O artigo / vídeo que você requisitou não existe ainda.
The article/video you have requested doesn't exist yet.
您所请求的文章/视频尚不存在。
The article/video you have requested doesn't exist yet.
あなたが要求した記事/ビデオはまだ存在していません。
The article/video you have requested doesn't exist yet.
L'articolo / video che hai richiesto non esiste ancora.
The article/video you have requested doesn't exist yet.
요청한 문서 / 비디오는 아직 존재하지 않습니다.
The article/video you have requested doesn't exist yet.
המאמר / הסרטון שביקשת אינו קיים עדיין.
The article/video you have requested doesn't exist yet.
O artigo / vídeo que você requisitou não existe ainda.
The article/video you have requested doesn't exist yet.
您所请求的文章/视频尚不存在。
The article/video you have requested doesn't exist yet.
あなたが要求した記事/ビデオはまだ存在していません。
The article/video you have requested doesn't exist yet.
L'articolo / video che hai richiesto non esiste ancora.
The article/video you have requested doesn't exist yet.
요청한 문서 / 비디오는 아직 존재하지 않습니다.
The article/video you have requested doesn't exist yet.
המאמר / הסרטון שביקשת אינו קיים עדיין.
The article/video you have requested doesn't exist yet.
Uislamu hutoa haki nyingi za kibinadamu kwa mtu binafsi. Zifuatazo ni baadhi ya haki hizo za kibinadamu ambazo Uislamu hulinda.
Uhai na mali ya raia wote katika nchi ya Kiislamu huhesabiwa kuwa takatifu, iwe mtu huyo ni Muislamu au asiye Muislamu. Uislamu pia hulinda heshima. Kwa hivyo, katika Uislamu, kutukana wengine ama kuwafanyia mzaha hakuruhusiwi. Mtume Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, alisema: "Kwa hakika damu zenu, na mali zenu, na heshima zenu zisikiukwe."[1]
Ubaguzi wa rangi hauruhusiwi katika Uislamu, kwa sababu Kurani inaongelea kuhusu usawa wa kibinadamu kwa njia ifuatayo:
"Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mcha Mungu zaidi katika nyinyi.[2] Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye habari." (Kurani 49:13)
Uislamu unapinga baadhi ya watu binafsi au mataifa fulani kupendelewa kwa sababu ya utajiri wao, nguvu zao ama koo zao. Mwenyezi Mungu aliwaumba wanadamu wakiwa sawasawa, ambao wanapaswa kupambanuliwa na kila mmoja kwa msingi wa imani zao na uchaji Mungu wao. Mtume Muhammad alisema: "Enyi Watu! Mungu wenu ni mmoja na babu mkuu wenu (Adam) ni mmoja. Mwarabu sio bora kuliko asiye Mwarabu na asiye Mwarabu sio bora kuliko Mwarabu, na mtu mwekundu (yaani weupe wa asili ya Uesia) sio bora kuliko mtu mweusi (yaani weusi wa asili ya Uafrika) na mtu mweusi sio bora kuliko mtu mwekundu,[3] isipokuwa katika uchaji Mungu."[4]
Shida moja kuu inayowakabili wanadamu leo ni ubaguzi wa rangi. Mataifa ambayo yameendelea yanaweza kumtuma mtu kwenda mwezini lakini hayawezi kuzuia mtu kumchukia na kupigana na mwanadamu mwenzake. Tangu enzi za Mtume Muhammad, Uislamu umetoa mfano dhahiri wa jinsi ubaguzi wa rangi unaweza kukomeshwa. Hija ya kila mwaka kwenda Makkah inaonyesha udugu halisi wa Kiislamu wa makabila na mataifa yote, ambapo Waislamu wapatao milioni mbili kutoka kote ulimwenguni hukutana Makkah kutekeleza amali ya hija.
Uislamu ni dini ya uadilifu. Mwenyezi Mungu anasema:
"Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe. Na mnapo hukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu...." (Kurani 4:58)
Vilevile anasema:
"...Na hukumu ni kwa uadilifu. Hakika, Mwenyezi Mungu anawapenda wanao hukumu kwa haki." (Kurani 49:9)
Tunafaa hata kuwa waadilifu kwa wale tunaowachukia, kama vile Mungu anavyosema:
"...Wala kuchukia wengine kusiwafanye kuacha uadilifu. Kuweni Waadilifu; hivyo ndivyo kuwa karibu mno na uchaMungu...." (Kurani 5:8)
Mtume Muhammad alisema: "Enyi watu, jihadharini na dhuluma,[5] kwani udhalimu utakuwa giza siku ya Kiyama."[6]
Na wale ambao hawajapata haki zao (yaani, kwa kudai haki zao) katika maisha ya sasa duniani watazipata Siku ya Kiyama, kama vile Mtume alivyosema: "Siku hiyo ya Kiyama, haki zote zitapewa kwa wale wanaostahiki (na maovu yatalipizwa)..."[7]
[1] Imepokelewa kutoka Saheeh Al-Bukhari, #1739, and Mosnad Ahmad, #2037.
[2] Mcha Mungu ni muumini anayejiepusha na kila aina za madhambi, anayetenda kila lililo jema ambalo Mwenyezi Mungu alituamrisha kulitekeleza, na humwogopa na kumpenda Mwenyezi Mungu.
[3] Rangi zilizotajwa katika hadithi hii ya Mtume ni mifano tu. Maana yake ni kuwa katika Uislamu hakuna mtu bora kuliko mwingine kwa sababu ya rangi ya ngozi yake, iwapo ni nyeupe, nyeusi, nyekundu, au rangi yoyote ile.
[4] Imepokelewa kutoka Mosnad Ahmad, #22978.
[5] yaani kudhulumu wengine, kutofanya uadilifu, au kuwatendea wengine maovu.
[6] Imepokelewa kutoka Mosnad Ahmad, #5798, and Saheeh Al-Bukhari, #2447.
[7] Imepokelewa kutoka Saheeh Muslim, #2582, and Mosnad Ahmad, #7163.
Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.
Orodha yako ya historia ipo tupu.
Kwa nini kujiandikisha? Tovuti hii ina miundo kadhaa uliyoundwa mahsusi kwa ajili yako, kama vile: vipendwa vyako, historia yako, kutia alama makala ambazo umezitazama awali, kuorodhesha makala zilizochapishwa tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho, kubadilisha ukubwa wa herufi, na zaidi. Vipengele hivi vinatokana na vidakuzi na vitafanya kazi ipasavyo tu unapotumia kompyuta ile ile. Ili kuwezesha vipengele hivi kutoka kwa kompyuta yoyote, unapaswa kuingia wakati katika tovuti hii.
Tafadhali ingiza Jina lako la mtumiaji na anwani ya barua pepe kisha ubofye kitufe cha Tuma neno la siri. Utapokea neno la siri jipya hivi karibuni. Tumia neno la siri hili jipya kufikia tovuti.
Ongeza maoni