Eric Schrody, MKatoliki wa Zamani, Marekani (sehemu ya 1 kati ya 2)

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Mazungumzo na mwimbaji wa zamani wa rapu, nyota EverLast na safari yake kuelekea Uislamu. Sehemu ya 1.

  • Na Adisa Banjoko (interviewer)
  • Iliyochapishwa mnamo 14 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 2,973 (wastani wa kila siku: 3)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Muziki wa Rapu umepata hadhi mkubwa kwa kiasi fulani kutokana na dini ya Uislamu. Makundi kama vile Public Enemy yalitoa muziki kuhusu heshima yao kwa kundi la Taifa la Islam, huku watu kama vile Q-Tip wa kundi linaloitwa Quest wakiingia katika Uislamu, dini hii inaonekana kuwa maudhui ya kurejea rejea katika muziki wa Rapu, ikiathiri mistari na maisha pia. Msanii mmoja ambaye hivi karibuni aliathirika na Uislamu ni Eric Schrody, anayefahamika zaidi katika dunia ya muziki kama Everlast.

Ingawa Everlast alianza kazi yake ya muziki kama msanii wa rapu, hivi karibuni amejionyesha kuwa na kina zaidi na utofauti. Albamu yake ya sasa, Whitey Ford Sings the Blues (kwa sasa imeshika nafasi ya #49 kwenye chati za Billboard baada ya kushika nafasi ya #9) inaonyesha hili kwa sauti yake ya kutafakari na kwa kiasi fulani ya kifalsafa, ikionyesha athari Uislamu umekuwa nayo katika maisha yake.

Kinachofuata ni mahojiano ambapo Everlast anaeleza safari yake kwa Uislamu na changamoto anazozikabili kama Mwislamu.

AB: Niambie mara ya kwanza ulipojifunza kuhusu Uislamu?

E: Ilikuwa labda karibu na mwishoni mwa miaka ya 1980. Nilikuwa naketi na Divine Styler (msanii maarufu wa rapu wa Los Angeles). Alikuwa mwishoni mwa kipindi chake cha 5% (akimaanisha dhehebu la bandia la “Taifa la Miungu na Dunia” kundi). Alikuwa akianza kuingia katika Uislamu. Aliishi na familia ya Bashir. Abdullah Bashir alikuwa kwa kiwango fulani mwalimu wake; na baadaye akawa wangu pia. Alipokuwa akifanya mpito kutoka 5% kuingia Uislamu, ningekuwa karibu naye na hivyo kujua mambo mengi.

Ninajaribu kufikiria mara ya kwanza nilipoitambua kama Uislamu. Nadhani ilikuwa wakati mmoja wa marafiki wa Divine alipochukua Shahadah (ushuhuda wa Kiislamu wa imani) na nilikuwa huko. Nikamsikia akisema: “Nashuhudia ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na Muhammad ni mtumwa na Mtume.“ Na ninakumbuka nikiwaza, “Hii ni nini? Mimi ni mzungu. Naruhusiwa kuwa hapa kweli?” Ilikuwa ni kutokana na ujahili, kwa sababu hapa Marekani, Uislamu unachukuliwa kuwa “kitu cha watu weusi.” Na hapo ndipo mtu aliniambia, “Huwezi amini kuna Waislamu wangapi weupe duniani.” Nilisema , “Kwa uhakika?” na mtu akanieleza. Nikasema, “Hilo ni jambo kubwa. Sikujua.“

AB: Je, unahisi shinikizo lolote la ziada kwa kuwa Muislamu mweupe nchini Marekani?

E: Siifikirii kwa kiwango kikubwa. Kwangu mimi, Uislamu ni wangu. Mwenyezi Mungu ni Mungu wa walimwengu wote, na wanadamu wote, na Aalameen (walimwengu wote). Uislamu ni uhusiano wangu binafsi na Mungu. Kwa hivyo hakuna yeyote anayeweza kunishinikiza zaidi kuliko ninavyoweza kujishinikiza. Lakini kulingana na msikiti ambapo ninaswali, sijawahi kuhisi nipo nyumbani kwingine kama ninavyohisi nikiwa huko. Na siyo wangu tu. Misikiti michache ambayo nimeenda kote nchini, sijawahi kufanywa kusikia wasiwasi. Kama huko New York, msikiti ni mkubwa na kuna watu wengi sana hadi kwamba hakuna mtu anayekutazama au kukutambua. Kulikuwa na Wachina, Wakorea, Wahisapania- kila mtu, na hilo ni jambo zuri kwangu kwa sababu katika msikiti wangu mimi ndiye kiume pekee mweupe, [ingawa] kuna wanawake wazungu.

Nadhani kwa mara ya kwanza, nilifikiria kuhusu hilo zaidi ya kila mtu mwingine nilipokwenda Jumma (sala ya mkutano wa Ijumaa). Mara yangu ya kwanza kwenda Jumma, nilichukuliwa na rafiki yangu huko New York. Ilikuwa katika Brooklyn katika Bed-Stuy (Bedford Stuyvestant). Nilikuwa na wasiwasi kuhusu mtaa niliokuwa, si msikiti. Lakini niliishiwa na wasiwasi wote pindi nilipofika huko. Niliwaza, “Haya ni mazuri.” Sikuhisi utofauti wowote kuliko mtu mwingine yeyote katika msikiti.

AB: Familia yako ilichukulia aje Uislamu wako? Kwa sababu ulilelewa kikatoliki, sivyo?

E: Kusema kweli, unajua mama yangu ni mtu mwenye nia safi sana, mwenye ujuzi mwingi. Mama yangu anaishi nami. Na nimelelewa maishani mwangu wote bila kuamini kwa Mungu, bali elimu tu ya kwamba yupo. Nilifundishwa kwamba kama [ningejua] chochote ulimwenguni, ningejua ya kuwa Mungu yupo. Na mama yangu, ingawa alikuwa Mkatoliki, alikuwa mtu wa kwanza kuelezea unafiki katika kanisa. Mama yangu kwa kweli hajahudhuria kanisa kwa muda mrefu. Lakini kuhusiana na mimi, mama yangu anafurahi kwamba nina Mungu katika maisha yangu.

Ananiona nikiswali. Na Kasisi ni mmoja wa watu anaowapenda sana duniani. Anajua jinsi tulivyobadilika sana kwa sababu alitujua tangu utotoni. Mimi na Kasisi tulipopatana mara ya kwanza, tulikuwa vichaa. Tulikuwa tukipoteza wakati kwa masherehe, vita, na kufanya chochote tulichohitaji kufanya. Tuliwaza, “Naam, hivi ndivyo mwanaume anafaa kuwa. Tutakwenda nje tuwe wahuni.”

[Lakini] ameona ni kiasi gani uislamu umetubadilisha mimi na yeye; na ni kiasi gani umeleta amani kwa maisha yangu tangu nianze kuyatumia vizuri. Hivi karibuni nilikuwa na majadiliano marefu na mama yangu na tulikuwa tukiongelea mada ya dini. Kwa kweli tulikuwa tunazungumzia kuhusu maisha na kifo, na wakati ujao na wakati anapoweza kwenda (kufa, kufariki). Hayo hayatakuwa karibuni, inshallah (Mwenyezi Mungu akipenda). Lakini nikamwomba anifanyie jambo moja. Nikasema, “Mama, unapokufa huenda kuna malaika watakaokuuliza swali, na nataka ujibu; na sijui hasa jinsi itakavyokwenda, kwa sababu sijafa bado. Kumbuka kwamba kuna Mungu mmoja tu, na hajawahi kuwa mwanadamu.“

Akasema, “Najua unachojaribu kuniambia.” [Na] nikasema, “Yesu hakuwa Mungu, Ma.”

Baadhi ya ninayoyajua kwa hakika yamedhihirika katika maisha ya mama yangu. Yeye si Muislamu, lakini anajua kuna Mungu mmoja tu. Na hilo hunifurahisha sana. Najua vijana wengi ambao wameingia Uislamu, na jamaa zao zimewageukia (wamewakataa).

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.