Kwa Nini kumpenda Mungu (sehemu ya 2 kati ya 2)

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Kuelewa upendo wa Mungu kupitia Majina Yake, na jinsi ya kupokea upendo Wake maalumu.

  • Na Hamza Andreas Tzortzis (http://www.hamzatzortzis.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 05 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 1,639 (wastani wa kila siku: 2)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Rehema

Why-Love-God-part-2.jpgInasemekana kuwa neno lingine la upendo ni rehema. Moja ya majina ya Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa Rehema; neno la Kiarabu lililotumika ni Ar-Rahmaan. Tafsiri hii ya Kiingereza haiwakilishi kikamilifu kina na uzito ambao maana ya neno hili hubeba. Jina la Ar-Rahmaan lina maana tatu kuu: ya kwanza ni kwamba rehema ya Mungu ni rehema kali; ya pili ni kwamba rehema yake ni rehema ya mara moja; na ya tatu ni rehema yenye nguvu sana ambayo hakuna kinachoweza kuizuia. Rehema ya Mwenyezi Mungu imezunguka kila kitu na anapendelea mwongozo kwa watu. Katika kitabu cha Mwenyezi Mungu, Kurani, Anasema,

"… Na Rehema yangu imeenea kila kitu…." (Kurani 7:156)

"Arrah'man, Mwingi wa Rehema amefundisha Kurani." (Kurani 55:1-2)

Katika aya hiyo hapo juu, Mungu anasema Yeye ni Mwingi wa Rehema, ambayo inaweza kueleweka kama "Mola wa Rehema", na kwamba alifundisha Kurani. Hii ni dalili ya kubainisha kwamba Kurani iliteremshwa kama dhihirisho la rehema ya Mwenyezi Mungu. Kwa maneno mengine, Kurani ni kama barua moja kubwa ya upendo kwa wanadamu. Kama tu kwa upendo wa kweli, yule anayependa huwatakia mema wapendwa, na huwaonya juu ya mitego na vizuizi, na kuwaonyesha njia ya furaha. Kurani sio tofauti: inawaita wanadamu, na pia inaonya na kutoa habari njema.

Rehema Maalum

Iliyounganishwa na Ar-Rahmaan, ni Ar-Raheem. Jina hili lina mzizi sawa na la awali, ambalo hutoka kwa neno la Kiarabu linaoashiria tumbo. Hata hivyo tofauti ya kimaana ni muhimu. Ar-Raheem inamaanisha rehema maalumu kwa wale wanaotaka kuikumbatia. Yeyote anayechagua kukubali mwongozo wa Mungu kimsingi amekubali rehema yake maalumu. Rehema hii maalum ni kwa ajili ya waumini na inadhihirika peponi; amani yenye furaha isiyo na mwisho na Mungu.

Upendo maalumu

Kwa mujibu wa Kurani, Mwenyezi Mungu ni Mwenye upendo. Jina la Kiarabu ni Al-Wadood. Hii inahusu upendo maalumu unaoonekana. Inatokana na neno wudi, ambalo linamaanisha kuonyesha upendo kupitia tendo la kutoa: "Naye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi." (Kurani 85:14)

Upendo wa Mungu unapita aina zote tofauti za upendo. Upendo wake ni mkuu kuliko aina zote za upendo za kidunia. Kwa mfano, upendo wa mama, ingawa hauna ubinafsi, unategemea uhitaji wake wa ndani wa kumpenda mtoto wake. Inamkamilisha, na kupitia kujitoa kwake anajisikia mzima na aliye ridhika. Mungu ni Kiumbe huru anayejitosheleza na mkamilifu; Yeye hahitaji chochote. Upendo wa Mungu hautegemei hitaji au haja; kwa hiyo ni aina safi kabisa ya upendo, kwa sababu Yeye hapati chochote kabisa kutokana na kutupenda.

Katika nuru hii, tunawezaje kutompenda Yule ambaye ni mwenye upendo zaidi kuliko chochote tunachoweza kufikiria? Mtume Muhammad (amani na baraka ziwe juu yake) amesema: “Mwenyezi Mungu ni Mpole zaidi kwa waja wake kuliko mama kwa watoto wake.[1]

Ikiwa Mungu ndiye mwenye upendo zaidi, na upendo Wake ni mkuu kuliko upendo mkuu zaidi wa kidunia ambao tumepitia, hii inapaswa kuweka ndani yetu upendo wa kina zaidi kwa Mungu. Kwa kiasi kikubwa, hili linapasa kufanya tutake kumpenda kwa kuwa mmoja wa watumishi Wake. Al-Ghazali alisema kwa usahihi, "Kwa wale waliojaaliwa ufahamu kwa hakika hakuna kitu cha kupendwa isipokuwa Mungu, hakuna anaye stahili upendo ila Yeye."[2]

Kwa mtazamo wa kiroho, upendo wa Mungu ni baraka kuu zaidi ambayo mtu yeyote anaweza kupata, kwa kuwa ni chanzo cha utulivu wa ndani, upole, na furaha ya milele akhera. Kutompenda Mungu sio tu njia ya kutokuwa na shukrani, lakini ni aina kuu ya chuki. Kutompenda Yeye ambaye ni chanzo cha upendo ni kukataa kile kinachowezesha upendo kutokea na kujaza mioyo yetu.

Mungu halazimishi upendo Wake maalumu kwetu sisi. Ingawa, kwa rehema Zake, anatupa kwa upendo kila wakati wa maisha yetu, ili kushika kikamilifu upendo wa Mungu na kuwa wapokeaji wa upendo Wake maalumu, mtu lazima aingie katika uhusiano Naye. Ni kana kwamba upendo wa Mungu unatungoja tuukubali. Hata hivyo, tumefunga mlango na kuweka vitasa. Tumeufunga mlango kwa kumkana, kumpuuza na kumkataa Mungu. Ikiwa Mungu angelazimisha upendo Wake maalumu juu yetu, upendo ungepoteza maana yote. Tuna chaguo: kufuata njia sahihi na hivyo kupata upendo maalumu wa Mungu na rehema, au kukataa mwongozo wake na kukabiliana na matokeo ya kiroho.

Kiumbe mwenye upendo zaidi anakupenda, lakini ili uweze kushika kikamilifu upendo huo maalumu, na ili uwe na maana, unapaswa kuchagua kumpenda yeye na kufuata njia inayoongoza kwenye upendo Wake. Njia hii ni njia ya Mtume Muhammad (rehema na amani ziwe juu yake):

"Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu." (Kurani 3:31)

Swali muhimu linalofuata kutokana na hili ni: Ninajua kwa nini ni lazima nimpende Mungu, lakini ninampendaje? Natumaini kuelezea hili katika kipande kingine. Hata hivyo, kuhitimisha, nakuacha na maneno ya mwanatheolojia wa karne ya 14, Ibn Al-Qayyim:

"Hakuna shaka kwamba utumwa kamili kwa Mungu ni sehemu ya upendo kamili, na upendo mkamilifu umeunganishwa na ukamilifu wa mpendwa ndani Yake, kwani Mungu, na atukuzwe, ni mkamilifu na ametimia kabisa katika nyanja zote, na Kwa mtu wa namna hii, hakuna kitu kinachoweza kuwa kipenzi zaidi kwa mioyo ya watu kuliko Yeye; mradi asili yao ya msingi na akili ni nzuri, ni jambo lisiloepukika kwamba Yeye atakuwa kipenzi cha kila kitu katika mioyo yao. Bila shaka kumpenda Yeye kunapelekea kwenye kunyenyekea na kumtii Yeye, kutafuta radhi zake, kufanya kila linalowezekana katika kumwabudu Yeye na kurejea Kwake. Hii ndiyo nia bora na yenye nguvu zaidi ya kufanya ibada."[3]

Ilisasishwa mara ya mwisho tarehe 5 Januari 2017. Imechukuliwa na kurekebishwa kutoka kwa kitabu cha "The Divine Reality: God, Islam & The Mirage of Atheism". Unaweza kununua kitabu hapa.



Rejeleo la maelezo:

[1] Abu Dawud

[2] Al-Ghazali. (2011) Al-Ghazali kuhusu Upendo, Matamanio, Ukaribu na Kutosheka, uk. 23.

[3] Miftaah Daar al-Sa‘aadah, 2/88-90.

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.