Hadithi ya Adam (sehemu ya 4 kati ya 5): Maisha Duniani

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Adamu, watoto wake, mauaji ya kwanza na kifo chake.

 • Na Aisha Stacey (© 2008 IslamReligion.com)
 • Iliyochapishwa mnamo 09 Dec 2021
 • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
 • Ilichapishwa: 2
 • Imetazamwa: 6,447 (wastani wa kila siku: 9)
 • Ukadiriaji: bado hakuna
 • Imekadiriwa na: 0
 • Imetumwa kwa barua pepe: 0
 • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Adam na Hawa waliondoka Peponi na kuanza maisha yao duniani. Mungu alikuwa amewaandaa kwa njia nyingi. Aliwapa uzoefu wa kujitahidi dhidi ya minong'ono na hila za Shetani. Alimfundisha Adam majina ya kila kitu na akamuagiza katika mali na manufaa yake. Adam alichukua nafasi yake kama mlinzi wa ardhi na Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Adam, Mtume wa kwanza wa Mwenyezi Mungu alikuwa na jukumu la kumfundisha mkewe na kizazi chake jinsi ya kumwabudu Mwenyezi Mungu na kuomba msamaha Kwake. Adam alianzisha sheria za Mungu na kutekeleza mahitaji ya familia yake na kudhibiti na kuitunza dunia. Kazi yake ilikuwakudumisha, kupalilia, kujenga na kuongeza idadi ya watu; alipaswa kulea watoto ambao wangeishi kulingana na maagizo ya Mungu vile vile kutunza na kuboresha dunia.

Watoto Wanne wa Kwanza wa Adam

Watoto wa kwanza wa Adam na Hawa, walikuwa mapacha,; Kaini na dadake, walifuatwa upesi na seti nyingine ya mapacha, Habili na dadake. Adam na familia yake waliishi kwa amani na maelewano. Kaini alikuwa mkulima huku Habili akiwa mfungaji. Siku zilipita na hatimaye wakati uliwadia kwa watoto wavulana wa Adam kufunga ndoa. Simulizi ya kikundi cha masahaba wa Mtume Muhammad akiwemo Ibn Abbas na Ibn Masud ya kwamba ilikuwa ni desturi ya kufungisha ndoa baina ya mwanamume wa mimba moja na mwanamke wa mimba nyingine miongoni wa watoto wa Adam. Kwa hiyo, tunajua kwamba mpango wa Mungu wa kuijaza dunia ulichangiwa na kila mmoja wa wana wa Adam kuoa dada Pacha wa yule mwingine.

Tangu jadi, inaonekana kuwa urembo ulichangia katika kivutio cha wanaume na wanawake. Kaini hakupendezwa na mchumba aliyechaguliwa kwa ajili yake. Kaini alianza kumuonea wivu nduguye na kukataa kutii amri ya babake, kitendo hicho kilisababisha yeye kutomtii Mungu. Mungu alimuumba mwanadamu akiwa na tabia njema na mbaya, na jitihada za kufanikisha ni sehemu moja ya majaribioYake kwetu.

Mungu aliamuru kwamba kila mtoto wa kiume alipaswa kutoa kafara. Hukumu yake ingempendekeza kulingana na sadaka itakayokubaliwa zaidi. Kaini alitoa nafaka yake mbaya zaidi, huku Habili ​​akitoa mfugo wake bora zaidi. Mungu alikubali sadaka ya habili, kwa hiyo, Kaini alikasirika na kumtishia kumuua nduguye.

“Na wasomee khabari za wana wawili wa Adam kwa kweli. Walipo toa mhanga, ukakubaliwa wa mmoja wao, na wa mwengine haukukubaliwa. Akasema: Nitakuuwa. ’” (Kurani 5:27)

Habili alimshauri kaka yake kwamba Mwenyezi Mungu atakubali matendo mema kutoka kwa wale wachamungu na wenye kumtii, lakini anakataa matendo mema ya walio na kiburi, ubinafsi na wasiomtii Mungu.

“Akasema: Nitakuuwa. Akasema mwengine: Mwenyezi Mungu huwapokelea wachamngu. Ukininyooshea mkono wako kuniuwa, mimi sitakunyooshea mkono wangu kukuuwa. Hakika mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote.’” (Kurani 5:27-28)

Mauaji ya Kwanza

“Basi nafsi yake ikampelekea kumuuwa nduguye, akamuuwa na akawa miongoni mwa wenye kukhasirika..” (Kurani 5:30)

Mtume Muhammad alitufahamisha kwamba Kaini alikasirika na kumpiga kaka yake kichwani kwa kipande cha chuma. Pia ilisemwa katika simulizi nyingine kwamba Kaini alimpiga Habili ​​kichwani alipokuwa amelala.

“Hapo Mwenyezi Mungu akamleta kunguru anaye fukua katika ardhi ili amwonyeshe vipi kumsitiri nduguye Akasema: Ole wangu!

Nimeshindwa kuwa kama kunguru huyu nikamsitiri ndugu yangu? Basi akawa miongoni mwa wenye kujuta.” (Kurani 5:31)

Adam alihuzunika; kwa kuwa alikuwa amewapoteza wanawe wa kwanza na wa pili. Mmoja alikuwa ameuawa; na mwengine ilishinikizwa na adui mkuu wa wanadamu - Shetani. Adam alisali kwa utulivu kwa ajili ya mwana wake, na kuendelea kuishughulikia dunia. Aliwafundisha watoto na wajukuu zake wengi kuhusu Mungu. Aliwaambia juu ya kukutana kwake mwenyewe na Shetani na akawashauri wajihadhari na hila na njama za Shetani. Miaka mingi ilipita, na Adam alizeeka na watoto wake wakaenea duniani kote.

Kifo cha Adam

Wanadamu wote ni watoto wa Adam. Katika simulizi moja, Mtume Muhammad alitufahamishakwamba Mungu alimwonyesha Adam kizazi chake. Adam aliona nuru inayopendeza machoni mwa Mtume Daudi na akampenda, hivyo basi, akamgeukia Mwenyezi Mungu na akasema: “Ee Mwenyezi Mungu! Mpe miaka arobaini kutoka kwa maisha yangu.” Mungu alitakabali dua ya Adam, nalo likaandikwa na likatekelezwa.

Muda wa maisha ya Adam ulipaswa kuwa miaka 1000 lakini baada ya miaka 960 Malaika wa mauti alimjia Adam. Adam alishangaa na kusema "lakini bado nina miaka 40 ya kuishi". Malaika wa mauti alimkumbusha zawadi yake ya miaka 40 kwa kizazi chake kipenzi Mtume Daudi, lakini Adam akakana.Miaka mingi sana baadaye, Mtume wa mwisho Muhammad alisema Adam alikanusha hivyo hivyo na wana wa Adam wakakanusha bile vile, Adam akasahau na wanawe pia wakasahau; Adamu alifanya makosa na watoto wake pia hufanya makosa.” (At-Tirmidhi)

Katika lugha ya Kiarabu neno la mwanadamu ni insan na linatokana na chanzo la neno nisyan ambayo ni kusahau. Hii ni hali halisi ya maisha ya mwanadamu, mwanadamu ni mwepesi wa kusahau, na pindi tunaposahau tunakana na kukataa. Adam alisahau (na hakuwa mwongo), na Mungu akamsamehe. Kisha, Adam aliukubali wito wa Mwenyezi Mungu na hatimaye akafa. Malaika walishuka na kuuosha mwili wa Mtume Adam kwa idadi isiyo ya kawaida; walichimba kaburi na kuuzika mwili wa baba ya wanadamu, Adam.

Mrithi wa Adam

Kabla ya kifo chake Adam aliwakumbusha watoto wake kwamba Mungu hatawaacha peke yao au bila mwongozo. Aliwaambia Mungu angewatuma Mitume wengine wenye majina ya kipekee, sifa na miujiza, lakini wote watakuwa na lengo moja - ibada ya Kweli kwa Mungu Mmoja. Adam alimteua mwanawe Sethi kuwa mrithi wake.


Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

 • (Haitaonyeshwa kwa umma)

 • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

  Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.