa jamii kubwa za Mashariki na Magharibi utabadilishwa na ushirikiano, upatanishi wa Uislamu utakuwa wa lazima. Katika mikono yake lipo suluhisho la shida ambayo Ulaya inakabiliwa nayo katika uhusiano wake na Mashariki. Ikiwa wataungana, matumaini ya kuimarika kwa amani hautapimika. Ila ikiwa Ulaya,itakataa ushirikiano huu wa Uislamu, inaitupa mikononi mwa wapinzani wake, suala hilo linaweza kuwa baya kwa wote wawili.”

G.B. Shaw, The Genuine Islam, Juzuu. 1, Nambari. 81936:

“Nimekuwa nikiishikilia dini ya Muhammad kwa makadirio ya juu kwa sababu ya uhai wake mzuri. Ni dini pekee inayoonekana kwangu kumiliki uwezo huo wa kuingiza mabadiliko ya maisha ambayo inaweza kujiweka katika kila kizazi. Nimemsoma - mtu mzuri na kwa maoni yangu yupo mbali na kuwa mpinga Kristo, lazima aitwe Mwokozi wa Wanadamu. Ninaamini kuwa ikiwa mtu kama yeye angeuchukua udikteta wa ulimwengu wa sasa, angefanikiwa kutatua shida zake kwa njia ambayo italeta amani na furaha inayohitajika sana: Nimetabiri juu ya imani ya Muhammad kuwa itakubalika na Ulaya ya kesho kwani inaanza kukubalika na Ulaya ya leo.”

Mbaya Nzuri zaidi

Uislam, katika Jamii ya Kisasa (sehemu ya 2 kati ya 2): Kauli Zaidi

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Kauli za wasomi mbali mbali wasio Waislamu kuhusu ukuu wa dini ya Uislamu kama jamii. Sehemu ya 2: Kauli zaidi.

  • Na iiie.net
  • Iliyochapishwa mnamo 01 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 3,703
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

A.J. Toynbee, Civilization on Trial, New York, 1948, uk. 205:

“Kutoweka kwa ufahamu wa asili kati ya Waislamu ni moja wapo ya mafanikio bora ya Uislamu na ulimwengu wa sasa. Kuna, kama inavyotokea, hitaji la muhimu la uenezaji wa fadhila hii ya Kiislam.”

A.M.L. Stoddard, aliyenukuliwa katika Islam – The Religion of All Prophets, Begum Bawani Waqf, Karachi, Pakistan, uk. 56:

“Kukuwa kwa Uislamu labda ni tukio la kushangaza zaidi katika historia ya mwanadamu. Kuibuka kutoka kwenye ardhi na watu ambao hawakudhaniwa, Uislamu ulienea kipndi cha karne zaidi ya nusu ya dunia, ukivunja falme kubwa, ukipindua dini zilizodumu kwa muda mrefu, ukirudisha roho za jamii, na kujenga ulimwengu mpya - ulimwengu wa Uislamu.

“Kadri tunavyochunguza maendeleo haya ndivyo inavyoonekana ya kushangaza zaidi. Dini zingine kubwa zilishinda polepole, kwa mapambano ya maumivu na mwisho zilishinda kwa msaada wa wafalme wenye nguvu waliobadilishwa kuwa na imani mpya. Ukristo ulikuwa na Konstantino wake, Ubudha Asoka wake, na Zoroastrianism ilikuwa na Koreshi, kila mmoja aliangukia kwenye ibada yake iliyolazimishwa katika utawala wake. Sio hivyo kwenye Uislamu. uliinuka katika ardhi ya jangwa lililokaliwa kidogo na jamii za kuhamahama ambazo hapo awali hazikujulikana katika historia za wanadamu, Uislam ulisafiri kwenda mbele kwenye ukubwa na uungwaji mkono wa kibinadamu dhidi ya mpingo wa nyenzo. Ila Uislamu ulishinda kwa urahisi na kunaonekana kuwa muujiza, na vizazi kadhaa viliona Mwezi Mwandamo wa Moto ukishinda kutoka Pyrenees hadi Himalaya na kutoka jangwa la Asia ya Kati hadi majangwa ya Afrika ya Kati.”

Edward Montet, "La Propaganda Chretienne it Adversaries Musulmans", Paris, 1890, iliyonukuliwa na T.W. Arnold katika kitabu cha The Preaching of Islam, London, 1913, uk. 413-414:

“Uislamu ni dini ambayo kimsingi ni ya kimantiki kwa maana pana zaidi ya neno hili inazingatiwa kietimolojia na kihistoria. Ufafanuzi wa kimantiki kama mfumo ambao wenye kutegemea imani ya kidini katika kanuni zilizowekwa na kwa sababu hiyo hutumika kwake hasa... Haiwezi kukataliwa kuwa mafundisho mengi na mifumo ya theolojia na mapokezi mengi, kutoka kwenye ibada ya watakatifu hadi utumiaji wa rozari na hirizi, zimepandikizwa kwenye shina kuu la imani ya Waislamu. Lakini licha ya maendeleo mengi, kwa kila maana ya neno, la mafundisho ya mtume, Kurani imekaa mahali pake kama msingi wa kuanzia, na mafundisho ya umoja wa Mungu yametangazwa humo ndani juu ya ukuu , utukufu, usafi usiobadilika na kwa kumbukumbu ya uhakika, ambayo ni ngumu kuipata kwa kupita nje ya rangi ya Uislamu. Uaminifu huu wa mafundisho ya msingi wa dini, msingi rahisi wa kanuni ambayo imetaja, uthibitisho ulioupata kutoka kwenye imani thabiti ya wahubiri waliyoieneza, kuna sababu nyingi sana za kuelezea mafanikio ya juhudi za uhubiri wa Muhammad. Imani iliyo sahihi sana, iliyovuliwa magumu yote ya kitheolojia na kwa hivyo kupatikana katika uelewa wa kawaida inaweza kutarajiwa kuwa nayo na hakika inamiliki nguvu ya kushangaza ya kushinda kwenye njia zake katika dhamiri za wanadamu.”

W. Montgomery Watt, Islam and Christianity Today, London, 1983, uk. 6:

“Mimi sio Muisllam kwa maana ya kawaida, ingawa ninatumahi kuwa mimi ni "Muislam" kama "mtu aliyejisalimisha kwa Mungu", lakini naamini kwamba yaliyomo ndani ya Kurani na maelezo mengine ya maono ya Uislam ni duka kubwa la ukweli wa kimungu ambao Mimi na Wamagharibi mengine bado tuna mengi ya kujifunza, na 'Uislamu hakika ni mshindani mkubwa wa kusambaza mfumo wa kimsingi wa dini moja ya baadaye.’”

Paul Varo Martinson (editor), ISLAM, An Introduction for Christians, Augsburg, Minneapolis, 1994, uk. 205:

“Uislamu ni imani halisi inayotengeneza mawazo ya majirani zetu Waislamu na huamua mtazamo wao maishani. Na pia imani ya Uislam kwa ujumla inahusu tamaduni zaidi kuliko sura ya sasa ya Magharibi katika imani ya Kikristo, ambayo inahusu maisha ya kawaida zaidi ya dini. Ila tutakuwa tupo sawa kwa jamii ya kiislam pindi tutakapo waelewa kutokana na msingi wao wa kidini na kuwaheshimu kama jamii ya imani. Waislamu wamekuwa washirika muhimu katika mazungumzo ya imani.”

John Alden Williams (mhariri), ISLAM, George Braziller, New York, 1962, ndani ya kifuniko cha vumbi:

“Uislamu ni zaidi ya dini: ni njia muhimu ya maisha. Katika njia nyingi ni suala la kuamua zaidi katika uzoefu wa wafuasi wake kuliko dini nyingine yoyote ya ulimwengu. Muislam ("Mwenye Kujisalimisha") anaishi ana kwa ana na Mungu wakati wote na hataanzisha utengano kati ya maisha yake na dini yake, siasa zake na imani yake. Kwa msisitizo wake mkubwa juu ya udugu wa wanadamu wanaoshirikiana kutimiza mapenzi ya Mungu, Uislamu umekuwa moja ya dini zenye ushawishi mkubwa ulimwengu wa leo.”

John L. Esposito, ISLAM, The Straight Path, Oxford University Press, New York, 1988, uk. 3-4:

“Uislamu unasimama katika mstari mrefu wa Wasemiti, mila za tabiri za kidini ambazo zinawakilisha imani ya Mungu mmoja, na imani katika ufunuo wa Mungu, manabii wake, uwajibikaji wa kimaadili na majukumu, na Siku ya Hukumu. Hakika, Waislam, kama Wakristo na Wayahudi, ni watoto wa Ibrahimu, kwani wote wanarudi katika uzao wa jamii yake. Uhusiano wa kihistoria wa kidini na kisiasa wa Uislamu na Jumuiya ya Wakristo na Uyahudi umebaki imara katika historia. Mwingiliano huu umekuwa chanzo cha manufaa na kuazimana pia na kutokuelewana na mizozo.”

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

(Soma zaidi...) Ondoa