Madai ya Muhammad katika Utume (sehemu ya 1 katika ya 3): Ushahidi wa Utume Wake
Maelezo: Ushahidi wa madai kuwa Muhammad alikuwa nabii wa kweli na si muongo. Sehemu ya 1: Baadhi ya ushahidi uliopelekea masahaba mbalimbali kuamini utume wake.
- Na Imam Mufti
- Iliyochapishwa mnamo 25 Nov 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 02 Oct 2022
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 3,914
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Uwezeshaji wa kimungu unalingana na mahitaji ya mwanadamu. Mungu hurahisisha upataji kadiri uhitaji wa wanadamu unavyoongezeka. Hewa, maji, na nuru ya jua ni vya lazima kwa ajili ya kuwepo kwa mwanadamu, na hivyo Mungu ameruhusu kupatikana kwake kwa vyote bila ugumu. Hitaji kuu zaidi la mwanadamu ni kumjua Muumba, na hivyo, Mungu amefanya iwe rahisi kumjua. Ushahidi wa Mungu, hata hivyo, hutofautiana katika asili yake. Kwa njia yake yenyewe, kila kitu katika uumbaji ni uthibitisho wa Muumba wake. Uthibitisho mwingine wa dhahiri sana hadi mtu yeyote wa kawaida anaweza ‘kumwona’ mara moja Muumba, kwa mfano, mzunguko wa uhai na kifo. Wengine ‘wanaona’ kazi ya mikono ya Muumba katika umaridadi wa nadharia za hisabati, sanjari za ulimwengu mzima wa fizikia, na ukuzi wa kijusi:
"Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na kukhitalifiana usiku na mchana ziko Ishara kwa wenye akili." (Kurani 3:190)
Kama vile uwepo wa Mungu, wanadamu wanahitaji ushahidi ili kuthibitisha ukweli wa manabii walionena kwa jina Lake. Muhammad, kama manabii waliomtangulia, alidai kuwa nabii wa mwisho wa Mungu kwa wanadamu. Kwa kawaida, ushahidi wa ukweli wake ni tofauti na mwingine. Baadhi ni dhahiri, nyingine huonekana tu baada ya kutafakari kwa kina.
Mwenyezi Mungu anasema ndani ya Kurani:
"…Haikutoshi kwamba Mola wako Mlezi kuwa Yeye ni Shahidi wa kila kitu?" (Kurani 41:53)
Ushahidi wa Kimungu peke yake unatosha bila ushahidi mwingine wowote. Shahidi wa Mungu kwa Muhammad upo katika:
(a) Ufunuo wa Mungu uliopita kwa mitume wa mwanzo ulitabiri kutokea kwa Muhammad.
(b) Matendo ya Mungu: miujiza na ‘ishara’ alizozitoa ili kuunga mkono madai ya Muhammad.
Haya yote yalianza vipi katika siku za mwanzo za Uislamu? Waumini wa mwanzo walisadikishwaje kwamba alikuwa nabii wa Mungu?
Mtu wa kwanza kuamini utume wa Muhammad alikuwa mke wake mwenyewe, Khadija. Aliporudi nyumbani akitetemeka kwa hofu baada ya kupata ufunuo wa Mwenyezi Mungu, alikuwa ni faraja yake:
"Kamwe! Mungu hatakuaibisha. Dumisha uhusiano mzuri na watu wa ukoo wako, saidia masikini, wahudumie wageni wako kwa ukarimu, na saidia wale waliopatwa na misiba." (Saheeh Al-Bukhari)
Alimuona mtu kwa mumewe, ambaye Mungu hatamdhalilisha, kwa sababu ya fadhila zake za uaminifu, haki, na kusaidia masikini.
Rafiki yake wa karibu zaidi, Abu Bakr ambaye alikuwa amemfahamu maisha yake yote na alikuwa wakikalibiana kwa kwa rika, aliamini mara tu aliposikia maneno, ‘Mimi ni Mtume wa Mungu’ bila ya uthibitisho wowote wa ziada zaidi ya kitabu kilicho wazi cha maisha ya rafiki yake.
Mtu mwingine ambaye alikubali wito wake kwa kuusikiliza tu, alikuwa ‘Amr’[1] Anasema:
"Nilikuwa nikifikiri kabla ya Uislamu kwamba watu ni wakosefu na hawakuwa juu ya kitu. Waliabudu sanamu. Wakati huohuo, nilisikia juu ya mtu mmoja akihubiri huko Makka; basi nikaenda kwake…nikamuuliza: ‘Wewe ni nani?’ Akasema: ‘Mimi ni Mtume.’ Nikasema tena: ‘Nabii ni nani?’ Akasema: ‘Mungu amenituma.’ Nikasema: Alikutuma na nini?’ Akasema: ‘Nimetumwa kuunganisha mafungamano, kuvunja masanamu, na kutangaza umoja wa Mwenyezi Mungu, bila kuwa na chochote kinachomshirikisha (katika ibada). Nani yu pamoja nawe katika hili?’ Akasema: ‘Mtu huru na mtumwa (akimaanisha Abu Bakr na Bilal, mtumwa, ambaye alikuwa ameukubali uislam kwa wakati huo)’ Nikasema: ‘Ninakusudia kukufuata wewe.’" (Saheeh Muslim)
Dimad alikuwa mganga wa jangwani aliyebobea katika magonjwa ya akili. Katika ziara yake huko Makka, aliwasikia watu wa Makka wakisema kwamba Muhammad (rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alikuwa mwendawazimu! Akiwa na uhakika na ujuzi wake, alijiambia, ‘Kama ningemkuta mtu huyu, Mungu anaweza kumponya mkononi mwangu.’ Dimad alikutana na Mtume na akasema: ‘Muhammad, ninaweza kumlinda (mtu) anayeugua ugonjwa wa akili au kwa uchawi, na Mwenyezi Mungu humponya amtakaye kwa mkono wangu. Je, unatamani kuponywa?’ Mtume wa Mwenyezi Mungu akajibu, akianza na utangulizi wake wa kawaida wa hotuba zake:
"Hakika sifa na shukrani ni kwa Mungu. Tunamsifu na kumuomba msaada. Anaye muongoza Mwenyezi Mungu hakuna wa kumpoteza, na aliye potea hawezi kuongozwa. Nashuhudia hakuna anayestahiki kuabudiwa ila Mwenyezi Mungu, Yeye ni Mmoja, hana mshirika, na Muhammad ni mja na Mtume wake."
Dimad akiwa ameshtushwa na uzuri wa maneno hayo, akamwomba ayarudie, akasema, ‘Nimesikia maneno ya waganga, wachawi na washairi, lakini sijawahi kusikia maneno ya namna hii, yanafika kwenye kina cha bahari. Nipe mkono wako ili niweke kiapo cha utii wangu kwako juu ya Uislamu.[2]
Baada ya Jibrili kuleta ufunuo wa kwanza kwa Mtume Muhammad, Khadija, mke wake, alimchukua kwenda kumtembelea binamu yake mzee, Waraqa ibn Nawfal, msomi wa masuala ya Biblia, ili kujadiliana nae kuhusu tukio hilo. Waraqa alimtambua Muhammad kutokana na tabiri za Biblia na kuthibitisha:
"Huyu ndiye Mlinzi wa Siri (Malaika Jibrili) aliyekuja kwa Musa." (Saheeh Al-Bukhari)
Uso unaweza kuwa dirisha la roho. Abdullah ibn Salam, rabi mkuu wa Madina wa muda huo, aliutazama uso wa Mtume alipofika Madina, na akasema:
"Pindi nilipoutazama uso wake, nikajua siyo uso wa mtu mwongo!" (Saheeh Al-Bukhari)
Wengi wa wale waliokuwa karibu na Mtume ambao hawakuukubali Uislamu hawakutilia shaka ukweli wake, lakini walikataa kufanya hivyo kwa sababu nyinginezo. Ami yake, Abu Talib, alimsaidia katika maisha yake yote, alikiri ukweli wa Muhammad, lakini alikataa kujitenga na dini ya babu zake kwa sababu ya aibu na hadhi ya kijamii.
Ongeza maoni