Je Muhammad ndiye Mwandishi wa Kurani?
Maelezo: Baadhi ya ushahidi kwamba Muhammad hakuweza kuwa mwandishi wa Qur'ani.
- Na Imam Mufti
- Iliyochapishwa mnamo 24 Nov 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 05 Sep 2022
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 2,750 (wastani wa kila siku: 2)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Nani aliyeitunga Qur'ani? Lazima kuwe na aliyeitunga! Kwa vyovyote, ni wakazi wangapi wa jangwa katika historia ya mwanadamu wamesimama na kupea ulimwengu kitabu kama Kuranii? Kitabu kina maelezo ya ajabu ya mataifa yaliyopita, manabii, na dini zilizopita pamoja na habari sahihi za kisayansi zisizopatikana wakati huo. Ni nini chanzo cha yote haya? Iwapo tutakanusha ya kwamba Kurani imetoka kwa Mungu, tunaachwa na uwezekano chache tu:
- Mtume Muhammad aliiandika mwenyewe.
- Aliichukua kutoka kwa mtu mwingine. Katika kesi hiyo, aidha aliichukua kutoka kwa Myahudi au Mkristo au mmoja wa wageni wa Arabia. Wakazi wa Makka hawakujishughulisha na kumshtaki kuwa ameichukua kutoka kwa mmoja wao.
Jibu fupi kutoka kwa Mwenyezi Mungu:
"Na wakasema: Hivi ni visa vya watu wa kale alivyo viandikisha, anavyo somewa asubuhi na jioni. Sema: Ameyateremsha haya ajuaye siri za katika mbingu na ardhi. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.’" (Kurani 25:5-6)
Ilijulikana vizuri na wapinzani wake kwamba Muhammad, ambaye alilelewa kati yao, hakujifunza kusoma au kuandika tangu wakati wa kuzaliwa kwake. Walijua kina nani alisuhubiana nao na mahali aliposafiri; walikubali uadilifu na uaminifu wake kwa kumwita 'Al-Ameen,' Mwenye kuaminika, Muaminifu.[1] Walimshtaki tu baada ya mahubiri yake kuwa yeye ni mchawi, malenga na hata mwongo! Hawakuweza kuwa na msimamo. Mungu anasema:
"Tazama vipi wanavyo kupigia mifano. Basi wamepotea. Kwa hivyo hawawezi kuipata njia." (Kurani 17:48)
Hakika Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo mbinguni na katika ardhi. Anayajua ya zamani na yaliyomo, na humdhihirishia haki Nabii wake.
Inawezekana kuwa Muhammad ndiye Mwandishi wake?
Haiwezekani kuwa Muhammad ndiye mwandishi wa Kurani kutokana na sababu zifuatazo:
Kwanza, matukio kadhaa yalijitokeza ambapo angeweza kuja na ufunuo mwenyewe. Kwa mfano, baada ya ufunuo wa kwanza, watu walisubiri kusikia zaidi, lakini Mtume hakupokea chochote kipya kwa miezi. Wakazi wa Makkka Wakaanza kumdhihaki, “Mola wake amemwacha!” Hii iliendelea hadi sura ya 93, Ad-Doha, ilipofunuliwa. Mtume angeweza kutunga kitu na kukitoa kama ufunuo wa hivi karibuni ili kuepukana na kejeli, lakini hakufanya hivyo. Pia, wakati mmoja, baadhi ya wanafiki walimshtaki mke wake mpendwa Aisha kuwa ni mzinifu. Mtume angeweza kuzua kwa urahisi kitu cha kumtoa Aisha lawama, lakini alisubiri siku nyingi zenye adha, maumivu, kejeli na dhiki, mpaka ufunuo ulipotoka kwa Mwenyezi Mungu ukimwondolea Aisha mashtaka.
Pili, kuna ushahidi wa ndani ya Kurani kwamba Muhammad hakuwa mwandishi wake. Aya kadhaa zilimkosoa, na wakati mwingine zilikuwa na maneno makali. Mtume mwongo anawezaje kujilaumu wakati anaweza kupatana na hatari ya kupoteza heshima, labda ufuasi, wa wafuasi wake? Hapa kuna baadhi ya mifano:
"Ewe Nabii! Kwa nini unaharimisha alicho kuhalilishia Mwenyezi Mungu? Unatafuta kuwaridhi wake zako. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." (Kurani 66:1)
"…Na ukaficha nafsini mwako aliyo taka Mwenyezi Mungu kuyafichua, nawe ukawachelea watu, hali Mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki zaidi kumchelea..." (Kurani 33:37)
"Haimpasii Nabii na wale walio amini kuwatakia msamaha washirikina, ijapo kuwa ni jamaa zao, baada ya kwisha bainika kuwa hao ni watu wa Motoni." (Kurani 9:113)
"Ama anaye kujia kwa juhudi. Naye anaogopa! Ndio wewe unampuuza? Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana." (Kurani 80:8-11)
Na lau angelificha chochote basi angezificha aya hizi, lakini aliwasomea watu kwa uaminifu.
"Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu. Wala hii si kauli ya Shetani maluuni. Basi mnakwenda wapi? Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote." (Kurani 81:24-27)
Mtume anatahadharishwa, au labda hata kuonywa, katika Aya zifuatazo:
"Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu hiki kwa haki ili upate kuhukumu baina ya watu kwa alivyo kuonyesha Mwenyezi Mungu. Wala usiwe mtetezi wa makhaaini. Na muombe maghfira Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu. Wala usiwatetee wanao khini nafsi zao. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi aliye khaaini, mwenye dhambi. Wanataka kujificha kwa watu, wala hawataki kujificha kwa Mwenyezi Mungu, naye yu pamoja nao pale wanapo panga njama usiku kwa maneno asiyo yapenda. Na Mwenyezi Mungu anayajua vyema wanayo yatenda,. Hivyo nyinyi mmewatetea hawa katika uhai huu wa duniani. Basi nani atakaye watetea kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama? Au ni nani atakuwa wakili wao wa kumtegemea? Na anaye tenda uovu au akajidhulumu nafsi yake, kisha akaomba maghfira kwa Mwenyezi Mungu, atamkuta Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu. Na anaye chuma dhambi, basi ameichumia nafsi yake mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hikima. Na atendaye kosa au dhambi kisha akamsingizia asiye na kosa, basi amejitwika dhulma na dhambi iliyo wazi. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yako na rehema yake, kundi moja kati yao linge dhamiria kukupoteza. Wala hawapotezi ila nafsi zao, wala hawawezi kukudhuru kwa lolote. Na Mwenyezi Mungu amekuteremshia Kitabu na hikima na amekufundisha uliyo kuwa huyajui. Na fadhila za Mwenyezi Mungu zilizo juu yako ni kubwa." (Kurani 4:105-113)
Aya hizi zinaelezea tukio ambapo mtu kutoka kwa wenyeji Waislamu wa Madina aliiba silaha na kuificha katika ardhi ya jirani yake Myahudi. Wamiliki wa silaha walipomshika alikanusha makosa yoyote, na silaha zikagunduliwa kwa Myahudi. Hata hivyo, Myahudi alimsema jirani yake Mwislamu, pia akikana kuhusika kwake katika uhalifu huo. Watu kutoka kabila la Muislamu walikwenda kwa Mtume ili kumtetea kwa niaba yake, na Mtume akaanza kuelekea upande wao hadi Aya zilizo juu zilipofunuliwa na yule Myahudi kuondolewa ubaya huo. Yote haya licha ya Myahudi kukataa unabii wa Muhammad! Aya zilimuelekeza Mtume Muhammad mwenyewe asiwatetee wadanganyifu! Aya:
"…Wala usiwe mtetezi wa makhaaini. Na muombe maghfira Mwenyezi Mungu…Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yako na rehema yake, kundi moja kati yao linge dhamiria kukupoteza."
Ikiwa ni Muhammad mwenyewe ndiye aliyetunga Kurani, na hivyo kuwa mwongo, angehakikisha kuwa hakuna kitu chochote ambacho kingeweza kuhatarisha ufuasi wa wafuasi wake. Ukweli kwamba Kurani, kwa matukio mbalimbali, inamkosoa Mtume katika masuala fulani ambayo alikuwa amefanya hukumu isiyo sahihi, wenyewe ni ushahidi kwamba haikuandikwa na yeye.
Vielezi-chini:
[1] ‘Muhammad: Maisha Yake Kulingana na Vyanzo vya Mapema Zaidi' na Martin Lings, uk. 34.
Ongeza maoni