Ukanaji Mungu (Sehemu 2 kati ya 2): Suala la Ufahamu

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Kushindwa kuelewa baadhi ya kazi za Mungu sio sababu ya kupuuza kuwepo kwake.

  • Na Laurence B. Brown, MD
  • Iliyochapishwa mnamo 29 Nov 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 2,666 (wastani wa kila siku: 3)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Hoja nyingi za Wakanaji Mungu zinaongelea kuhusu uhusiano kati ya Mungu mwenye upendo na dhuluma zinazoonekana maishani. Wenye dini huona kuwa hoja kama hizi zinaonyesha kiburi kwa upande wa mwanadamu — kuwa na dhana kwamba sisi kama wanadamu, ambao sisi wenyewe ni kipengele cha uumbaji, tunajua mengi kuliko Mungu na jinsi uumbaji wake unapaswa kuendelezwa- pamoja na kushindwa kufahamu muundo mkubwa zaidi.

Ukweli kwamba wanadamu wengi wanashindwa kuelewa mambo fulani ya maisha haya haupaswi kuzuia imani kwa Mungu. Wajibu wa mwanadamu si kuhoji au kukataa sifa au uwepo wa Mungu, na si kuwa na kiburi kwa kudai kuwa na uwezo wa kufanya kazi bora zaidi, bali kukubali cheo cha binadamu katika maisha haya na kufanya vizuri iwezekanavyo na kile tulichopewa. Kwa kulinganisha, ukweli kwamba mtu hapendi jinsi bosi wake anavyofanya kazi, na anashindwa kuelewa maamuzi anayofanya, haipuuzi kuwepo kwake. Badala yake, wajibu wa kila mtu ni kutimiza malengo ya kazi yake ili kulipwa na kupewa cheo. Vilevile, kushindwa kufahamu au kuridhishwa na jinsi Mungu anavyoendeleza uumbaji wake haupuuzi kuwepo kwake. Badala yake, wanadamu wanapaswa kutambua kwa unyenyekevu kwamba, tofauti na bosi wa kazini, ambaye anaweza kukosea, Mungu ni wa ukamilifu kabisa, daima mwenye kufanya haki na kamwe hakosei. Binadamu anapaswa kuinama kwake kwa kujisalimisha nakutambua kwamba kushindwa kuelewa muundo wake kwa upande wetu hakumaanishi kuna makosa kwa upande wake. Badala yake, Yeye ni Bwana na Muumba wa Ulimwengu na sio sisi, Yeye anajua yote na sisi hatujui, Anaamuru mambo yote kulingana na sifa zake kamili, na sisi tunabaki tu viumbe vyake, tukiendelea tu kwa ajili ya safari ya maisha yetu.

Mioyo iliyochanganyikiwa na mizito inayoona ugumu katika kupatanisha kuwepo kwa Mungu na aghlabu maisha magumu yenye uchungu mwingi yanahitaji huruma na maelezo ya kina. Ikiwa mtu anakubali ukweli kwamba Mungu anajua anachofanya na sisi hatujui, anapaswa kutulia na kufahamu kwamba mambo yanaweza kuwa tofauti na yale yanayoonekana mwanzoni. Labda waovu miongoni mwa wanadamu wanastahili mateso yao maishani kwa sababu zisizojulikana na wanadamu, na pengine wanakabiliwa na mateso kwa muda mfupi tu wa kidunia ili wapokee thawabu ya milele katika maisha ya Ahera. Asije mtu akasahau, Mwenyezi Mungu aliwapatia viumbe vyake alivyovipenda (k.v. Mitume), zawadi kubwa zaidi duniani, ambayo ni uongofu na ufunuo; ila waliteseka sana kwa mujibu wa kidunia. Kwa kweli, majaribio na dhiki ya watu wengi huwa madogo kwa kulinganisha na yale ya manabii. Hivyo ingawa watu wengi wanateseka sana, ujumbe wa matumaini ni kwamba vielelezo vya Wapenzi wa Mungu, yaani manabii, walikuwa wamenyimwa raha ya dunia hii na badala yake kupewa malipo ya Akhera. Mtu anaweza kutarajia thawabu inayofanana na ya wale wanaovumilia majaribu na shida za maisha haya, huku wakisimama wima kwa imani ya kweli.

Vilevile mtu hawezi kulaumiwa kwa kutazamia madhaalimu makafiri kupata kheri zote za duniani, ila wasipate za Akhera. Baadhi ya wakazi wanaojulikana wa Jahannamu huja akilini. Farao, kwa mfano, aliishi maisha ya raha mustarehe hadi kwamba alijitangaza kuwa mungu mkuu. Kivyovyote, mtu anaweza kutarajia kuwa farao kwa sasa haridhiki akikumbuka kuwa makao yake ya raha, na kumbukumbu ya mazulia yake maridadi, na vyakula anuwai na wasichana wenye harufu nzuri, kwa sasa hawampi raha na faraja tena kutokana na joto la jahanamu .

Watu wengi wamepitia hisia za kumaliza siku nzuri kwa hali mbaya kutokana na tukio baya lililotokea mwisho wa siku hiyo. Hakuna mtu anayethamini chakula kizuri kinachomalizika kwa talaka, au kujamiana kunakoleta UKIMWI, au usiku wa raha unaoisha kwa kuibiwa kikatili au ajali mbaya ya gari . Jinsi gani ingekuwa nzuri? Vile vile, hakuna furaha katika maisha haya, bila kujali ni furaha kiasi gani au wa muda gani, ambao haufutwi hapo hapo kwa asilimia 100 kutoka kwa kumbukumbu baada ya kuchomwa mwili mzima kikamilifu. Upande mmoja wa mkono mmoja unawakilisha asilimia 1% ya jumla ya mwili wa mwanadamu, na kuchomeka jikoni kwa sehemu ya kidole ina wakilisha chini ya asilimia 0.1 ya mwili. Hata hivyo, ni nani asiyesahau kabisa kila jambo ndogo, kila jambo kubwa, kila kitu katika sekunde hiyo ya mateso na maumivu ya moto? Maumivu ya kuchomwa kwa mwili mzima, hasa kama hakuna misaada -- hakuna kuruka nyuma, hakuna kuuvuta mwili mbali -- ni zaidi ya uwezo wa mawazo ya kibinadamu. Wachache ambao wamepona baada ya kuchomeka watakubaliana. Mateso ya kuchomeka mwili mzima hauzidi tu mipaka ya mawazo ya kibinadamu, bali pia uchungu wake unapita mipaka ya kuelezwa kwa lugha yoyote. Hofu haiwezi kuelezwa kwa ukamilifu na waliokuwa na bahati mbaya ya kuipitia, wala kueleweka kikamilifu na wale wenye bahati nzuri ya kuiepuka. Hakika uchomwaji mmoja mreeeeeeefu, wa milele, wa mwili mzima katika moto inaweza kutarajiwa kufuta kumbukumbu zozote nzuri ya zamani, jambo ambalo linaafikiana na hitimisho kwamba

“…Na uhai wa dunia kwa kulingana na Akhera si kitu ila ni starehe ndogo.” (Kurani 13:26)

Kuhusiana na suala la kiambatisho cha sasa [1], mambo mawili ya kuongoza ufahamu yanastahili kuzingatiwa, ya kwanza ni kuwa ndani ya mioyo yao watu wote wana elimu ya asili ya kuwepo kwa Muumba. Binadamu wanaweza kutupilia mbali elimu na ufahamu huu katika pilkapilka za kutafuta urahisi na raha za dunia hii, lakini ndani kwa mioyo yao, wanadamu wote wanajua ukweli huu. Zaidi ya hayo, Mungu anajua kwamba tunajua hili, na Yeye peke yake ndiye anayeweza kuhesabu kiwango cha uasi wa mtu binafsi na/au ujisalimishaji wake.

Kipengele cha pili cha ufahamu wa kiroho ni kuelewa tu kwamba hakuna kitu cha bure maishani. Ni nadra sana kupata kitu bila ya kupeana kingine. Iwapo mtu anafanya kazi kwa bwana ambaye hamuelewi au ambaye hakubaliana naye, hatimaye bado anahitaji kufanya kazi yake ili alipwe. Hakuna mtu anayeenda kufanya kazi (kwa muda mrefu) na asifanye chochote zaidi ya kusema, “Ninafanya kazi,” akitarajia alipwe kwa kuhudhuria tu bila kufanya chochote. Vilevile, mwanadamu lazima atimize wajibu wa utumwa na kumuabudu Mungu ikiwa anatarajia kupokea thawabu yake. Kwani hili si lengo la maisha tu, bali ndio maelezo ya kazi na majukumu yetu. Kwa jambo hilo, Waislamu wanaamini kuwa hayo ndiyo maelezo ya kazi kwa wanadamu na majini (wingi, umoja ni 'Jinn'ee, ambayo ndio asili ya neno la Kimagharibi' genie '), kwani Mungu anaeleza katika Kurani Tukufu:

“Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.” (Kurani 51:56)

Watu wengi wanajiuliza malengo ya maisha, lakini msimamo wa waaminifu wa dini nyingi ni hasa ule uliotajwa hapo juu - wanadamu hawapo kwa sababu nyingine isipokuwa ya kumtumikia na kumwabudu Mungu. Pendekezo ni kwamba kila kipengele cha maumbile kinafanya kazi ya kuwaunga mkono au kuwajaribu wanadamu katika kutimiza wajibu huo. Tofauti na ajira ya kidunia, mtu anaweza kupuuza majukumu yake na bado akapewa kipindi cha kutosha. Hata hivyo, mwishoni mwa kipindi hiki cha majaribio kinachoitwa maisha, akaunti lazima zilipwe, na huo si wakati mzuri wa kupata akaunti ya mtu ina alama 'nyekundu. '

Francis Bacon alitoa hitimisho ya ajabu kwa mada ya kiambatisho hiki, akisema, “Wale wanaomkataa Mungu huharibu utukufu wa mwanadamu; kwa hakika mwanadamu ni wa jamaa moja na wanyama kwa mwili wake; na, kama yeye si wa jamaa moja na Mungu kwa roho yake, yeye ni kiumbe cha msingi kisicho na faida.” [2] Iwapo mtu anaamini kwamba baada ya miaka milioni kitu kinacholingana na nyama choma kitaibuka kutoka kwa povu ya Stanley Miller na Harold Urey ya supu asili, binadamu bado anafaa kueleza kile ambacho sisi wote husikia ndani ya mioyo yetu- yaani roho au nafsi. Kila mwanadamu ana moja, na huu ndio mpaka wa kimetafizikia unaomtenganisha mtu kutoka kwa wanyama.

Pia, wale ambao wana shaka kuhusu yale ambayo hayawezi kuhisika moja kwa moja wanaweza kupata udhuru ya kukataa roho, lakini watakuwa na uwezekano mkubwa wa kujikuta kuwa na elimu chache. Zaidi ya hayo, majadiliano kisha huenda kwa ya asili ya ukweli, maarifa, na ushahidi, ambayo huruka kimantiki kwa sehemu inayofuata, uagnosti.



Rejeleo la maelezo:

[1] Makala hii ni kiambatisho kwa kitabu “The First and Final Commandment” cha mwandishi huyo.

[2] Bacon, Francis. Atheism. uk. 16.

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.