Agano Jipya

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Angalia kile wasomi wa Kikristo wa Kiyahudi wanasema juu ya ukweli na uhifadhi wa Agano Jipya.

  • Na Laurence B. Brown, MD
  • Iliyochapishwa mnamo 19 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 1,820 (wastani wa kila siku: 2)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Wote tunasoma biblia mchana na usiku,

ila wewe unasoma nyeusi mimi ninasoma nyeupe.

—William Blake, The Everlasting

Injili

The_New_Testament_001.jpgHakika, hisia za Blake katika nukuu ya hapo juu sio jambo jipya. Agano Jipya lina utofauti wa kutosha kwa kuzalisha tafsiri mbali mbali, imani na dini, zote zinazodaiwa ni za Biblia. Kwa hivyo, tunamwuona mwandishi mmoja akitoa maoni ya kufurahisha :

Unaweza na hauwezi,

Utakuwa na hautakuwa,

Utafanya na hautafanya,

Na utalaaniwa ikiwa uta,

Na hautalaaniwa ikiwa hauta.[1]

Kwa nini kuna kutofautiana katika maoni hayo? Mwanzo kabisa, kambi tofauti za kitheolojia hazikubaliani ni vitabu gani vinapaswa kuingizwa katika Biblia. Kambi moja ya Apocrypha ni maandiko ya mwingine. Pili, hata kati ya vitabu hivyo ambavyo vimetangazwa kuwa vitakatifu, maandishi mbali mbali ya vyanzo hayana usawa. Upungufu huu wa usawa uko kila mahali ambapo The Interpreter’s Dictionary of the Bible inasema, "Ni salama kusema kuwa hakuna sentensi moja katika NT (Agano Jipya) ambayo inafanana kabisa na MS [andiko].''[2]

Siyo sentesi hata moja? Hatuwezi kuiamini sentesi moja ya biblia? Ngumu kuamini.

Labda

Ukweli ni kwamba kuna zaidi ya maandiko 5700 ya Kigiriki katika Agano Jipya lote au sehemu.[3] Tena, “hakuna usawa katika maandiko haya mawili katika maelezo hayo yote…. Na baadhi ya tofauti hizi ni za muhimu sana”[4] Katika maandiko takriban elfu kumi za Vulgate ya Kilatini, ongeza aina zingine nyingi za zamani (i.e., Syriac, Coptic, Armenian, Georgia, Ethiopia, Nubian, Gothic, Slavonic), sasa tuna nini?

Maandiko mengi

Maandiko mengi ambayo yalishindwa kuendana katika maeneo na mara kwa mara kupingana. Wasomi wanakadiria idadi mbalimbali za maandiko yapo mamia kwa maelfu, wengine wanakadiria kuwa juu ya 400,000.[5] Bart D. Ehrman’s katika maneno yake maarufu, “Labda ni rahisi kuliweka jambo kwa kulinganisha: kuna utofauti mwingi katika maandiko yetu kuliko maneno katika Agano Jipya.”[6]

Hii imetokea vipi?

Utunzaji dhaifu. Udanganyifu. Uzembe. Upendeleo wa Mafundisho. Fanya uchaguzi.

Hakuna maandiko yoyote ya asili yaliyosalimika tangu kipindi cha Ukristo wa mwanzo.[7]/[8] Maandiko kamili ya zamani zaidi (Vatican MS. No. 1209 na Sinaitic Syriac Codex) ni za karne ya nne, miaka mia tatu baada ya uongozi wa Yesu. Lakini nakala za asili? Zilipotea. Na nakala za asili? Pia zimepotea. Maandiko yetu ya zamani zaidi, kwa maneno mengine, ni nakala za nakala za nakala za hakuna mtu anayejua-ni-nakala ngapi za asili.

Ndio sababu aishangazi kutofautiana

Katika mikono mizuri, kunakili makosa hakushangazi. Ila, maandiko ya Agano Jipya hayakuwa katika mikono mizuri. Katika kipindi cha chimbuko la Ukristo, waandishi walikuwa wasio na mafunzo, wasioaminika, wasio na uwezo, na wakati mwingine hawajui kusoma na kuandika.[9] Wale ambao walikuwa na ulemavu wa kuona wangeweza kufanya makosa ya kiherufi na maneno yanayofanana, wakati wale ambao walikuwa na ulemavu wa kusikia wanaweza kuwa walifanya makosa katika kunakili maandiko wakati yalipokuwa yanasomwa kwa sauti. Mara kwa mara waandishi walikuwa wakifanya kazi kupita kiasi, na kwa hivyo kupelekea kufanya makosa ambayo yanaambatana na uchovu.

Kwa maneno ya Metzger na Ehrman, "Kwa kuwa wengi, ikiwa sio wote, hao [waandishi] walikuwa wageni katika sanaa ya kunakili, idadi kubwa ya makosa bila shaka yaliingia kwenye maandishi yao wakati wanayatengeneza.”[10] Mbaya zaidi, waandishi wengine waliruhusu ubaguzi wa kimafundisho kuathiri uwasilishwaji wao wa maandiko.[11] Kama Ehrman asemavyo, "Waandishi ambao walinakili maandishi hayo waliyabadilisha." [12] Hasa zaidi, "Idadi ya mabadiliko ya makusudi yaliyofanywa kwa maslai ya muandishi ni ngumu kuyatathmini."[13] Na Pia la zaidi, "Kwa maoni ya kiufundi ya ukosoaji wa waandishi - ambayo ninahifadhi kwa muhimu mkubwa - waandishi hawa 'walichafua' maandishi yao kwa sababu za kitheolojia."[14]

Makosa yaliletwa kwa njia ya nyongeza, kufutwa, kubadilisha na kurekebishwa, kwa kawaida inakuwa maneno au mistari, lakini mara kwa mara inakuwa aya nzima.[15] [16] Kwa hakika, "mabadiliko mengi na nyongeza ziliingia kwenye maandishi,"[17] na matokeo yake kuwa "mashahidi wote wanaojulikana wa Agano Jipya wamechanganywa kwa kiwango kikubwa au kidogo, na hata maandiko kadhaa za mwanzo hayana makosa mengi."[18]

Katika Kumnukuu Yesu vibaya, Ehrman anatoa ushahidi wenye kushawishi kwamba hadithi ya yule mwanamke aliyechukuliwa katika uzinzi (Yohana 7: 53-8: 12) na aya za kumi na mbili za mwisho za Marko hazikuwa kwenye injili ya asili, lakini ziliongezwa na waandishi wa baadaye.[19] Cha kuongezea, mifano hii "inawakilisha sehemu mbili tu kati ya maelfu ya sehemu ambazo maadiko ya Agano Jipya yalibadilishwa na waandishi."[20]

Kwa hakika,vitabu vyote vya biblia vilighushiwa.[21] Hii haimaanishi kuwa maudhui yake siyo sahihi, lakini kwa hakika haimaanishi kuwa yapo sawa. Sasa ni vitabu gani vilighushiwa? Waefeso, Wakolosai, 2 Wathesalonike, 1 na 2 Timotheo, Tito, 1 na 2 Petro, na Yuda — ambavyo ni vitabu tisa kati ya ishirini na saba vya Agano Jipya na waraka—kwa kiwango kimoja au kutuhumiwa kwa kiwango fulani.[22]

Vitabu vya kughushi? Kwenye Biblia?

Kwa nini hatushangai? Kwa haya, hata waandishi wa injili hawajulikani. Kiuhakika, hawatambuliki.[23] Wasomi wa kibiblia ni adimu, kama wapo, waandishi wa uandishi kwa injili ya Mathayo, Marko, Luka, au Yohana. Kama vile Ehrman anatuambia, "Wasomi wengi leo wameacha utambulisho huu, na wanatambua kuwa vitabu hivyo viliandikwa na Wakristo wanao okuongea (na kuandika) vizuri Kigiriki wakati wa nusu ya pili ya karne ya kwanza."[24] Graham Stanton anathibitisha, "Injili, tofauti na maandiko mengi ya Wagiriki na Warumi, haijulikani. Vichwa ya habari vinavyojulikana ambavyo vinatoa jina la mwandishi (‘Injili kulingana na…’) havikuwa sehemu ya maandiko ya asili, kwaajili hiyo viliongezwa mwanzo wa karne ya pili. ”[25]

Hivyo, ikiwa kuna chochote, wanafunzi wa Yesu walikuwa na uhusiano gani na uandishi wa injili? Kidogo au hakuna wowote,kama tunavyojua. Ila hatuna sababu ya kuamini kuwa waliandika vitabu vyovyote vya Biblia. Kwa kuanza, hebu tukumbuke kuwa Marko alikuwa msaidizi wa Petro, na Luka alikuwa mwenzake Paulo. Mistari ya Luka 6: 14-16 na Mathayo 10: 2-4 huorodhesha wanafunzi kumi na wawili, na ingawa orodha hizi zinatofautiana juu ya majina mawili, Marko na Luka hawapo kwenye orodha yoyote. Kwa hivyo ni Mathayo na Yohana tu ndio walikuwa wanafunzi wa kweli. Lakini, hata hivyo wasomi wa sasa wanawakataa kuwa kama waandishi.

Kwanini?

Swali zuri. Yohana akiwa maarufu zaidi kati ya hao wawili, kwa nini tunamkataa kuwa mwandishi wa Injili ya "Yohana"?

Umm … kwasababu alikufa?

Vyanzo vingi vinakubali kuwa hakuna ushahidi, isipokuwa tu ushuhuda wenye kutiliwa shaka wa waandishi wa karne ya pili, kupendekeza kwamba mwanafunzi Yohana ndiye mwandishi wa Injili ya "Yohana."[26] [27] Labda mkanusho mkubwa ni kuwa mwanafunzi John anaaminika kufa ndani au karibu ya 98 CE.[28] Ila, Injili ya Yohana iliandikwa karibu ya 110 CE.[29] Kwa hiyo hakuwa Luka (mwenza wa Paulo), Marko (msaidizi wa Petro), na Yohana (asiyejulikana, na pia kwa hakika sio yule aliyekufa kwa kipindi kirefu), hatuna sababu ya kuamini injili yoyote iliandikwa na wanafunzi wa Yesu. . . .

Hakimiliki © 2007 Laurence B. Brown; Inatumika kwa ruhusa.

Dondoo ya hapo juu imechukuliwa kutoka kwenye kitabu kijacho cha Dkt. Brown, MisGod'ed, ambacho kinatarajiwa kuchapishwa pamoja na mwendelezo wake, God'ed. Vitabu vyote vinaweza kuangaliwa kwenye tovuti ya Dkt.Brown,www.Leveltruth.com. Dkt. Brown anaweza kupatikana kwa BrownL38@yahoo.com



Rejeleo la maelezo:

[1] Dow, Lorenzo. Reflections on the Love of God.

[2] Buttrick, George Arthur (Mh.). 1962 (Magazeti ya 1996). The Interpreter’s Dictionary of the Bible. Toleo la 4. Nashville: Abingdon Press. pp. 594-595 (Chini ya Matini, AJ).

[3] Ehrman, Bart D. Misquoting Jesus. Uk. 88.

[4] Ehrman, Bart D. Lost Christianities. Uk. 78.

[5] Ehrman, Bart D. Misquoting Jesus. Uk. 89.

[6] Ehrman, Bart D. The New Testament: A Historical Introduction to the Early Christian Writings. P. 12.

[7] Ehrman, Bart D. Lost Christianities. Uk. 49.

[8] Metzger, Bruce M. A Textual Commentary on the Greek New Testament. Introduction, p. 1.

[9] Ehrman, Bart D. Lost Christianities and Misquoting Jesus.

[10] Metzger, Bruce M. and Ehrman, Bart D. The Text of the New Testament: Its Transmission, Corruption, and Restoration. P. 275.

[11] Ehrman, Bart D. Lost Christianities. Uk. 49, 217, 219-220.

[12] Ehrman, Bart D. Lost Christianities. Uk. 219.

[13] Metzger, Bruce M. and Ehrman, Bart D. The Text of the New Testament: Its Transmission, Corruption, and Restoration. P. 265. See also Ehrman, Orthodox Corruption of Scripture.

[14] Ehrman, Bart D. 1993. The Orthodox Corruption of Scripture. Oxford University Press. P. xii.

[15] Ehrman, Bart D. Lost Christianities. Uk. 220.

[16] Metzger, Bruce M. A Textual Commentary on the Greek New Testament. Introduction, p. 3

[17] Metzger, Bruce M. A Textual Commentary on the Greek New Testament. Introduction, p. 10.

[18] Metzger, Bruce M. and Ehrman, Bart D. The Text of the New Testament: Its Transmission, Corruption, and Restoration. P. 343.

[19] Ehrman, Bart D. Misquoting Jesus. Uk. 62-69.

[20] Ehrman, Bart D. Misquoting Jesus. Uk. 68.

[21] Ehrman, Bart D. Lost Christianities. Uk. 9-11, 30, 235-6.

[22] Ehrman, Bart D. Lost Christianities. Uk. 235.

[23] Ehrman, Bart D. Lost Christianities. Uk. 3, 235. Also, see Ehrman, Bart D. The New Testament: A Historical Introduction to the Early Christian Writings. P. 49.

[24] Ehrman, Bart D. Lost Christianities. Uk. 235.

[25] Stanton, Graham N. Uk. 19.

[26] Kee, Howard Clark (Vidokezo na Marejeleo). 1993. The Cambridge Annotated Study Bible, New Revised Standard Version. Cambridge University Press. Introduction to gospel of ‘John.’

[27] Butler, Trent C. (General Editor). Holman Bible Dictionary. Nashville: Holman Bible Publishers. Under ‘John, the Gospel of’

[28] Easton, M. G., M.A., D.D. Easton’s Bible Dictionary. Nashville: Thomas Nelson Publishers. Under ‘John the Apostle.’

[29] Goodspeed, Edgar J. 1946. How to Read the Bible. The John C. Winston Company. uk. 227.

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.