Wanasema nini kuhusu Kurani (sehemu ya 1 kati ya 2)

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Kauli za wasomi wa magharibi ambao wamejifunza Uislamu kuhusu Kurani. Sehemu ya 1: Utangulizi na taarifa zao.

  • Na iiie.net
  • Iliyochapishwa mnamo 02 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 2,823 (wastani wa kila siku: 3)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

What_They_Said_about_the_Quran_(part_1_of_2)_001.jpgWanadamu wamepokea mwongozo wa Kiungu kupitia njia mbili tu: kwanza neno la Mungu, pili Manabii ambao walichaguliwa na Mungu kuwasiliana mapenzi yake kwa wanadamu. Vitu hivi viwili vimekuwa vikienda pamoja kila wakati na majaribio ya kujua mapenzi ya Mungu kwa kupuuza mojawapo ya haya mawili yamekuwa yakipotosha. Wahindu waliwapuuza manabii wao na kuweka mkazo kwenye vitabu vyao ambapo ilithibitisha mafumbo ya maneno ambayo walikosa. Hivyo hivyo, Kwa Wakristo, kwa kupuuza kabisa Kitabu cha Mungu, waliweka umuhimu wote kwa Kristo na kwa hivyo sio tu walimwinua kwa Uungu, lakini pia walipoteza kiini cha Tawheed (monotheizim) kilichomo kwenye Biblia.

Kwa hakika, maandiko makuu yaliyofunuliwa kabla ya Kurani, yaani, Agano la Kale na Injili, yalikuja katika mfumo wa vitabu muda mrefu baada ya siku za Manabii na hiyo pia katika tafsiri. Hii ilikuwa kwa sababu wafuasi wa Musa na Yesu hawakufanya juhudi kubwa kutunza Aya hizi wakati wa maisha ya Manabii wao. Badala yake, ziliandikwa muda mrefu baada ya vifo vyao. Kwa hivyo, tunavyo sasa katika mfumo wa Biblia (Agano la Kale na Agano Jipya) ni tafsiri ya mifumo ya kibinafsi ya mafunuo ya asili ambayo yana nyongeza na ufutaji uliofanywa na wafuasi wa Manabii waliotajwa. Kinyume chake, Kitabu kilichofunuliwa mwisho, Kurani, bado kimebaki katika hali yake ya mwanzo. Mungu mwenyewe alihakikishia utunzaji wake na Kurani nzima iliandikwa wakati wa uhai wa Mtume Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, katika vipande tofauti vya majani ya mitende, ngozi, mifupa n.k. Isitoshe, kulikuwa na zaidi ya maswahaba 100 000 ambao walihifadhi Kurani nzima au sehemu yake. Mtume mwenyewe alikuwa akisoma kwa Malaika Gabrieli mara moja kwa mwaka na mara mbili katika mwaka aliokufa. Khalifa wa kwanza Abu Bakr alikabidhi ukusanyaji wa Kurani nzima kwa ujazo mmoja wa mwandishi ya Mtume, Zaid Ibn Thabit. Juzuu hii ilikuwa kwa Abu Bakr hadi kifo chake. Kisha ilikuwa kwa Khalifa wa pili Umar na baada yake ilimjia Hafsa, mke wa Mtume. Ilikuwa kutoka kwenye nakala hii ya asili kuwa Khalifa wa tatu Uthman aliandaa nakala zingine kadhaa na kuzipeleka katika maeneo tofauti ya Waislamu.

Kurani ilihifadhiwa kwa uangalifu sana kwani ni Kitabu cha Mwongozo kwa wanadamu mpaka mwisho wa muda. Ndio sababu haiwalengi Waarabu peke yao ambao ilifunuliwa kwa lugha yao. Inazungumza na mwanadamu kama mwanadamu:

"Enyi watu, nini kimekudanganyeni kuhusu Mola wenu Mlezi, Mkarimu."

Utendaji wa mafundisho ya Kurani umewekwa kwa mifano ya Mtume Muhammad na Waislamu wazuri kwa kila kizazi. Njia tofauti ya Kurani ni kuwa maagizo yake yanalenga ustawi wa jumla wa mwanadamu na yanategemea uwezekano wa yeye kuyafikia. Katika vipimo vyake vyote hekima ya Kurani ni kamilifu. Hailaani wala kuutesa mwili wala haijali roho. Haiweki ubinadamu kwa Mungu wala haifanyi mwanadamu kuwa mungu. Kila kitu kimewekwa kwa uangalifu mahali panapostahili.

Hakika wasomi ambao wanadai kuwa Muhammad ndiye mwandishi wa Kurani wanadai kitu ambacho kibinadamu hakiwezekani. Je! Kuna mtu yeyote wa karne ya sita K.W.K .anayeweza kusema ukweli wa kisayansi kama vile Kurani ilivyo? Je! Angeweza kuelezea mageuzi ya kijusi ndani ya uterasi kwa usahihi jinsi tunavyopata katika sayansi ya kisasa?

Pili, ni jambo la busara kuamini kwamba Muhammad, ambaye hadi umri wa miaka arobaini aliwekwa alama kwa uaminifu na uadilifu wake, kuanza ghafla uandishi wa kitabu kisicholingana na sifa ya fasihi na usawa ambao kundi lote la washairi wa Kiarabu na wasemaji wa hali ya juu hawakuweza kutoa? Mwisho, je! Ni mantiki ya kuwa Muhammad, aliyejulikana kama Al-Ameen (anayeaminika) katika jamii yake na ambaye bado anasifiwa na wasomi wasio Waislamu kwa uaminifu na uadilifu wake, alikuja na madai ya uwongo na aliweza kutoa mafunzo kwa maelfu ya wanadamu, ambao walikuwa wanadamu waadilifu ili kuunda jamii bora ya wanadamu duniani?

Hakika, mtaftaji yeyote wa ukweli na asiye na upendeleo atakuja kuamini kuwa Kurani ni ufunuo wa Kitabu cha Mungu.

Bila ulazima wa kukubaliana na yote waliyosema, hapa tunatoa maoni kadhaa ya muhimu ya wasomi wasio Waislamu juu ya Kurani. Wasomaji wanaweza kuona kwa urahisi jinsi ulimwengu wa kisasa unaukaribia ukweli kuusu Kurani. Tunatoa rai kwa wasomi wote wenye nia ya wazi ya kusoma Kurani kwa kuzingatia maoni yaliyotajwa hapo juu. Tuna hakika kwamba jaribio lolote kama hilo litamsadikisha msomaji kuwa Kurani haiwezi kuandikwa na mwanadamu yeyote.

Goethe, aliyenukuliwa katika T.P. Hughes’ Dictionary of Islam, uk. 526:

"Hata hivyo, mara kwa mara tunairejelea (Kurani Tukufu) awali ikijitokeza kila mara kama mpya, kisha kwa haraka inavutia na kushangaza, na mwishowe itaimarisha uchaji Mungu wetu...Mbinu yake, kuambatana na yale yaliyomo na malengo yake yanashangaza, makubwa, hatari - ya milele na kwa hakika yaliyotukuka - Kwa hivyo, kitabu hiki kitafaa pakubwa kwa mazoezi ya ngazi zote za umri kama njia bora ya kukisambaza."

Maurice Bucaille, The Quran and Modern Science, 19812, uk. 18:

"Kuichunguza [Kurani] kwa dhati kabisa kulingana na maarifa ya kisasa, kunatuongoza kutambua makubaliano haya wawili, kama ilivyoonyeshwa tayari mara kadhaa, Inatufanya tuone kuwa haifikiriki kwa mtu kama Muhammad. kuwa mwandishi wa taarifa kama hizo kwa sababu ya kiwango cha maarifa katika zama zake. Mawazo kama hayo ni sehemu ya kile kinachoipa Ufunuo wa Kurani nafasi yake ya kipekee, na inamlazimisha mwanasayansi asiye na upendeleo kukubali kutoweza kwake kutoa ufafanuzi ambao unatafuta tu hoja ya tafakuri au mawazo ya kidunia."

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.