Ukanaji Mungu (Sehemu 1 kati ya 2): Kukataa Kisichokatalika
Maelezo: Ingawa mtu anaweza kukataa kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, lakini ndani ya moyo wake, ni ukweli ambao hawezi kuukanusha.
- Na Laurence B. Brown, MD
- Iliyochapishwa mnamo 29 Nov 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 31 Jan 2024
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 4,361 (wastani wa kila siku: 4)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
“Janga kubwa la maisha ni kumpoteza Mungu na kutotamani kurudi kwake.”
--F.W. Norwood
Wakanaji Mungu wanaweza kudai kwamba hawakubali kuwepo kwa Mungu, lakini mtazamo wa baadhi ya Wakristo na Waislamu wote ni kwamba kwa kiwango fulani hata yule mkanaji sugu anakubali uwepo wa Mungu. Ufahamu wa ndani uliopuuzwa wa uwepo wa Mungu kawaida hujitokeza tu katika akili za Wakanaji kwenye nyakati za dhiki nyingi, na mfano bora ni dondoo hili la Vita vya Pili vya Dunia “Hakuna Wakanaji Mungu kwenye mashimo ya vita.”[1]
Bila shaka kuna nyakati - iwe siku za uchungu wa ugonjwa usioisha, au nyakati za udhalilishaji usioisha, au sekunde chache kabla ya ajali ya gari - ambapo wanadamu wote wanatambua ukweli wa udhaifu wa mwanadamu na kuwa hana udhibiti juu ya hatima na majaliwa. Mtu humwomba nani msaada katika hali kama hizo isipokuwa Muumba? Nyakati hizo za kukatatisha tamaa zinapaswa kumkumbusha kila mtu, awe ni msomi wa dini au Mkanaji sugu, kuhusu utegemezi wa wanadamu kwa Kitu kikubwa zaidi kuliko maisha yetu wenyewe ndogo. Kitu kikubwa zaidi kwa ujuzi, nguvu, dhati, adhama na utukufu.
Katika nyakati hizo za dhiki, wakati jitihada zote za binadamu zimeambulia patupu na hakuna kitu kingine duniani kinaweza kuwa na uwezo wa kuleta faraja, Nani mwingine wa kuombwa? Katika nyakati hizo za majaribio, ni dua ngapi, zinazosababishwa na matatizo, zinaombwa kwa Mungu, zikiwa na ahadi za kuwa wanyenyekevu baada ya hapo? Hata hivyo, ni ahadi zipi chache hutimizwa?
Bila shaka siku ya dhiki kubwa kabisa itakuwa Siku ya Kiyama. Na mtu atakuwa ni mwenye bahati mbaya iwapo atamwamini Mungu kwa mara ya kwanza kwa siku hiyo. Mshairi wa Kiingereza, Elizabeth Barrett Browning, alikejeli kilio cha mwanadamu akiwa kwenye masaibu katika kilio cha Binadamu:
“Na midomo inasema “Mungu nionee huruma,”
Na ni nani ambaye hayajawahi kusema, “Mwenyezi Mungu atukuzwe”
Anayemkana Mwenyezi Mungu mwenye tafakuri zake, akiwa na shaka kubwa lakini anaogopa uwezekano wa kuwepo kwa Mungu na Siku ya Hukumu, anaweza kukubali 'dua ya wasio na hakika, 'kama ifuatavyo:
“Ewe Mola--ikiwa kuna Mola,
Okoa roho yangu--ikiwa nina roho.”[2]
Mbele ya shaka inayozuia imani, mtu anawezaje kupotea akiwa na dua iliyopo hapo juu? Ikiwa wakanaji watabaki kwa ukufuru wao, hawatakuwa wamepoteza chochote. Ikiwa Imani itafuata dua hiyo, Thomas Jefferson anasema yafuatayo:
“Ikiwa unapata sababu ya kuamini kuwa kuna Mungu, ufahamu kwamba upo chini ya ulinzi wake, na kwamba Anakukubali, itakuwa uhimizi mkubwa zaidi; ikiwa kutakuwa na hali ya baadaye, matumaini ya kuwepo kwa furaha inayoongeza hamu ya kuistahili...”[3]
Pendekezo linaweza kufanywa kwamba ikiwa mtu haoni ushahidi wa kuwepo kwa Mungu katika ukubwa wa uumbaji wake, wangeshauriwa kutazama mara nyingine. Kama Francis Bacon anavyoeleza kwa maoni yake, “Afadhali niamini hurafa zote za kale , na Talmud, na alkoran (yaani Kurani), kuliko kuamini kwamba ulimwengu huu hauna muumba.” [4] Aliendelea kutoa maoni, “Mungu hakuleta miujiza kuwashawishi Wakanaji Mungu, kwa sababu kazi zake za kawaida zina ushawishi wa kutosha.” [5] Jambo linalostahili kufikiriwa ni kwamba hata viumbe vidogo kabisa vya Mungu, ingawa uumbaji wake ni wa kawaida kwake, ni miujiza kwetu. Chukua mfano wa mnyama mdogo kama buibui. Je, kuna mtu yeyote anayeamini kwamba kiumbe hicho cha ajabu kilitokana na supu ya asili (Primordial soup)? Mmoja tu kati ya viumbe hivi vya miujiza anaweza kuzalisha hadi aina saba tofauti za hariri, ambapo baadhi ni nyembamba kama lukoka ya mwanga unaoonekana, lakini imara kuliko chuma. Hariri mbalimbali hutofautiana, kuanzia kwa zile nyumbufu nata za kutumika kwa mnaso, hadi kwa yasiyo ya wambiso na fremu ya nyuzi , pamoja na hariri za kufunikia mawindo, na kutengeneza kifuko yai, nk. Buibui anaweza pia, kulingana na mahitaji, kutengeneza hariri zozote kati ya aina hizo saba, na pia kuzifyonza tena, kuvunja na kutengeneza tena,ujirejelezaji-binafsi, kwa kutumia vipengele vya mwanzo. Na hii ni sehemu moja tu ndogo ya muujiza wa buibui.
Hata hivyo, wanadamu hujiinua kwa kiburi. Mtazamo wa kina unapaswa kuelekeza mioyo ya wanadamu kwa unyenyekevu. Akiangalia jengo mtu anafikiria mchoraji, akitazama uchongaji hufikiria msanii . Lakini kuchunguza utata wa kifahari wa maumbile, kutoka kwa utata na usawa wa fizikia ya nyuklia ya chembe hadi kwa ukubwa wa anga, na mtu hafikirii chochote? Tukizungukwa na ulimwengu wenye utata wa kihandisi, sisi kama wanadamu hatuwezi hata kutengeneza ubawa wa mbu. Na bado dunia nzima na Ulimwengu wote ambao uko katika hali ya usawa kamili ulitokana na ajali za hapa na pale tu ambazo zimepanga msukosuko wa ulimwengu na kuufanya uwe na ukamilifu na uwiano? Baadhi watasema ni ajali tu, na wengine uumbaji.
Ongeza maoni