Uislam ni nini? (sehemu ya 1 kati ya 4): Msingi wa Uislamu
Maelezo: Ujumbe wa Uislamu ni sawa sawa na msingi wa ujumbe uliofunuliwa na dini zote, kwakuwa zote zimetoka katika asili moja, na sababu zinazopatikana katika dini.
- Na M. Abdulsalam (© 2006 IslamReligion.com)
- Iliyochapishwa mnamo 06 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 23 Oct 2023
- Ilichapishwa: 13
- Imetazamwa: 11,734
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Miongoni mwa baraka na upendeleo ambao amewapa wanadamu ni kuwa Amewajaalia uwezo wa asili wa kutambua na kujua uwepo Wake. Aliweka ufahamu huu chini kabisa ya mioyo yao kama tabia ya asili ambayo haijabadilika tangu mwanzo wa mwanadamu alipoumbwa. Aidha, Ameiweka tabia hii ya asili na ishara ambazo ameziweka kwenye uumbaji ambazo zinathibitisha uwepo Wake. Lakini, kwakuwa haiwezekani kwa mwanadamu kuwa na maarifa ya kina juu ya Mungu isipokuwa kupitia ufunuo kutoka Kwake Yeye Mwenyewe, Mungu ametuma Wajumbe wake ili kuwafundisha watu kuhusu Muumbaji wao wanaotakiwa kumuabudu. Wajumbe hawa pia wameleta maelezo ya jinsi ya kumuabudu Mungu, sababu maelezo hayo hayawezi kujulikana isipokuwa kwa njia ya ufunuo. Misingi hii miwili ilikuwa vitu muhimu ambavyo Wajumbe wa funuo zote za Mungu walizileta kutoka kwa Mungu. Kwa msingi huu, funuo zote za Mungu zimekuwa na malengo yale yale, ambayo ni:
1. Kuthibitisha Umoja wa Mungu - Muumba wa kusifiwa na kutukuzwa – Katika asili Yake na sifa Zake.
2. Kuthibitisha Mungu peke yake ndiye anapaswa kuabudiwa na hakuna kuabudu kiumbe chochote sambamba na Yeye au badala Yake.
3. Kulinda maslahi ya mwanadamu na kupinga ufisadi na uovu. Hivyo, kila kitu kinacholinda imani, maisha, hoja, utajiri na kizazi ni sehemu ya maslahi ya mwanadamu huyu ambaye dini hulinda. Katika mkono mwingine, kitu chochote ambacho kinahatarisha mahitaji haya muhimu ni njia ya ufisadi ambayo dini inapinga na kukataza.
4. Kuwaalika watu kwa fadhila ya hali ya juu, maadili, na desturi safi.
Lengo la msingi la Ujumbe wa Mungu limekuwa lile lile: kuwaongoza watu kwa Mungu, kuwafanya wamjue Yeye, na kuwafanya wamuabudu Yeye. Kila Ujumbe wa Mungu umekuja kuiwekea nguvu maana hii, na maneno haya yafuatayo yalirudiwa katika ndimi za Wajumbe wote: “Muabuduni Mungu, hakuna mungu zaidi Yake.” Ujumbe huu ulifikishwa kwake mwanadamu kwa kupitia Manabii na Mitume ambayo Mungu aliwatuma Kila nchi. Wajumbe hawa wote walikuja na ujumbe ule ule, Ujumbe wa Uislamu.
Jumbe zote za Mungu zimekuja kufanya maisha ya watu katika kukubali kurudi kwa Mungu. Kwa sababu hii, zote zinachangia katika jina la “Uislamu”, au “Kumrudia” lililoletwa kutoka neno moja kama “Salam”, au “amani”, kwa Kiarabu. Uislamu, kwa maana hii, ilikuwa dini ya mitume yote, ila kwanini mmoja anaona aina tofauti tofauti za dini ya Mungu ikiwa zote zinatoka katika asili moja? Majibu yako mawili.
Sababu ya kwanza ni matokeo ya muda kupita, na kwa ukweli kwamba dini zilizopita hazikuwa katika ulinzi wa Mungu, zimepitia mabadiliko mengi na aina. Matokeo yake, tunaona msingi wa ukweli ambao uliletwa na wajumbe wote sasa unatofautiana kutoka kwa mmoja hadi mwingine, mbainisho wa wazi kabisa ni ukali wa imani ya kumuabudia Mungu na Mungu peke yake.
Sababu ya pili kwa aina hizi ni kwamba Mungu, katika Hekima yake ya milele na Mapenzi ya milele, alituma kazi zote za Kimungu kabala ya ujumbe wa mwisho wa Uislam ulioletwa na Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, kuwa katika wakati maalumu. Matokeo yake, sheria na mbinu zao ziliendana na hali mahususi za watu ambao walitumwa kuwaambia.
Mwanadamu amepitia vipindi vingi vya kuongozwa, kutokuongozwa, uadilifu, na kupotoka, kuanzia kipindi cha jamii isiyojitambua hadi jamii inayojitambua. Muongozo wa Mungu uliambatana na mwanadamu katika haya yote, mara zote kupata suluhisho sahihi na kuponya.
Hii ilikuwa kiini cha kuwepo utofauti baina ya dini mbali mbali. Kutokukubaliana huku kamwe hakuendi zaidi ya Sheria za Mungu. Kila ufunuo wa Sheria unaeleza matatizo fulani ya watu walio kusudiwa. Ila, sehemu zinazokubaliana ni kubwa na nyingi, kama vile msingi wa imani; kanuni na malengo ya Sheria za Mungu, kama vile kulinda imani, maisha, hoja, utajiri, na kizazi na kusimamia haki katika nchi. ; na baadhi ya makatazo ya kimsingi, baadhi ya haya yenye umuhimu ni ibada ya masanamu, uasherati, mauaji, wizi, na kutoa ushahidi wa uongo. Ila, pia hukubaliana katika maadili mema kama ukweli, haki, sadaka, ukarimu, usafi wa roho, wema, na rehema. Kanuni hizi na zingine ni za kudumu na zinaishi; ndio kiini cha Jumbe zote za Mungu na zinaunganisha zote pamoja.
Uislam ni nini? (sehemu ya 2 kati ya 4): Asili ya Uislamu
Maelezo: Jukumu la Uislamu katika didi zingine za ulimwenguni, Hususani katika uhusiano na Mila ya Ukristo wa Kiyahudi.
- Na M. Abdulsalam (© 2006 IslamReligion.com)
- Iliyochapishwa mnamo 06 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 12
- Imetazamwa: 8,275
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Ila wapi ujumbe wa Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, unakaa kwenye jumbe zilizofunuliwa mwanzo na Mungu? Historia fupi ya mitume itaonyesha hili.
Mwanadamu wa kwanza, Adamu, aliufuata Uislamu, katika hilo alielekezwa kumuabudia Mungu peke yake na siyo mwingine na kutii amri zake. Ila baada ya muda kupita na kutawanyika kwa watu duniani kote, watu walitoka katika ujumbe huu na kuanza kuwaabudia wengine badala ya au pamoja na Yeye. Baadhi waliamua kuwaabudia wachamungu waliokufa katika wao, na wengine waliamua kuabudia roho na nguvu za asili. Hapo ndipo Mungu alipoanza kutuma wajumbe kwa wanadamu ili kuwarudisha katika kumuabudu Mungu Pekee, kulingana na asili yao, na kuwaonya na matokeo mabaya ya kuwaabudia wengine badala ya Yeye.
Miongoni mwa Wajumbe wa awali hawa alikuwa Nuhu, ambaye alitumwa kuhubiri ujumbe huu wa Uislamu kwa watu wake, baada ya kuwaabudia wachamungu wa wazee wao na Mungu. Nuhu aliwaita watu wake kuacha kuabudia masanamu, na kuwaamuru kurudi kumwabudia Mungu Pekee. Baadhi walifuata mafundisho ya Nuhu, wakati wengine wengi hawakumuamini. Wale waliomfuata Nuhu walikuwa wafuasi wa Uislamu, au Waislamu, na wale ambao hawakufuata, walibaki kwenye kutokuamini na walipotezwa kwa adhabu kwa kufanya hivyo.
Baada ya Nuhu, Mungu alituma wajumbe katika kila Nchi ambao walipotea kutoka kwenye ukweli, ili kuwarudisha. Ukweli huu ulikuwa katika muda wote: kukataa vitu vyote vya kuabudu na kumuabudia bila shaka Mungu na siyo yoyote, Muumbaji na Mola wa wote, na kutii sheria Zake. Ila kama tulivyosema kabla, sababu kila nchi ipo tofauti na jinsi wanavyoishi, lugha, na tamaduni, wajumbe mahususi walitumwa katika nchi mahususi katika kipindi cha wakati mahususi.
Mungu ametuma wajumbe katika mataifa yote, na katika utawala wa Babiloni alimtuma Ibrahimu – mmoja wa mitume ya mwanzo na wakubwa – ambaye aliwaita watu wake kukataa kuwaabudia masanamu ambayo walijitoa kwao. Aliwaita kwenye Uislamu, ila wakamkataa na hata wakataka kumuua. Mungu alimjaribu Ibrahimu kwa majaribu mengi, na akaishinda yote. Kwa kafara zake nyingi, Mungu akatangaza kuinua taifa kubwa katika kizazi chake na kutoa manabii. Kila mara watu kutoka katika kizazi chake walipoanza kupotea kutoka kwenye Ukweli, ambao ulikuwa kumuabudia Mungu peke yake na kufuata sheria zake, Mungu aliwatumia mjumbe mwingine kuwarudisha kwenye njia.
Hivyo, tunaona wajumbe wengi walitumwa katika kizazi cha Ibrahim, kama vile watoto wake wawili Iskhaka na Ismaili, pamoja na Yakobo (Israeli), Yusufu, Daudi, Sulemani, Musa, na bila shaka, Yesu, kwa kutaja wachache, amani na baraka za Mungu ziwe juu yao. Kila mtume alitumwa kwa wama wa Israeli (Wayahudi) walipotoka katika dini ya Mungu, na walikuwa na jukumu la kufuata ujumbe ambao uliletwa kwao na kutii sheria zake. Wajumbe wote walikuja na ujumbe sawa sawa, kukataa kuabudu viumbe vyote ila Mungu pekee na kutii Sheria Zake. Baadhi walikuwa hawawamini mitume, wakati wengine waliwaamini. Wale walio waamini walikuwa wafuasi wa Uislamu, au Waislamu.
Miongoni mwa wajumbe alikuwa Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, kutoka katika kizazi cha Ismaili, mtoto wa Ibrahim, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, ambaye alituma mjumbe katika mfululizo na Yesu. Muhammad alihubiri ujumbe ule ule wa Uislamu kama mitume na wajumbe – Kupeleka ibada zote kwa Mungu na siyo mwingine na kutii sheria Zake – ambapo wafuasi wa mitume iliyopita walipotea.
Hivyo kama tulivyoona, Mtume Muhammad hakuwa muanzilishi wa dini mpya, kama watu wengi wanavyokosea kufikiria, ila alitumwa kama Mtume wa mwisho wa Islam. kwa ufunuo wa mwisho kwa Muhammad, ambao ni wa milele na, wa kilimwengu kwa wanadamu, Hatimae Mungu alitimiza agano lake aliloliweka kwa Ibrahim.
Kama ilivyokuwa juu ya wale walio hai kufuata ujumbe wa mwisho wa Mitume uliotumwa kwao, Imekuwa wajibu kwa wanadamu wote kuufuata ujumbe wa Muhammad. Mungu ameahidi kuwa ujumbe huu utabaki bila kubadilika na kuweza kukidhi kwa muda wote na sehemu yoyote. Inatosha kusema Uislamu ni njia ile ile ya Ibrahim, kwa sababu vyote Biblia na Kurani vinamwelezea Ibrahimu kuwa mfano mzuri kama mtu aliyejisalimisha kikamilifu kwa Mungu na kumuabudia Mungu pekee na sio mwingine, bila waombezi wengine. Hili likieleweka, itajulikana kuwa Uislamu una ujumbe unaoendelea na, wa kilimwengu ukilinganisha na dini nyingine, kwa sababu mitume yote na wajumbe walikuwa “Waislamu”, mf. wale wanaojisalimisha kwa mapenzi ya Mungu, na walihubiri“Uislamu”, mf. kujisalimisha katika mapenzi ya Mungu mtukufu kwa kumuabudu Yeye Peke na kutii Sheria zake.
Hivyo tumeona wale wanao jiita Waislamu leo hawafuati dini mpya; bali wanafuata dini na ujumbe wa manabii na wajumbe ambao ulitumwa kwa wanadamu kwa amri ya Mungu, pia inajulikana kama Uislamu. Neno “Islam” ni neno la Kiarabu ambalo linamaana ya “kujisalimisha kwa Mungu”, na Waislamu ni wale kwa ridhaa zao hujisalimisha na, kwa bidii humtii mungu, huishi kulingana na ujumbe Wake.
Uislam ni nini? (sehemu ya 3 kati ya 4): Imani Muhimu ya Uislamu
Maelezo: Mtazamo wa baadhi ya imani ya Uislamu.
- Na IslamReligion.com
- Iliyochapishwa mnamo 06 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 12
- Imetazamwa: 8,534
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Kuna mambo mengi ya imani ambayo mtu anayeshikamana na Uislamu lazima awe na usadikisho thabiti. Kutoka katika mambo hayo, muhimu zaidi ni sita, yanayojulikana kama "Nguzo Sita za Imani".
1) Kumwamini Mungu
Uislamu unashikilia imani kuu ya Mungu mmoja na imani katika Mungu huunda moyo wa imani hiyo. Uislamu unafundisha imani ya Mungu mmoja ambaye hazai wala hakuzaliwa, na hana mshirika katika utunzaji Wake wa ulimwengu. Yeye peke yake ndiye huleta uhai, anasababisha kifo, huleta mema, husababisha shida, na hutoa riziki kwa uumbaji Wake. Mungu katika Uislamu ndiye Muumba pekee, Mola, Mlezi, Mtawala, Jaji, na Mwokozi wa ulimwengu. Hana usawa katika sifa na uwezo Wake, kama maarifa na nguvu. Ibada zote, kutii na heshima zinapaswa kuelekezwa kwa Mungu na sio mwingine. Ukiukaji wowote wa dhana hizi unakiuka msingi wa Uislamu.
2) Kuwaamini Malaika
Wanaoshikamana na Uislamu lazima waamini ulimwengu usioonekana kama ilivyoelezwa katika Kurani. Kwenye ulimwengu huu ni malaika wajumbe wa Mungu, kila mmoja amepewa jukumu maalum. Hawana hiari au uwezo wa kutotii; ni asili yao kuwa watumishi waaminifu wa Mungu. Malaika hawapaswi kuchukuliwa kama miungu au vitu vya kusifiwa au kuabudiwa; wao ni watumishi wa Mungu tu wanaotii kila amri Yake.
3) Kuwamini Mitume na Wajumbe
Uislamu ni dini ya kilimwengu. Waislamu wanaamini katika manabii, sio tu Nabii Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, lakini manabii wa Kihebrew, ikiwemo Ibrahim na Musa, na pia manabii wa Agano Jipya, Yesu, na Yohana Mbatizaji. Uislamu unafundisha Mungu hakutuma manabii kwa Wayahudi na Wakristo peke yao, bali alituma manabii kwa mataifa yote ulimwenguni na ujumbe mmoja wa msingi: kumwabudu Mungu peke yake. Waislamu lazima waamini manabii wote waliotumwa na Mungu waliotajwa katika Kurani, bila kufanya tofauti yoyote kati yao. Muhammad alitumwa na ujumbe wa mwisho, na hakuna nabii anayekuja baada yake. Ujumbe wake ni wa mwisho na wa milele, na kupitia yeye Mungu alikamilisha Ujumbe wake kwa wanadamu.
4) Kuamini katika Maandiko ya Dini
Waislamu wanaamini katika vitabu vyote ambavyo Mungu ametuma kwa wanadamu kupitia manabii wake. Vitabu hivi ni pamoja na Vitabu vya Ibrahim, Torati ya Musa, Zaburi ya Daudi, na Injili ya Yesu Kristo Vitabu hivi vyote vimetokwa katika chanzo kimoja (Mungu), ujumbe huo huo, na vyote vilifunuliwa kwa ukweli. Hii haimaanishi kuwa umehifadhiwa katika ukweli. Waislamu (na wasomi na wanahistoria wengi wa Kiyahudi na Kikristo) wanaona kuwa vitabu vilivyopo leo sio maandiko asili, ambayo kwa kweli yamepotea, kubadilishwa, na/ au kutafsiriwa tena na tena, kupoteza ujumbe wa asili.
Wakati Wakristo wanaona Agano Jipya linatimiza na kukamilisha Agano la Kale, Waislamu wanaamini kwamba Nabii Muhammad alipokea mafunuo kutoka kwa Mungu kupitia malaika Gabrieli ili kurekebisha makosa ya kibinadamu ambayo yalikuwa yameingia katika maandiko na mafundisho ya Uyahudi, Ukristo na dini zingine zote. Ufunuo huu ni Kurani, iliyofunuliwa kwa lugha ya Kiarabu, na inapatikana leo katika hali yake ya asili. Inawapeleka wanadamu katika nyanja zote za maisha; kiroho, kidunia, kibinafsi na kwa pamoja. Inatoa mwelekeo wa maisha, inaelezea hadithi na mifano, inaelezea sifa za Mungu, na inazungumza juu ya sheria bora za kutawala maisha ya kijamii. Ina maelekezo kwa kila mtu, kila mahali, na ya nyakati zote. Mamilioni ya watu leo wamehifadhi Kurani, na nakala zote za Kurani zilizopatikana leo na zamani zinafanana. Mungu ameahidi kwamba atailinda Kurani kutokana na mabadiliko hadi mwisho wa nyakati, ili Mwongozo uwe wa wazi kwa wanadamu na ujumbe wa manabii wote upatikane kwa wale wanaoutafuta.
5) Kuamini Maisha baada ya Kifo
Waislamu wanaamini kuwa siku itakuja ambapo viumbe vyote vitaondoka na kufufuliwa ili kuhukumiwa kwa matendo yao: Siku ya Hukumu. Siku hii, wote watakusanyika mbele za Mungu na kila mtu ataulizwa juu ya maisha yake ulimwenguni na jinsi alivyoishi. Wale ambao walikuwa na imani sahihi juu ya Mungu na maisha, na kufuata imani yao na matendo mema wataingia Peponi, ingawa wanaweza kulipia baadhi ya dhambi zao katika Jehanamu ikiwa Mungu kutokana na Haki Yake isiyo na kipimo atachagua kutowasamehe. Ama wale walioanguka katika ushirikina katika sura zao nyingi, wataingia Motoni bila kuacha milele.
6) Kuamini katika Nguvu ya Mungu
Uislamu unasisitiza kwamba Mungu ana nguvu kamili na ujuzi wa vitu vyote, na kuwa hakuna kinachotokea isipokuwa kwa mapenzi Yake na kwa ufahamu Wake kamili. Kile kinachojulikana kama amri ya Mungu, hatma, au "kusudio" inajulikana kwa Kiarabu kama al-Qadr. Hatima ya kila kiumbe tayari inajulikana na Mungu.
Hata hivyo imani hii haipingani na wazo la hiari ya mwanadamu kuchagua njia yake ya kutenda. Mungu hatulazimishi kufanya chochote; tunaweza kuchagua kumtii au kutomtii. Chaguo letu linajulikana kwa Mungu kabla hata hatujafanya. Hatujui hatma yetu ni nini; lakini Mungu anajua hatma ya vitu vyote.
Hivyo, tunapaswa kuwa na imani thabiti kuwa chochote kinachotupata, ni kulingana na mapenzi ya Mungu na kwa ufahamu Wake kamili. Kunaweza kuwa na mambo yanayotokea katika ulimwengu huu ambayo hatuelewi, lakini tunapaswa kuamini kwamba Mungu ana hekima katika vitu vyote.
Uislamu ni nini? (sehemu ya 4 kati ya 4): Ibada ya Uislamu
Maelezo: Kutazama baadhi ya vitendo muhimu vya Uislam, na maelezo mafupi ya Waislamu ni akina nani.
- Na IslamReligion.com
- Iliyochapishwa mnamo 06 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 12
- Imetazamwa: 8,218
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Kuna mazingatio matano rahisi ila muhimu ambayo Waislamu wanayakubali na kuyafata. Hizi ni “Nguzo za Uislamu” zinazowakilisha misingi ambayo inawaunganisha Waislamu wote.
1) ‘Tamko la Imani’
Muislamu ni yule anayetoa ushuhuda kwamba “hakuna anayestahili kuabudiwa ila Allah, na Muhammad ni mjumbe wa Allah.” Tamko hili linajulikana kama “shahada” (ushahidi, ushuhuda). Allah ni neno la Kiarabu la Mungu, kama vile Yahweh kwa Kiebrania jina la Mungu. Kwa kutamka neno hili rahisi mtu anakuwa Muislamu. Tamko linathibitisha Uislamu katika umoja wa Mungu, Haki yake ya kuabudiwa, na fundisho linalohusu kuhusisha kitu chochote na Mungu ni moja ya dhambi isiyo sameheka kama tulivyosoma kwenye Koran:
“ Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa. ” (Kurani 4:48)
Sehemu ya pili ya ushuhuda wa imani inaeleza kuwa Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, ni mtume wa Mungu kama Ibrahim, Musa na Yesu kabla yake. Muhammad ameleta ufunuo wa mwisho. Kwa kumuamini Muhammad kama “muhuri wa manabii,” Waislamu wanaamini kuwa utabili wake unathibitisha na kukamilisha ufunuo wa jumbe zote, kuanzia Adam. Cha nyongeza, Muhammad hutumika kama mfano katika maisha yake ya mfano. Jitihada za walioamini kufuata mfano wa Muhammad unaakisi mkazo wa Uislamu katika vitendo na matendo.
2) Kuswali (Salah)
Waislamu wanaswali mara tano kwa siku: alfajiri, mchana, alasili, jioni, na usiku. Inafanya Walio amini kumkumbuka Mungu katika mfadhaiko wa kazi na familia. Inauelekeza umakini wa kiroho, inaimarisha tegemeo kamili la Mungu, na huweka wasiwasi wa kilimwengu katika mtazamo wa hukumu ya mwisho na maisha ya baadaye. Sala hizo zinajumuisha kusimama, kuinama, kupiga magoti, kuweka paji la uso chini, na kukaa. Ibada ni njia ambayo inaweka mahusiano kati ya Mungu na uumbaji wake ili uweze kudumishwa. Inajumuisha kusoma Kurani, sifa za Mungu, maombi ya msamaha na dua zingine mbali mbali. Maombi ni kuonyesha kujisalimisha, unyenyekevu, na kumuabudu Mungu. Maombi yanaweza kufanywa katika sehemu yoyote iliyo safi, pekee au kwa pamoja, msikitini au nyumbani, kazini au barabarani, ndani ya nyumba au nje. Inapendeza kuswali na watu wengine kama mwili mmoja ulioungana katika ibada ya Mungu, kuonyesha nidhamu, udugu, usawa, na mshikamano. Wanaposali, Waislamu wanaangalia Makka, jiji takatifu lililoizunguka Kaaba - nyumba ya Mungu iliyojengwa na Ibrahim na mwanawe Ismaili.
3) Sadaka ya Lazima (Zakah)
Kwenye Uislamu, mmiliki wa kweli ni Mungu, siyo mwanadamu. Watu wanapewa utajiri kama amana kutoka kwa Mungu. Zakah ni ibada na zawadi kwa Mungu kwa kuwasaidia masikini, na kwa hilo mtu anasafishwa. inahitajika mchango wa kila mwaka wa asilimia 2.5 ya utajiri wa mtu binafsi na mali. Kwa hiyo, Zakah siyo “Msaada”, ni wajibu kwa wale ambao wamepata utajiri kutoka kwa Mungu kukidhi mahitaji ya wanajamii wasio na baraka hiyo. Zakah inatumika kuwasaidia masikini na wanaohitaji, msaada wale wenye deni, na, kipindi cha zamani, kuwaachia watumwa.
4) Kufunga Ramadan (Sawm)
Ramadhani ni mwezi wa tisa wa kalenda ya mwezi wa Kiislamu ambayo hutumika katika kufunga. Waislamu wenye afya hujinyima chakula, vinywaji, na tendo la ndoa alfajiri hadi machweo. Kufunga kunaongeza imani, kumtegemea Mungu, na kuleta utambulisho kwa wale wasio na bahati. Sala maalumu ya usiku pia ufanyika msikitini ambapo usomaji wa Kurani unasikika. Familia zinaamka kabla ya asubuhi kupata chakula cha kwanza cha siku ili kuweza kuhimili hadi jioni. Mwezi wa Ramadhani unaisha kwa sherehe kuu mbili za Kiislamu, Siku kuu ya Kuvunja Saumu, inaitwa Eid al-Fitr, ambayo inapambwa kwa furaha, familia kutembeleana, na kubadilishana zawadi.
5) Nguzo ya tano ni Hajj kwenda Makka
Angalau mara moja katika maisha, Muislamu mtu mzima ambaye anauwezo wa kiakili na kipesa anahitajika kuutoa kafara muda, mali, cheo, na maisha mazuri ya kila siku kufanya safari ya Hajj, kujiweka katika huduma ya Mungu. Kila mwaka zaidi ya walio amini milioni mbili kutoka tamaduni mbali mbali na lugha husafiri kutoka ulimwenguni kote kwenda katika mji mtakatifu wa Makka[1] Kuitikia wito wa Mungu.
Waislamu ni Akina nani?
Neno la Kiarabu la “Muislamu” linamaanisha “mtu ambaye yupo kwenye hali ya Uislamu (kujisalimisha katika mapenzi na sheria ya Mungu)”. Ujumbe wa Uislamu ulikusudiwa kwa walimwengu wote, na mtu yoyote atakaye ukubali ujumbe huu atakuwa Muislamu. Kuna Waislamu zaidi ya bilioni duniani. Waislamu wanawakilisha idadi kubwa ya watu katika nchi hamsini na sita. Watu wengi wanashangaa kujua kuwa Waislamu wengi siyo Waarabu. Japokuwa Waarabu wengi ni Waislamu, kuna Waarabu ambao ni Wakristo, Wayahudi na Wasiokuwa na dini. Asilimia 20 tu ya Waislamu bilioni 1.2 duniani wanatoka nchi za Kiarabu. Kuna idadi kubwa ya Waislamu kutoka India, Uchina, Jamuhuri ya Asia ya kati, Urusi, Ulaya, na Marekani. Iwapo mtu ataangalia watu mablimbali wanoishi Ulimwengu waUislamu - kuanzia Nigeria hadi Bosnia na kuanzia Morocco hadi Indonesia - ni rahisi kuona kuwa Waislamu wanatoka katika asili, makabila, tamaduni na mataifa tofauti tofauti. Uislamu mara zote umekuwa ujumbe wa ulimwengu kwa watu wote. Uislamu ni dini kubwa ya pili katika ulimwengu na karibuni itakuwa dini ya pili kwa ukubwa ndani ya Marekani. Huku ni , watu wachache wanajua Uislamu ni nini.
Ongeza maoni