Matabiri ya Kurani

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Utimilifu wa matabiri mbalimbali katika Kurani ni ushahidi wazi kwamba umetoka kwa Mwenyezi Mungu.

  • Na Imam Mufti
  • Iliyochapishwa mnamo 23 Nov 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 17 Mar 2024
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 1,828 (wastani wa kila siku: 2)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

The_Prophecies_of_the_Quran_001.jpgKurani ina matabiri mengi ambayo yamekuja kutimia, lakini katika makala hii, tutaja matano tu.[1] Matabiri mawili ya kwanza ni muhimu sana: tofauti na maandiko mengine duniani, Qur'ani inatabiri utunzaji wake chini ya uangalizi wa Mungu, na tutaonyesha jinsi ulivyotokea.

Ulinzi wa Kurani dhidi ya Mabadiliko

kurani inafanya madai ambayo hakuna kitabu kingine cha kidini hufanya, kwamba Mungu mwenyewe atalinda maandishi yake dhidi ya mabadiliko. Mungu anasema:

"Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda ." (Kurani 15:9)

Urahisi wa Kuhifadhi Kurani Kwenye Kumbukumbu

Mwenyezi Mungu ameufanya Kurani uwe rahisi kuhifadhi :

"Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anaye kumbuka?" (Kurani 54:17)

Urahisi ambao Kurani huhifadhiwa akilini ni wa kustaajabisha. Hakuna andiko moja au maandishi ya kidini duniani ambayo ni rahisi kuhifadhi akilini kama Kurani; hata wasio Waarabu na watoto wanaiweka akilini kwa urahisi. Kurani nzima imehifadhiwa akilini na takriban kila msomi wa Kiislamu na mamilioni ya Waislamu wa kawaida, kizazi baada ya kizazi. Takriban kila Muislamu amehifadhi akilini sehemu fulani ya Kurani na kuisoma katika sala zake.

Utabiri Maradufu

Kabla ya kuinuka kwa Uislamu Warumi na Waajemi walikuwa madola mawili yaliyoshindana. Warumi waliongozwa na Heraclius (610—641 BK), Kaizari Mkristo, ilhali Waajemi walikuwa Wazoroastri wakiongozwa na Khosrow Parviz (alitawala 590—628 BK), ambapo chini yake dola ilipata upanuzi wake mkubwa zaidi.

Mwaka wa 614, Waajemi walitawala Syria na Palestina, wakichukua Yerusalemu, na kuharibu kaburi Takatifu na 'Msalaba wa Kweli' uliopelekwa mjini Stesifon. Kisha, mnamo mwaka wa 619, walichukua Misri na Libya. Heraclius alikutana nao katika Thracian Heraclea (617 au 619), lakini walitaka kumkamata, naye alirudi nyuma haraka kwa Konstantinopo, akifuatwa kwa karibu.[2]

Waislamu walihuzunishwa na kushindwa kwa Warumi kwa vile walivyojisikia kuwa wapo karibu kiroho na Roma ya Kikristo kuliko Uajemi wa Kizoroastri, lakini Wakazi kwa Makka kwa kawaida walifurahishwa na ushindi wa Uajemi. Kwa Wakazi wa Makka, udhalilishaji wa Warumi ulikuwa ni dalili ya kushindwa kwa Waislamu kwa mikono ya Waabudu-masanamu. Wakati huo utabiri wa Mungu uliwafariji waumini:

"Warumi wameshindwa,Katika nchi iliyo karibu. Nao baada ya kushindwa kwao watashinda. Katika miaka michache. Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu, humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu." (Kurani 30:2-5)

Kurani ilifanya utabiri wa ushindi mbili:

(i) Ushindi wa Warumi juu ya Waajemi ndani ya miaka kumi , jambo ambalo halikutarajiwa kamwe.

(ii) Furaha ya waumini kwa ushindi wao juu ya Waabudu-sanamu.

Matabiri haya mawili yalikuja kutimia.

Katika mwaka wa 622, Heraclius aliondoka Konstantinopo huku sala zikiongezeka kutoka kwenye patakatifu zake nyingi kwa kuomba ushindi juu ya Wazoroastri wa Kiajemi na kurudishwa kwa Yerusalemu. Alitumia miaka miwili yaliyofuata kwa kampeni huko Armenia. Mwaka wa 627, alikutana na Waajemi karibu na Ninawi. Huko, aliwaua majenerali watatu wa Kiajemi katika vita moja, akamuua kamanda wa Kiajemi, na kutawanya Jeshi lake. Mwezi mmoja baadaye, Heraclius aliingia Dastagird na hazina yake nyingi. Khosrow alipinduliwa na mwanawe, ambaye alifanya mkataba wa amani na Heraclius. Kurudi Konstantinopo akiwa na ushindi, Heraclius alisifiwa kama shujaa.[3]

Pia, katika mwaka wa 624 AH, Waislamu waliwashinda Watu wa Makka katika vita vya kwanza vilivyokuwa muhimu kabisa huko Badr.

Kwa maneno ya msomi mmoja mhindi:

"…mstari mmoja wa utabiri ulihusiana na mataifa manne na hatima ya dola mbili kubwa. Haya yote yanathibitisha kuwa Qur'ani Takatifu ni Kitabu cha Mungu."[4]

Utabiri wa Kushindwa kwa Makafiri

Kurani ilitabiri kushindwa kwa makafiri huko Makka wakati Mtume Muhammad na wafuasi wake bado walikuwa wakiteswa na makafiri hao:

"Au ndio wanasema: Sisi ni wengi tutashinda tu? Wingi wao huu utashindwa, na wao watasukumwa nyuma!" (Kurani 54:45)

Utabiri huu ulifunuliwa huko Makka, lakini ulitimizwa katika vita vya Badr, miaka miwili baada ya uhamiaji wa Mtume kwenda mji wa Madina.

Hatima ya Watu Mahususi

Waleed ibn Mugheera alikuwa adui mkubwa aliyedhihaki Qur'ani waziwazi::

"Na akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulio nukuliwa. Haya si chochote ila kauli ya binaadamu!" (Kurani 74:24-25)

Kurani ilitabiri kuwa hangewahi kukubali Uislamu:

"Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar! Na nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar?Haubakishi wala hausazi." (Kurani 74:26-28)

Waleed alifariki katika hali ya kutoamini kama ilivyotabiriwa na Kurani.

Pia, kuhusu Abu Lahab, mpinzani mkali wa Uislamu, Kurani ilitabiri kwamba angekufa akipinga dini ya Mungu:

"Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia. Hayatamfaa mali yake, wala alivyo vichuma. Atauingia Moto wenye mwako." (KuranI 111:1-3)

Hasa, matabiri matatu yalifanywa kuhusu Abu Lahab:

(i) Njama za Abu Lahab dhidi ya Mtume hazingefaulu.

(ii) Mali yake na watoto wake hawangemfaa.

(iii) Angekufa akipinga Dini ya Mwenyezi Mungu, na kuingia Motoni.

Abu Lahab pia alikufa katika hali ya kutoamini kama ilivyotabiriwa na Kurani. Lau Waleed au Abu Lahab wangekubali Uislamu hata kwa nje tu, wangekuwa wameubatilisha utabiri wake na hivyo chanzo chake cha mbinguni!

Zaidi ya hayo, Abu Lahab alikuwa na wana wanne, wawili kati yao walikufa wakiwa na umri mdogo wakati wa uhai wake. Wana wengine wawili na binti mmoja walikubali Uislamu na kumfanya apoteze matumaini! Hatimaye, alikufa kutokana na tauni; watu wasingegusa mwili wake kutokana na hofu ya kuambukizwa na wakatupa matope na mawe juu ya mahali alipofariki ili kuifanya kaburi lake.

Msingi muhimu wa kuamini kwamba maandiko fulani kwa hakika ni ufunuo wa Mungu ni ukweli wa ndani, iwe ni kuhusiana na matukio ya zamani, ya siku zijazo, au katika zama hizo ambazo ufunuo ulitokea. Kama mtu anavyoona, kuna matabiri mengi yaliyotajwa hapo ambayo yatakuja kutimia, huku baadhi yake yalitimizwa katika maisha ya Mtume, na mengine yametimia baada ya kifo chake, na mengine bado hayajatimia.



Vielezi-chini:

[1]Ili kusoma matabiri zaidi ya Kurani, tazama ‘Rehema kwa Walimwengu,' Qazi Suliman Mansoorpuri, vol.3, uk. 248 - 313.

[2] "Heraclius." Encyclopædia Britannica kutoka Malipo ya Encyclopædia Britannica. (http://www.britannica.com/eb/article?tocId=9040092)

[3] "Heraclius." Encyclopædia Britannica kutoka Huduma ya Malipo ya Encyclopædia Britannica. (http://www.britannica.com/eb/article?tocId=9040092)

[4]‘Rehema kwa Walimwengu,’ Qazi Suliman Mansoorpuri, vol.3, uk. 312.

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.