Je! tuko peke yetu? (sehemu ya 3 kati ya 3): Majini yapo kati yetu lakini mbali na sisi

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Majini huishi wapi na jinsi ya kujilinda kutokana nao.

  • Na Aisha Stacey (© 2011 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 09 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 2,993 (wastani wa kila siku: 3)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Are_We_Alone_(part_3_of_3)._001.jpgHatuko peke yetu! Tamko hili linaonekana kama tangazo la sinema za uwongo za kisayansi. Inaweza kuwa hivyo, Ila sivyo. Hakika hatuko peke yetu hapa kwenye sayari hii ya dunia. Hakika sisi ni viumbe vya Mungu lakini sisi sio viumbepekee vya Mungu. Katika makala mbili yaliyopita tumejifunza mengi juu ya majini. Tuligundua kwamba waliumbwa na Mungu, kabla ya kuumba wanadamu, kutokana na moto usio na moshi. Tulibaini pia kwamba majini ni wa kiume na wa kike, wazuri na wabaya, waumini na wasiowaumini.

Majini yapo katika ulimwengu wetu lakini wamejitenga nao. Shaytaan anatokana na majini na wafuasi wake ni kutoka kwa jini na wanadamu. Sasa kwa kuwa tunaelewa kuwa hatuko peke yetu, ni muhimu kutambua ishara zinazoonyesha uwepo wa majini na kujua jinsi ya kujilinda kutokana na ufisadi na uovu wao.

“Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura. Na majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo umoto. ” (Kurani 15:26-27)

“Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi tu.” (Kurani 51:56)

Kwa sababu tunashirikiana na majini katika ulimwengu huu tunapaswa kujua makazi yao. Majini huwa wanakusanyika kwa pamoja, wakati mwingine katika idadi kubwa, kwenye magofu na maeneo yaliyotengwa. Huwa wanakusanyika katika maeneo yenye uchafu, majalala na makaburi. Majini wakati mwingine hukusanyika mahali ambapo ni rahisi kwao kusababisha ufisadi na ghasia, kama vile sokoni.

Katika mila ya Mtume Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, tunaona kuwa baadhi ya masahaba walishauri watu wasiwe wa kwanza kuingia au wa mwisho kuondoka kwenye soko kwa sababu ulikuwa uwanja wa vita wa mashetani na mafisadi.[1]

Ikiwa Shaytaan atachagua makazi ya binadamu kama mahali pake pa kukaa, tumepewa "silaha" ambazo tunaweza kuzitumia kuwafukuza kutoka kwenye nyumba. Hii ni pamoja na kusema Bismillah (naanza na jina la Mungu), kumkumbuka Mungu mara kwa mara na kusoma maneno yoyote kutoka kwenye Quran lakini haswa Sura ya pili na tatu. Jini pia hukimbia kila wanaposikia wito wa kusali.

Mtume Muhammad alielezea kwamba majini hukusanyika kwa idadi kubwa na wanazagaa pindi giza linapoingia. Alituamuru kuwaweka watoto wetu ndani wakati wa jioni kwa sababu hii.[2] Alituambia pia majini wana wanyama na chakula cha wanyama wao ni mavi ya wanyama wetu.

Wakati mwingine, wanyama ambao wanamilikiwa na wanadamu wanahusishwa na majini. Kwa mfano, majini wengi wana uwezo wa kuchukua umbo la nyoka na Mtume Muhammad aliwataja mbwa weusi kama mashetani. Alisema pia, "Msiombe katika zizi la ngamia kwa sababu mashetani hukaa humo."[3] Aliwahusisha ngamia na majini kwa sababu ya tabia yao ya fujo.

Kuna njia nyingi ambazo tunaweza kujilinda sisi wenyewe na familia zetu kutokana na uovu unaosababishwa na majini. La muhimu zaidi ni kumgeukia Mungu na kutafuta ulinzi wake; tunafanya hivi kwa kuzingatia maneno ya Quran na mafundisho ya Mtume Muhammad. Kutafuta kimbilio kwa Mungu kutatulinda na majini na mashetani. Tunapaswa kutafuta ulinzi wake tunapoingia bafuni[4], Pindi tunapokuwa na hasira[5], kabla ya tendo la ndoa[6], na mapumziko ya safari au safari za milimani[7]. Ni muhimu pia kutafuta kimbilio kwa Mungu wakati wa kusoma Quran..

“Na ukisoma Qur'ani mwombe Mwenyezi Mungu akulinde na Shetani maluuni. Hakika yeye hana madaraka juu ya walio amini na wakamtegemea Mola wao Mlezi.” (Kurani 16:98-99)

Kuelewa asili ya majini hufanya iwezekane kuelewa baadhi ya matukio ya kushangaza yanayotokea katika ulimwengu wetu wa leo. Watu huwageukia watabiri na wanajimu ili kutabiriwa mambo ya siku zinazokuja au visivyojulikana. Wanaume na wanawake kwenye runinga na mtandaoni wanadai kuzungumza na watu waliokufa na kupeleka siri na taarifa za kushangaza. Uislamu unatufundisha kuwa hili haliwezekani. Watabiri na wanajimu wanadai kuwa wanaweza kutabiri siku zinazokuja na kusoma haiba kwa uwiano wa nyota na miili mingine ya mbinguni. Uislamu unatufundisha kuwa hili pia haliwezekani.

Ila, zama za kale majini waliweza kupanda mbinguni. Wakati huo waliweza kusikia na kujua juu ya matukio kabla hayajatokea. Wakati wa Mtume Muhammad ulinzi wa mbinguni uliongezeka na umebaki hivyo. Majini hawawezi kusikia kwa muda mrefu mazungumzo ya ulimwengu wa mbinguni.

“Nasi tulizigusa mbingu, na tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvu na vimondo. Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza; lakini sasa anaye taka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia! Nasi hatujui kama wanatakiwa shari wale wanao kaa kwenye ardhi au Mola wao Mlezi anawatakia uwongofu. ” (Kurani 72:8-10)

Nabii Muhammad alielezea maana ya aya hizi. “Wakati Mungu anatoa amri kadhaa Mbinguni, malaika hupiga mabawa yao kwa kutii taarifa Yake, ambayo inasikika kama mnyororo unaoburuzwa juu ya mwamba. Wao (malaika) wanasema, ‘Je! Mola wako amesema nini? Wengine hujibu, ‘Ukweli, na Yeye ndiye Aliye juu, Mkubwa.’ (Kurani 34.23) Halafu wale wanaopata kusikilizwa kwa kuiba (yaani mashetani au majini) husimama juu ya wengine. Mwali wa moto unaweza kumshika na kumteketeza yule anayesikiliza kabla ya kufikisha habari kwa yule aliye chini yake, au inaweza isimpate mpaka atakapofikisha kwa yule aliye chini yake, ambaye kwa upande wake, huiwasilisha kwa yule aliye chini yake, na kadhalika mpaka watakapofikisha habari hiyo katika dunia.[8]

Majini wana uwezo wa kuchukua punje ya ukweli na kuichanganya na uwongo ili kuwachanganya na kuwadanganya watu. Matukio ya kushangaza japo yanasumbua na wakati mwingine yanatisha sio kitu isipokuwa ni ufisadi mbaya ulioundwa ili kuwatoa watu wawe mbali na Mungu. Wakati mwingine majini na mashetani wa kibinadamu wataungana ili kuwadanganya waumini watende dhambi ya shirki - kumshirikisha Mungu.

Muda mwingine katika ulimwengu huu wa ajabu na mzuri tunakabiliwa na majaribu na dhiki ambazo mara nyingi huonekana kutuelemea. Kukabiliana na ufisadi na nia ovu za majini inaonekana kuwa mtihani mkubwa zaidi. Ila inatia moyo kujua kwamba Mungu ndiye chanzo cha ukakamau wote na nguvu na kuwa hakuna kinachoweza kutokea bila ruhusa yake.

Nabii Muhammad alituambia kwamba maneno bora zaidi ya kutafuta ulinzi wa Mungu kutoka kwa uovu wa wanadamu na majini ni sura tatu za mwisho za Quran. Wakati mwingine tunaweza kulazimika kukabiliwa na uovu wa jini lakini Mungu ndiye kimbilio letu salama, tukimgeukia Yeye ni wokovu wetu. Hakuna ulinzi isipokuwa ulinzi wa Mungu, ni yeye tu ambaye tunamuabudu na ni kwake yeye peke yake tunayemwendea kupata msaada.



Rejeleo la maelezo:

[1]Saheeh Muslim

[2]Saheeh Al-Bukhari, Saheeh Muslim

[3]Abu Dawood.

[4] Ibid

[5]Saheeh Al-Bukhari, Saheeh Muslim

[6] Ibid

[7]Ibn Majah.

[8]Saheeh Al-Bukhari

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.