Kufanana na Kutofautiana kati ya Uislamu na Ukristo (sehemu ya 1 kwa 2): Sawa lakini ni Tofauti

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Uislamu na Ukristo una mambo tofauti sana ya kusema juu ya dhambi ya asili, wokovu, na siku za mwisho za Yesu.

  • Na Aisha Stacey (© 2017 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 19 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 2,721 (wastani wa kila siku: 3)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Similarities-and-Differences-between-Islam-and-Christianity-2.jpgWaislamu na Wakristo wanafanana sana; kuanzia kwenye maoni yao juu ya kutoa na huruma hadi siku ya mwisho kama ilivyosimuliwa kwa Yesu akionyesha umuhimu huo kipindi chake. Mbali na kufungwa katika mgongano wa kijamii, hata maarifa kidogo huonyesha mfanano kwa kushangaza. Ila, mambo ya mafundisho na imani wakati mwingine yanaweza kuwa na utofauti wa kushangaza. Pamoja na hayo, kuna msingi wa pamoja na sehemu kadhaa za kuanza mazungumzo na majadiliano.

Dhambi ya Asili

Hadithi ya Adamu na Hawa ipo katika Ukristo na Uislamu. Juu juu, hadithi zinaonekana kuwa sawa. Adam ndiye mwanadamu wa kwanza, Hawa ameumbwa kutoka kwenye ubavu wake, na waliishi kwa utulivu katika Pepo. Shetani yuko pamoja nao Peponi; anawapotosha au kuwashawishi kula matunda ya mti uliokatazwa. Lakini mbali na muhtasari huu, hadithi zinatofautiana sana. Kurani na mila ya Mtume Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, zinatuambia kwamba Shetani hakuja kwa Adamu na Hawa akiwa mfano wa nyoka, wala hakuwadanganya kula tunda lililokatazwa. Shetani aliwapotosha na kuwadanganya, na wakafanya makosa makubwa ya maamuzi. Hili halikuwa kosa la Hawa peke yake bali Adamu na Hawa waligawana mzigo wa kosa sawa sawa.

Hakuna wakati wowote katika hadithi ya Kurani inatuambia kuwa Hawa alikuwa dhaifu baina yao wawili au alikuwa anahusika na majaribu ya Adam. Walifanya uamuzi pamoja, na baadaye waligundua makosa yao makubwa, walijitia, na wakaomba msamaha wa Mungu. Mungu aliwasamehe wote wawili. Kwa kuzingatia hii, tunaweza kuona kwamba Uislamu hauna dhana inayoitwa dhambi ya asili. Uzao wa Adamu hawaadhibiwi kwa matendo ya babu yao. Mungu anasema katika Kurani kwamba hakuna mtu anayehusika na maamuzi ya mtu mwingine. "... hakuna mbebaji atakayebeba mzigo wa mwingine ..." (Kurani 35:18) Uislamu hauna wazo kwamba mwanadamu anaweza kuzaliwa akiwa mwenye dhambi. Badala yake, watu huzaliwa katika hali ya usafi na kwa kawaida wanapenda kumwabudu Mungu. Sahani zao ni safi; hakuna kitu cha kusamehewa au kutubu.

Kwa upande mwingine, mafundisho ya Kikristo ya dhambi ya asili yanafundisha kwamba wanadamu wamezaliwa tayari wamechafuliwa na dhambi za Adamu na Hawa. Yesu, wanasema, alizaliwa na alikufa ili kufidia dhambi za wanadamu. Ikiwa unaamini kwamba kifo cha Yesu kilipatanisha dhambi zako, basi mlango wa wokovu umefunguliwa kwako. Uislamu unalikataa hili kabisa. Uislamu unafundisha kwamba Nabii Yesu alitumwa kwa Waisraeli kuthibitisha ujumbe wa Manabii wote kabla yake; kwamba Mungu ni Mmoja, hana washirika, ndugu, au watoto, kwa hivyo, hakuna kitu kinachostahili kuabudiwa isipokuwa Yeye.

Wokovu

Kwa sababu Uislamu unaamini kuwa kila mwanadamu amezaliwa akiwa huru bila dhambi, kubaki katika hali hii mtu anahitaji tu kufuata amri za Mungu, na kujaribu kuishi maisha mazuri. Ikiwa mtu ataangukia katika dhambi lakini anahisi kutaka kutubu, anapaswa kutafuta msamaha wa Mungu. Msamaha unapaswa kutafutwa moja kwa moja kutoka kwa Mungu; hakuna wapatanishi. Quran na Mtume Muhammad wanatuambia kuwa msamaha wa Mungu unapatikana kwa urahisi. Katika mila halisi, tunaona kuwa Nabii Muhammad alisema, "Mungu hunyosha mkono Wake usiku ili kukubali toba ya yule aliyefanya dhambi mchana, na Pia hunyosha mkono Wake mchana ili akubali toba ya yule aliyetenda dhambi wakati wa usiku, (na hayo yataendelea) mpaka jua litakapotoka magharibi. "[1]

Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.’ (Kurani 39:53)

Toba ya dhati huhakikisha msamaha, na wokovu unapatikana kwa kujitiisha kwenye mapenzi ya Mungu. Binadamu atapata tu utoshelevu wa kweli na usalama pindi akiwa na uwezo wa kuwa na matumaini katika rehema na msamaha wa Mungu wakati akiogopa matokeo ambayo yanatokana na kutomchukiza Yeye. Katika Uislamu kukaa katika uhusiano na Mungu ni ufunguo wa wokovu, na Quran inatuambia kuwa imani ya dhati pamoja na matendo mema na tabia zitasababisha uzima wa milele Peponi.

Katika Ukristo hata hivyo, wokovu ni jambo lingine kabisa. Ni kifo cha Yesu Kristo kinachosababisha wokovu. Hasa katika Theolojia ya Katoliki ya Kirumi, ni kifo cha Yesu asiye na hatia, kafara kamili ya damu, ambayo husababisha wokovu. Kifo chake huondoa dhambi za watu wote wanaomkubali Yesu kama mwana wa Mungu na kuamini katika ufufuo wake. Baadhi ya madhehebu ya Kikristo yanaongeza kuwa kazi njema na ukuzaji wa tabia nzuri husaidia katika wokovu wa mtu. Bado, zingine zinahitaji kwamba mtu abatizwe.

Kusulubiwa na Kurudi kwa Yesu

Uislamu na Ukristo unakubali kuwa kusulubiwa kulifanyika, hawakubaliani ikiwa Yesu mwenyewe alisulubiwa na akafa. Wazo la Yesu kufa msalabani ni kiini cha imani ya Kikristo, lakini linakataliwa na Uislamu. Imani ya Kiislamu juu ya kusulubiwa na kifo cha Yesu iko wazi. Uislamu unatufundisha kwamba Yesu hakufa ili kufidia dhambi za wanadamu. Kulikuwa na njama ya kumsulubisha, lakini haikufanikiwa. Mungu kwa rehema yake isiyo na mwisho alimwokoa Yesu kutoka kwenye aibu hii kwa kumuweka wa kufanana nae mtu mwingine na kumuinua akiwa hai, mwili na roho, mbinguni. Quran haiko kimya juu ya maelezo kamili ya mtu huyu alikuwa nani, lakini tunajua na tunaamini kwa hakika kwamba hakuwa Nabii Yesu.

Ukristo na Uislamu pia unakubaliana kuwa Yesu atarudi duniani. Uislamu unaelezea kuwa siku chache kabla ya Siku ya Hukumu, Yesu atarudi ulimwenguni na kuwafundisha wengine kuamini Umoja wa Mungu. Atakuwa mtawala mwenye haki, atavunja misalaba, amuue mpinga Kristo, kisha watu wote wa Maandiko (Wayahudi na Wakristo) wataingia katika Uislamu.

Katika Ukristo kurudi kwa Yesu mara nyingi hujulikana kama Ujio wa Pili. Kuna tofauti nyingi kati ya madhehebu ya Kikristo, hata hivyo, wengi hufundisha kuwa Yesu atarudi kuhukumu kati ya walio hai na wafu, (kufanya hukumu ya mwisho) na kuanzisha Ufalme wa Mungu. Wengi wanaamini kwamba atatawala duniani kwa miaka elfu moja, wengine wakisema kuwa utawala wa Yesu utaanza baada ya kumshinda mpinga Kristo.



Rejeleo la maelezo:

[1] Saheeh Muslim

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.