Craig Robertson, Mkatoliki wa Zamani, Canada (sehemu ya 1 kati ya 2): Kutoka hali mbaya hadi mbaya zaidi

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Baada ya kulelewa katika nyumba ya Kikatoliki na kutumia sehemu kubwa ya utotoni mwake kuhudhuria kanisa, Craig anakataa imani na kujiingiza maisha ya anasa.

  • Na Craig Robertson
  • Iliyochapishwa mnamo 14 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 2,224 (wastani wa kila siku: 3)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Craig_Robertson__Ex-Catholic__Canada_(part_1_of_2)_-_From_Bad_to_Worse_001.jpgJina langu ni Abdullah Al-Kanadi. Nilizaliwa huko Vancouver, Canada. Familia yangu, ambao walikuwa Wakatoliki wa Kirumi, walinilea kama Mkatoliki wa Roma hadi nilipokuwa na umri wa miaka 12. Nimekuwa Muislamu kwa takriban miaka sita, na ningependa kushiriki nanyi hadithi ya safari yangu kuingia Uislamu.

Nadhani katika hadithi yoyote ni bora kuanzia kutoka mwanzo. Utotoni mwangu nilihudhuria shule ya kidini ya Kikatoliki na nilifundishwa kuhusu imani ya Kikatoliki, pamoja na masomo mengine. Soma la kidini lilikuwa daima somo langu bora; Nilifaulu kitaaluma katika mafundisho ya Kanisa. Nililazimishwa kuwa 'mtumishi wa madhabahu' na wazazi wangu tangu nikiwa mdogo sana, jambo ambalo liliwapendeza babu na nyanya kwa kiasi kikubwa. Lakini kadiri nilipojifunza kuhusu dini yangu, ndivyo nilivyojiuliza maswali! Nina kumbukumbu hili kutoka utotoni mwangu; nilimwuliza mama yangu katika Misa: “Je, dini yetu ni ya ukweli?” Jibu la mama yangu bado ninalikumbuka hadi leo: “Craig, zote ni sawa, zote ni nzuri!” Lakini kwangu hili halikuonekana kuwa sawa. Ni faida gani kujifunza dini yangu ikiwa zote zilikuwa sawa?

Nilipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, nyanya yangu alipata saratani ya koloni na akafa miezi michache baadaye , baada ya kupigana vita vikali na ugonjwa huo. Sijawahi kutambua jinsi kifo chake kilivyoniathiri sana mpaka baadaye katika maishani mwangu. Wakati huo, nikiwa na umri mdogo wa miaka kumi na miwili, niliamua kuwa mkanaji Mungu ili kumwadhibu Mungu (kama unaweza hata kutambua kitu kama hicho!) Nilikuwa kijana mdogo mwenye hasira; Niliukasirikia ulimwengu, nikajikasiria mimi binafsi na mbaya zaidi kuliko yote, nilimkasirikia Mungu. Nilitumia miaka yangu ya ujana nikijaribu kufanya kila kitu nilichoweza ili kuwavutia “marafiki” wangu wapya katika shule ya sekondari ya umma. Nilitambua haraka kwamba nilikuwa na mengi ya kujifunza, kwa kuwa sikufundishwa mengi katika shule ya kidini kama unavyofunzwa katika shule ya umma. Niliwashawishi marafiki zangu wote faraghani wanifundishe kuhusu mambo yote ambayo sijajifunza, punde nilipata tabia ya kuapa na kuwadharau walio dhaifu kuliniliko. Ingawa nilijaribu sana kukubaliwa na wenzangu kwa uwezo wangu wote, sikufaulu. Nilikuwa nikinyanyaswa sana na wanafunzi wenzangu, na wasichana walikua wakinikejeli. Kwa mtoto wa umri wangu, hii ilikuwa mateso. Nilijirudia mwenyewe, katika kile unachokiita 'ganda la hisia'.

Miaka yangu ya ujana yalijaa taabu na upweke. Wazazi wangu walijaribu kuzungumza nami, lakini nilikuwa na ugomvi nao na kuwakosea heshima. Nilihitimu shule ya sekondari katika majira ya joto ya 1996 na nilihisi kuwa mambo yangeweza kubadilika yawe bora, kwani niliamini hayangeweza kuwa mbaya zaidi! Nilikubaliwa katika shule ya kiufundi ya kienyeji na nikaamua kuzidisha elimu yangu na labda nipate pesa nzuri, ili nipate furaha. Nilipata kazi katika mkahawa wa chakula cha haraka iliyokuwa karibu na nyumba yangu ili kujilipia karo.

Wiki kadhaa kabla ya kuanza shule, nilialikwa kuondoka kwetu na marafiki wengine kutoka kazi. Kwangu, hii ilionekana kama jibu la matatizo yangu! Ningeweza kusahau familia yangu na kuwa na marafiki zangu wakati wote. Usiku mmoja, niliwaambia wazazi wangu kuwa ningeondoka hivi karibuni. Waliniambia Siwezi, na kwamba sikuwa tayari na kwamba hawataniruhusu! Nilikuwa na umri wa miaka 17 na nilikuwa mkaidi sana; niliwaapia wazazi wangu na kuwaambia kila aina ya maovu, jambo ambalo bado ninajuta hata leo. Nilihisi kukumbwa na uhuru wangu mpya, nilihisi kana kwamba nimetolewa jela, na ningeweza kufuata tamaa zangu kama nilivyoona sawa. Nilihamia kwa marafiki zangu na sikuzungumza na wazazi wangu kwa muda mrefu baada ya hapo.

Nilikuwa nikifanya kazi na kwenda shule wakati wenzangu nilioishi nao walinifunza kuvuta bangi. Niliipenda baada ya kuivuta maara ya kwanza! Ningeivuta baada ya kurudi nyumbani kutoka kazini ili nipumzike. Hata hivyo, nilianza kuvuta bangi zaidi na zaidi, mpaka wakati mmoja, mwishoni mwa wiki, nilikuwa nikiivuta sana, hadi jumatatu ikafika na kabla sijajua, wakati wa shule ulikuwa umefika. Nikaamua kukosa shule siku moja na kwenda siku inayofuata, kwani hawangenikosa. Sijawahi kurudi shuleni baada ya hapo. Hatimaye niligundua bahati nzuri niliokuwa nao. Chakula chote cha mgahawa nilichoweza kuiba na bangi zote ambazo ningeweza kuvuta, na bado nihitaji shule ya nini?

Nilikuwa nikiishi maisha mazuri, au hivyo ndivyo nilifikiri; nilikuwa kijana mhuni wa kazi na hivyo wasichana walianza kutanabahi, kinyume na walivyokuwa katika shule ya sekondari. Nilijaribu madawa mabaya zaidi ya kulevya, lakini alhamdulillah, niliokolewa kutokana na mambo ya kutisha. Jambo la ajabu lilikuwa, wakati sikuwa nimelewa au kunywa madawa haya nilikuwa na huzuni. Nilihisi kutokuwa na maana na asiyekuwa na thamani kabisa. Nilikuwa nikiiba kazini na kutoka kwa marafiki ili kudumisha 'moshi wa kemikali'. Nilianza kushuku watu waliokuwa karibu nami na kufikiri maafisa wa polisi walikuwa wakinifukuza kwa kila kona. Nilikuwa nimeanza kulemewa na nilihitaji suluhisho, na nikaona kuwa dini ingenisaidia.

Nakumbuka nikiona filamu kuhusu uchawi na nilifikiri kwamba hiyo ingekuwa suluhisho kamili kwangu. Nilinunua vitabu kadhaa kuhusu Wicca na Ibada ya Maumbile, na kugundua kwamba vilihimiza matumizi ya dawa za kiasili na hivyo nikaendelea. Watu wangeniuliza kama namwamini Mungu, na tungekuwa na mazungumzo ya ajabu sana huku nikiwa nimelewa, lakini ninakumbuka wazi nikisema kwamba hapana, kwa kweli simwamini Mungu kabisa, bali naamini miungu mingi isiyo kamili kama mimi.

Kupitia yote haya, kulikuwa na rafiki mmoja ambaye alikwama nami. Alikuwa ni Mkristo 'Aliyezaliwa Upya' na alikuwa akinihubiria kila wakati, ingawa ningedhihaki imani yake kila mara. Alikuwa rafiki pekee niliyekuwa naye wakati huo ambaye hakunihukumu, hivyo aliponialika kwenda kambi ya vijana mwishoni mwa wiki niliamua kwenda naye. Sikuwa na matarajio. Nilidhani ningekuwa na kicheko kikubwa nikiwadhihaki “Wabeba Biblia” wote. Siku ya pili Wakati wa jioni, walikuwa na ibada kubwa katika ukumbi. Walicheza kila aina ya muziki ambayo ilimsifu Mungu. Niliwatazama vijana na wazee, wanaume na wanawake wakipiga kelele na kuomba msamaha na kumwaga machozi. Nilisisimuka kikweli na nikasema dua kimya kama ifuatavyo “Mungu, najua nilikuwa mtu mbaya, tafadhali nisaidie, na unisamehe na uniruhusu kuanza upya.” Nilihisi kulemewa na hisia, na nilihisi machozi yakimwagika chini kwa mashavu yangu. Niliamua wakati huo kumkubali Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wangu binafsi. Niliinua mikono yangu juu na kuanza kucheza na kupiga densi (ndiyo, densi!) Wakristo wote waliokuwa karibu nami walikuwa wananiangalia kwa kimya na kushangaa; yule kijana aliyewadhihaki na kuwaambia jinsi walivyokuwa wajinga kwa kumwamini Mungu, alikuwa akicheza na kumsifu Mungu!

Nilirudi nyumbani na kutupilia mbali madawa yote, ulevi, na wasichana. Niliwaambia marafiki zangu jinsi walivyohitaji kuwa Wakristo ili waweze kuokolewa. Nilishangaa kuwa walinikataa, kwa sababu daima walinisikiliza kabla ya hapo. Hatimaye nilihamia kwa wazazi wangu baada ya kutokuwepo kwa muda mrefu na nilianza kuwaambia walipaswa kuwa wakristo. Kwa kuwa walikuwa Wakatoliki waliona kuwa tayari walikuwa Wakristo, lakini nilihisi hawakuwa, kwa kuwa waliwaabudu Watakatifu. Niliamua kuhama tena lakini wakati huu tuliwachana kwa nia nzuri na nilipewa kazi na babu yangu ambaye alitaka kunisaidia katika “kupona” kwangu.

Nilianza kuenda “nyumba ya vijana” ya Kikristo ambayo ilikuwa nyumba ambapo vijana wangeweza kwenda, ili kuondokana na shinikizo la familia na kujadili Ukristo. Nilikuwa na umri mkubwa kuliko wengi wa wavulana hao, hivyo nikawa mmoja wa wale waliozungumza zaidi na kujaribu kuwafanya wavulana wahisi wapo nyumbani. Licha ya hayo, nilihisi kama mlaghai, kwani nilianza kunywa na kuenda na wasichana tena. Ningewaambia watoto kuhusu upendo wa Yesu kwao, na wakati wa usiku ningelewa. Kupitia yote haya, rafiki wangu mmoja wa Kikristo angejaribu kunipa ushauri na kuniweka kwenye njia sahihi.

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.