요청한 문서 / 비디오는 아직 존재하지 않습니다.
The article/video you have requested doesn't exist yet.
המאמר / הסרטון שביקשת אינו קיים עדיין.
The article/video you have requested doesn't exist yet.
Ukweli wa Pepo ni kitu ambacho watu hawataweza kukielewa mpaka waingie humo, lakini Mwenyezi Mungu ametuonyesha mambo machache ndani ya Kurani. Ameelezea kuwa ni sehemu ambayo kimsingi ni tofauti na maisha ya dunia hii, katika asili na madhumuni ya maisha, pamoja na aina za starehe ambazo watu watafurahia humo. Kurani inawaambia watu kuhusu Pepo, ambayo Mwenyezi Mungu anawapa, inaelezea baraka zake kuu, na inatangaza uzuri wake kwa kila mtu. Inafahamisha watu kwamba Pepo ni mojawapo ya njia mbili za maisha zilizo tayarishwa kwa ajili yao huko akhera, na kwamba kila jambo jema litakuwa lao Peponi kwa kiwango kinachopita uwezo wetu wa sasa wa kufikiria. Inaonyesha pia kwamba Pepo ni mahali ambapo baraka zote zimeumbwa kikamilifu na ambapo watu watapewa kila kitu ambacho nafsi na mioyo yao itatamani, na kwamba watu watakuwa mbali na uhitaji na mahitaji, wasiwasi au huzuni, uchungu na majuto. Kila aina ya uzuri na baraka zipo Peponi na zitafunuliwa kwa ukamilifu ambao haujawahi kuonekana au kujulikana hapo awali. Mungu ametayarisha baraka kama hizo hapo kama zawadi, na hizi zitatolewa kwa watu ambao Yeye amependezwa nao.
Lakini ni nini asili ya furaha hizo peponi , na zitakuwaje tofauti na furaha za ulimwengu huu? Tutajaribu kuangazia baadhi ya tofauti hizi.
Ingawa watu katika ulimwengu huu wanapata furaha fulani, kadhalika wanakabiliwa na taabu na mateso mengi. Ikiwa mtu angetathmini maisha wanayoishi, watajua kiwango cha magumu wanayokabiliana nayo yanazidi wepesi na starehe. Maisha ya Akhera hayatakuwa na dhiki wala taabu ndani yake, na watu wataishi humo kwa fahari na furaha tupu. Sababu zote za huzuni, maumivu na mateso wanayopata watu katika maisha haya yatakosekana huko Akhera. Hebu tuangalie baadhi ya sababu hizi.
Mtu anapofikiria mafanikio katika maisha haya, kwa kawaida, hupata taaswira ya nyumba kubwa, vito vya thamani na mavazi, na magari ya gharama kubwa; utulivu wa kifedha unaonekana kuwa ufunguo wa maisha ya furaha. Kwa watu wengi, mafanikio yanahusiana sana na utajiri, ingawa hii ipo mbali zaidi na ukweli. Ni mara ngapi tumewaona matajiri wakubwa wakiishi maisha duni kiasi kwamba wakati mwingine huwapelekea hata kujiua! Utajiri ni kitu ambacho wanadamu kwa asili yao wanatamani kwa gharama yoyote ile, na tamaa hii imeundwa kwa kusudi kubwa na la busara. Wakati tamaa hii haijatimizwa, husababisha kiasi fulani cha huzuni ndani ya mtu. Kwa ajili hiyo, Mwenyezi Mungu amewaahidi wakazi wa Peponi kwamba watapata kila walichokuwa wakikidhania kuhusu mali, kwa wale waliokuwa masikini wa kupindukia, hata walikumbwa na njaa na kiu, kwa wale walio na mali nzuri ambao walitamani hata zaidi. Mungu anatupa maono ya hili anaposema:
“... na vitakuwamo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia …” (Kurani 43:71)
“Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyo tanguliza katika siku zilizo pita!” (Kurani 69:24)
“… Humo watapambwa kwa mavazi ya mikononi ya dhahabu, na watavaa nguo za kijani za hariri na at'ilasi, huku wakiegemea humo juu ya makochi. Ni malipo bora hayo! Na matandiko mazuri mno ya kupumzikia!” (Kurani 18:31)
Sababu nyingine ya maumivu na mateso katika maisha haya ni kifo cha mpendwa au ugonjwa, ambayo yote hayapo Peponi. Hakuna atakayehisi ugonjwa au maumivu Peponi. Amesema Mtume Muhammad kuhusu watu wa Peponi rehema na amani ziwe juu yake:
“Hawataugua kamwe, kupiga chafya au kutema mate.” (Saheeh Al-Bukhari)
Hakuna atakayekufa Peponi. Wote wataishi milele wakifurahia starehe zilizomo. Mtume Muhammad alisema kuwa muitaji ataita watu peponi watakapoingia humo:
"Hakika uwe na afya njema na usiwe mgonjwa tena, uishi na usife tena, uwe mchanga na usiwe dhaifu tena, ufurahie, na usihisi huzuni na majuto tena." (Saheeh Muslim)
Kuhusu majuto yanayopatikana kwa sababu ya mpasuko katika mahusiano ya binafsi, watu hawatasikia kamwe uovu wowote au maoni au maneno yenye kuumiza katika Pepo. Watasikia tu maneno mazuri na maneno ya amani. Mungu anasema:
“Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi, Isipo kuwa maneno ya Salama, Salama!” (Kurani 56:25-26)
Hakutakuwa na uadui baina ya watu wala chuki:
“Na tutaondoa chuki vifuani mwao, na mbele yao iwe inapita mito.…” (Kurani 7:43)
Mtume alisema:
“Hakutakuwa na chuki wala hasira baina yao, nyoyo zao zitakuwa moja, na watamtukuza Mwenyezi Mungu asubuhi na jioni.” (Saheeh Al-Bukhari)
Watu watakuwa na maswahaba bora katika Akhera, ambao pia walikuwa watu bora zaidi duniani:
“Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume – hao wa pamoja na wale alio waneemesha Mwenyezi Mungu – miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Watu wema. Na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao!” (Kurani 4:69)
Nyoyo za watu wa Peponi zitakuwa safi, maneno yao yatakuwa mazuri, na matendo yao ni mema. Hakutakuwa na mazungumzo ya kuumiza, kuudhi, kukera au kuchochea, kwani Pepo haina maneno na vitendo vyote visivyofaa. Kama tungejadili sababu zote za uchungu katika maisha haya, bila shaka tungeona kutokuwepo kwake au kinyume chake kuwa ni kweli Peponi.
Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.
Orodha yako ya historia ipo tupu.
Kwa nini kujiandikisha? Tovuti hii ina miundo kadhaa uliyoundwa mahsusi kwa ajili yako, kama vile: vipendwa vyako, historia yako, kutia alama makala ambazo umezitazama awali, kuorodhesha makala zilizochapishwa tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho, kubadilisha ukubwa wa herufi, na zaidi. Vipengele hivi vinatokana na vidakuzi na vitafanya kazi ipasavyo tu unapotumia kompyuta ile ile. Ili kuwezesha vipengele hivi kutoka kwa kompyuta yoyote, unapaswa kuingia wakati katika tovuti hii.
Tafadhali ingiza Jina lako la mtumiaji na anwani ya barua pepe kisha ubofye kitufe cha Tuma neno la siri. Utapokea neno la siri jipya hivi karibuni. Tumia neno la siri hili jipya kufikia tovuti.
Ongeza maoni