Kuukubali Uislamu (sehemu ya 1 kati ya 2): Dini kwa watu wote, kila mahali

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Kupambana na vizuizi.

 • Na Aisha Stacey (© 2010 IslamReligion.com)
 • Iliyochapishwa mnamo 09 Dec 2021
 • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 07 Mar 2022
 • Ilichapishwa: 2
 • Imetazamwa: 4,128
 • Ukadiriaji: 2.3 kati ya 5
 • Imekadiriwa na: 75
 • Imetumwa kwa barua pepe: 0
 • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Accepting_Islam_(part_1_of_2)_001.jpgLeo, watu wengi kote ulimwenguni wanautafuta ukweli; wanatafuta maana halisi katika maisha yao, na wanastaajabia maisha yanahusu nini hasa. Wanaume kwa wanawake huuliza swali, kwa nini nipo hapa? Katikati ya mateso na maumivu, wanadamu huomba kwa sauti ndogo au kubwa faraja, au kueleweka. Mara nyingi katikati ya starehe, mtu hutafuta kuelewa chanzo cha furaha hiyo. Wakati mwingine watu hutafakari kuukubali Uislamu kuwa dini yao ya kweli lakini hupambana na vizuizi.

Katika nyakati za furaha zaidi maishani au nyakati za dhiki zaidi, kimaumbile mtu hutafuta njia za kujikurubisha kwa Kiumbe Mkuu, kwa Mwenyezi Mungu. Hata wale ambao hujichukulia kuwa wao ni wakanamungu au wasioamini walipitia hatua fulani katika maisha yao kuhisi hisia ya kimaumbile (fitra) ya kuwa sehemu ya mpango mkuu.

Dini ya Uislamu imejengwa katika imani moja kuu ya msingi, kwamba kuna Mungu Mmoja. Yeye peke yake ndiye Mlezi Mwenye Kuruzuku na Muumba wa Ulimwengu. Yeye hana washirika, watoto, au wasaidizi. Yeye ndiye Mwingi wa Rehema, Mwenye Hekima zaidi na Mwadilifu zaidi. Yeye ndiye Mwenye Kusikia kila kitu, Mwenye Kuona kila kitu, na Mjuzi wa Kila kitu. Yeye ndiye wa Kwanza, Yeye ndiye wa Mwisho.

Ni faraja kufikiria kwamba majaribu yetu, dhiki zetu, na ushindi wetu katika maisha haya sio matendo nasibu ya ulimwengu mbaya usiopangwa. Imani ya Mungu, kuamini Mungu Mmoja, Muumba, na Mlezi Mwenye Kuruzuku vyote vinavyoishi ni haki ya kimsingi. Kujua kwa hakika kuwa uwepo wetu ni sehemu ya ulimwengu uliopangwa vizuri na kwamba maisha yataendelea kama yalivyopangwa ni dhana inayoleta utulivu na amani.

Uislamu ni dini inayoutazama uhai na kukumbusha kuwa ulimwengu huu ni mahali pa kuishi kwa muda mfupi na sababu yetu ya kuumbwa ni kumuabudu Mungu. Kauli hii inakaa kueleweka kiurahisi au sio? Itafahamika hivyo iwapo utakubali kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja, na umwabudu Yeye ndipo kutapatikana amani na utulivu. Mwanadamu yeyote anaweza kuwa na ufahamu huu kwa kuamini kwa dhati kwamba hapana anayepaswa kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu.

Inasikitisha kwamba katika karne hii mpya ya ujasiri, tunaendelea kuvuka mipaka na kugundua tena ulimwengu na fahari zake zote lakini tumemsahau Muumba, na tumesahau kuwa kweli maisha yalikusudiwa kuwa rahisi. Kutafuta uhusiano wetu na Mwenyezi Mungu na kuimarisha uhusiano na Yeye ni muhimu iwapo tutaishi kwa amani na kutupulia mbali pingu zinazotufunga kutuletea maumivu, fadhaa na huzuni.

Uislamu ulifunuliwa kwa watu wote, kila mahali na kwa wakati wote. Haukupelekwa kwa wanaume tu au kwa asili fulani au kabila fulani. Ni njia kamili ya maisha kulingana na mafundisho yanayopatikana katika Kurani na mwenendo sahihi wa Mtume Muhammad. Kwa mara nyingine tena, taarifa hii iko wazi au sio? Itafahamika hivyo iwapo utaelewa mwongozo uliofunuliwa na Muumba kwa viumbe wake. Ni mpango usio na hitilafu wa kupata furaha ya milele katika maisha haya na yajayo.

Kurani na hadithi sahihi huelezea dhana ya Mwenyezi Mungu na kutoa maelezo ya kile kinachoruhusiwa na kile kilichokatazwa. Huelezea misingi ya tabia njema na maadili, na kutoa hukumu ya ibada. Husimulia hadithi kuhusu Mitume na watangulizi wetu wema, na huelezea Pepo na Jehanamu. Mwongozo huu uliteremshiwa wanadamu wote, na Mwenyezi Mungu mwenyewe anasema kwamba hataki kuwaweka wanadamu katika dhiki.

“Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu; bali anataka kukutakaseni na kutimiza Neema Yake juu yenu ili mpate kushukuru.” (Kurani 5:6)

Tunaporudi na kumuomba Mungu, Yeye husikiliza na kujibu, na papo hapo ndipo ukweli ambao ni Uislamu, imani halisi ya kumpwekesha Mungu mmoja tu, hutudhihirikia. Hii yote iko wazi, na haipaswi kutatiza, lakini cha kusikitisha, sisi, wanadamu, tuna njia ya kufanya mambo kuwa magumu. Sisi ni wakaidi hali ya kuwa Mwenyezi Mungu daima huendelea kutuachia njia wazi kwa ajili yetu.

Kukubali Uislamu kuwa dini moja ya kweli inapaswa kuwa rahisi. Hakuna Mungu mwingine isipokuwa Allah. Ni nini kinachoweza kuwa wazi kuliko taarifa hiyo? Hakuna jambo lisiloweza kueleweka, lakini wakati mwingine kwa kujaribu kufafanua upya mfumo wa imani kunaweza kuleta vitisho na hatari zenye vizuizi. Wakati mtu anakusudia kufanya Uislamu ni dini yake ya hiari aghlabu hushindwa kuukubali kwa sababu mbalimbali hata kama mioyo yao inawaambia ni ukweli.

Hivi sasa, ukweli wa Uislamu umefunikwa na kile kinachoonekana kuwa seti ya amri na kanuni ambazo zinaonekana kuwa ngumu kutimiza. Waislamu hawanywi pombe, Waislamu hawali nyama ya nguruwe, wanawake wa Kiislamu ni lazima wavae mitandio, Waislamu ni lazima wasali mara tano kila siku. Wanaume na wanawake hujikuta wakitoa nyudhuru kama hizi, "Nisingeweza kuacha kunywa", au "Ningeona ugumu kusali kila siku seuze mara tano".

Hata hivyo, ukweli wa mambo ni kwamba pindi mtu anapokubali kuwa hapana mungu ila Allah na kukuza uhusiano na Yeye, basi masharti na kanuni huwa hazina thamani. Ni njia ya polepole ya kutaka kumridhisha Mwenyezi Mungu. Kwa wengine kukubali mwongozo wa maisha ya furaha huwachukua siku, hata saa, lakini kwa wengine huweza kuwachukua wiki, miezi, au hata miaka. Safari ya kila mtu katika Uislamu ni tofauti. Kila mtu ana upekee na uhusiano wa kila mtu na Mwenyezi Mungu unakuja kupitia matukio fulani ya kipekee. Safari moja sio sahihi zaidi kuliko nyingine.

Watu wengi wanaamini kuwa madhambi yao ni makubwa sana na ya mara kwa mara ambayo Mwenyezi Mungu hawezi kuyasamehe kamwe. Wanasita kukubali kile wanachojua ni ukweli kwa sababu wanaogopa kuwa hawataweza kujidhibiti na kuacha kufanya madhambi au uhalifu. Hata hivyo, Uislamu ni dini ya msamaha na Mwenyezi Mungu anapenda kusamehe. Ingawa madhambi ya wanadamu huweza kufikia mawingu angani, Mwenyezi Mungu atasamehe na ataendelea kusamehe hadi Dakika ya Mwisho itakapotufikia.

Iwapo mtu anaamini kwa dhati kwamba hakuna mungu ila Allah, anapaswa kuukubali Uislamu bila kuchelewa. Hata kama wanaamini wataendelea kutenda dhambi, au ikiwa kuna vipengele fulani vya Uislamu hawavielewi kwa ukamilifu. Imani ya Mungu mmoja ni imani muhimu sana katika Uislamu na endapo mtu ataimarisha uhusiano na Mungu, mabadiliko yatatokea katika maisha yao; mabadiliko ambayo hawangeamini yangewezekana.

Katika makala ifuatayo tutajifunza kuwa kuna dhambi moja tu lisilosameheka na kwamba Mungu ni Mwingi wa Rehema, Mwenye Kusamehe tena na tena.

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Ongeza maoni

 • (Haitaonyeshwa kwa umma)

 • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

  Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.