Mwenyezi Mungu ni al-Hakeem – Mwenye Hekima

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Ufafanuzi wa majina mawili ya Mungu ambayo yanaonyesha kwamba matendo yake yote yana hekima ndani yake na kwamba haki yake ni kamilifu.

 • Na islamtoday.net [edited by IslamReligion.com]
 • Iliyochapishwa mnamo 08 Dec 2021
 • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
 • Ilichapishwa: 0
 • Imetazamwa: 1,482 (wastani wa kila siku: 2)
 • Ukadiriaji: bado hakuna
 • Imekadiriwa na: 0
 • Imetumwa kwa barua pepe: 0
 • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

God_is_al-Hakeem_-_the_Wise._001.jpgKurani inataja majina mawili ya Mungu ambayo yanahusiana sana ki lugha. La kwanza ni al-Hakeem (Mwenye hekima) na la pili ni al-Haakim (Hakimu). Mungu anatajwa katika Kurani kama "Mwenye hekima" mara 93 na "Hakimu" mara sita.

Kwa mfano, Mungu anasema:

"Hakika Wewe ndiye Mjuzi Mwenye hikima." (Kurani 2:32) na "…Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima." (Kurani 2:129).

"Na ndiye Mwenye hikima na Mwenye khabari zote." (Kurani 6:18)

"Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu Mwenye hikima. (Kurani 4:130)

Mungu anajitambua yeye kama Hakimu anaposema: "Je, nimtafute hakimu ghairi ya Mwenyezi Mungu, naye ndiye aliye kuteremshieni Kitabu kilicho elezwa waziwazi?" (Kurani 6:114)

Na: "Naye ndiye Mbora wa wenye kuhukumu." (Kurani 7:87)

Na pale Anaposema: "Na Nuhu alimwomba Mola wake Mlezi: ‘Ee Mola Mlezi wangu! Hakika mwanangu ni katika ahali zangu, na hakika ahadi yako ni haki. Na Wewe ni Mwenye haki kuliko mahakimu wote!’" (Kurani 11:45)

Na: "Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote?" (Kurani 95:8)

Hekima ya Mungu

Kuwa na hekima kuna maanisha kujua mambo jinsi yalivyo, kuyatendea ipasavyo, na kumudu kila kitu mahali pake na kazi yake ipasavyo. Mungu anasema kuhusu uumbaji wake: "Na unaiona milima unaidhunia imetulia; nayo inakwenda kama mwendo wa mawingu. Huo ndio ufundi wa Mwenyezi Mungu aliye tengeneza vilivyo kila kitu." (Kurani 27:88)

Hekima ya Mungu inaweza kushuhudiwa katika uumbaji Wake, na hasa katika uumbaji wa mwanadamu, pamoja na akili na nafsi yake. Mungu anatuambia kwamba alimuumba mwanadamu katika umbo bora kabisa:

"Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa. Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini, Lakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira usio kwisha. Basi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo? Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote?" (Kurani 95:4-8)

Hekima ya Kibinadamu

Mwenyezi Mungu ni Mwenye hekima ambaye huwapa hikima wale anao wapenda miongoni mwa waja wake. Mungu anasema: "Yeye humpa hikima amtakaye; na aliye pewa hikima bila ya shaka amepewa kheri nyingi. Na hawakumbuki ila wenye akili." (Kurani 2:269)

Mungu huwapa watu fulani uwezo wa pekee wa kuchunguza matatizo na kupata masuluhisho yanayoweza kutekelezeka, ambao wanapokabiliwa na matatizo au ugumu wanaweza kupima kila jambo kwa njia ifaayo na yenye usawa. Hawa ni watu ambao wengine hushauriana nao na kuwategemea katika nyanja mbalimbali za maisha yao. Watu wengine wana hekima kuhusu masuala ya kijamii. Wengine wana hekima linapokuja suala la mahusiano baina ya watu. Wapo wenye busara linapokuja suala la uchumi.

Nyanja ya ushauri ni muhimu sana kwa sasa. Washauri wengi waliofanikiwa ni watu ambao Mungu amewabariki hekima katika nyanja zao ili kutimiza maarifa, ufahamu, na uzoefu wao.

Ni lazima tutambue kwamba hekima inaweza kuwa maalumu. Mtu anaweza kuwa na hekima nyingi katika sehemu moja au zaidi ya maisha, bila kuwa na hekima katika kila njia. Mtu anaweza kuwa na hekima katika mambo ya kidunia bila ya kuwa na hekima katika mambo ya imani, hakika bila hata ya kuwa muumini.

Mungu: Hakimu Mkuu

Mungu ana ukuu juu ya mambo yote katika uumbaji. Hili linawasilishwa kwa jina al-Hakam, ambalo linaonekana katika aya ifuatayo: "Je, nimtafute hakimu ghairi ya Mwenyezi Mungu, naye ndiye aliye kuteremshieni Kitabu kilicho elezwa waziwazi?" (Kurani 6:114)

Zaidi ya hayo, hakuna kinachotokea katika uumbaji isipokuwa kwa mamlaka na amri Yake. Mungu anasema: "Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo." (Kurani 55:29)

Vivyo hivyo, amri Yake inaweza kuwa ya asili kisheria. Mungu huhalalisha baadhi ya matendo na matendo mengine kuwa dhambi. Anatuamuru kufanya mambo fulani na kutukataza kufanya mengine. Amri yake haiwezi kubadilishwa au kupinduliwa na mtu yeyote. Mungu anasema: "Fahamuni! Kuumba na amri ni zake." (Kurani 7:54)

Kurani inamtaja Mungu kama "Mbora wa Mahakimu." Huu ni uthibitisho wa haki yake kamilifu na rehema kubwa. Kamwe Mungu hamdhulumu mtu yeyote na hadhulumu. Sheria anazowawekea waja wake si mzigo wala haiwi isiyo na haki. Bali mafundisho ya kweli ya Uislamu yanasimamia haki za watu wote bila ya upendeleo: mtawala na mtawaliwa, mwenye nguvu na dhaifu, mwanaume na mwanamke, mwadilifu na mtenda dhambi, muumini na kafiri. Inasimamia haki zao wakati wa amani na wakati wa vita, na katika hali zote bila ubaguzi.

Ndio maana Waislamu warejee Kurani na Sunna (mafundisho) ya Mtume, rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kwa ajili ya mwongozo katika mambo yote. Wanapaswa kufanya hivyo kama watu binafsi ili kuwaongoza katika maisha yao binafsi, na wanapaswa kufanya hivyo kama jumuiya, jamii, na mataifa kwa mwongozo katika masuala yao ya kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Mwenyezi Mungu ni Mwenye hekima na ndiye Hakimu mwadilifu. Katika imani za Kiislamu, hakuna mtu anayeeleweka kubeba dhambi ya mwingine. Hakuna anayekosewa na Mungu. Hakuna mtenda dhambi anayeadhibiwa zaidi ya ukubwa wa dhambi iliyotendwa na hakuna jambo jema linalopita bila malipo.

Mungu anasema: "Hakika wale walio amini na wakatenda mema - hakika Sisi hatupotezi ujira wa anaye tenda mema." (Kurani 18:30)

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

 • (Haitaonyeshwa kwa umma)

 • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

  Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.