Mtu wa mwisho kuingia Peponi (sehemu ya 2 kati ya 2): Kidogo tu Zaidi

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Mtu wa mwisho kuingia Peponi na walio kama yeye wanahisi athari kamili ya huruma ya Mungu.

  • Na Aisha Stacey (© 2013 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 11 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 1
  • Imetazamwa: 3,312 (wastani wa kila siku: 4)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

LastPersonEnterParadise2.jpgKatika makala iliyotangulia tuliangalia kwa kina hadeeth kutoka kwa Mtume Muhammad. Ni hadithi fupi kuhusu tabia za mwanadamu inayokuja kwa umbo la simulizi kuhusu mtu wa mwisho kuingia Peponi. Ni mtu aliyetoka Jahannamu, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Mwanzoni mtu huyo alishukuru kwa kuwa katika nafasi kati ya Pepo na Jahannamu na kumhimidi Mungu kwa wema Wake na rehema Yake. Muda ulipita, hata hivyo, na akatambua kwamba kuna mti ulikuwa umetokea hapo. Aliangalia shina lake imara, matawi yake na majani na akatamani kuwa chini ya kivuli chake na kuzima kiu chake na maji yake. Hadithi inavyoendelea tunaona kwamba kila Mungu anapompa mtu huyo kile anachotamani, mtu huyo alitaka kitu kingine; kidogo tu zaidi.

Hadithi hii inaonyesha ukweli kwamba mwanadamu kamwe haridhiki, daima anataka zaidi. Ingawa hili linaweza kuwa jambo la kushangaza kwa mtu ambaye hajawahi kufikiria kuhusu mzunguko wa matakwa, mahitaji na tamaa ambazo wengi wetu tunajipata ndani yake, si jambo geni kwa Mungu. Yeye, Muumba na Mwanzilishi wa ulimwengu, anafahamu vizuri hali ya viumbe Vyake.

Mungu, Muumba, ana maarifa kamili. Anayajua yaliyo wazi na yasiyoonekana. Anajua yaliyo kuwa na yatakayokuwa. Na Yeye ndiye Mwenye kusikia yote, Mwenye kujua yote. Mungu amesema kwamba yeye yupo karibu na sisi kuliko mshipa wa shingoni, hakuna kitu kinachoepuka maarifa yake. Tunaweza kuficha hulka zetu mbaya na sifa zetu kutoka kwa wenzetu na familia zetu lakini Mungu anaona yote; sio tu hilo, lakini anaelewa pia vitu vipi vinatuhamasisha, vipi tunavyoviogopa, tunavyovipenda au tunavyovitamani. Na ndiyo sababu Yeye daima anatusamehe na anatupa rehema yake . Tunapohitaji rehema ya Mungu kwa jambo lolote, tunafaa kuiulizia tu.

“ Na hakika tumemuumba mtu, nasi tunayajua yanayo mpitikia katika nafsi yake. Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake." (Kurani 50:16)

Kamusi inafafanua rehema kuwa tabia ya kuwa mwema na kusamehe, na hisia inayoleta huruma. Neno la Kiarabu la rehema ni Rahmah na majina mawili muhimu zaidi ya Mwenyezi Mungu yanatokana na neno hili, Ar-Rahman, Mwingi wa Rehema na Ar-Raheem, Mwingi wa Rehema. Rehema ya Mungu inajumuisha upole, utunzaji, kujali, upendo na msamaha. Sifa hizi zinapoonekana katika ulimwengu huu, ni mfano tu wa rehema ya Mungu kwa uumbaji wake. Katika hadithi hii tunaweza kuona wazi rehema ya Mungu kwa jinsi anavyomwitikia huyu mtu wa mwisho kutoka Jahannamu.

Katika hatua hii ni muhimu kutambua kwamba mtu huyu hakuingia Paradiso kwa sababu ya matendo yake mema, la hasha. Mwishowe aliingia Peponi kwa huruma ya Mungu. Inaweza kusemwa kuwa Mungu hupeana rehema yake ingawa haionekani, kwa mtazamo ya mwanadamu, kuwa ya kustahiliwa. Hakika Mwenyezi Mungu ameahidi kwamba mwenye kuamini kwa moyoni mwake hata kama amefanya dhambi nyingi, ataingia Peponi siku moja. Ili kuimarisha ufahamu huu Mtume Muhammad alituacha na maneno yafuatayo:

"Na atakaye kufa bila ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu basi ataingia Peponi.”[1]

Ukweli kwamba watu hawa pamoja na mtu anayezungumziwa watatolewa nje ya Jahannamu na kupelekwa Peponi haitawafanya watu hawa wenye heri wapate huzuni wowote au dhiki. Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu anatuambia kwamba Pepo ndiyo nyumba ya neema. Hakuna chochote ndani ya Qurani au hadeeth za Mtume Muhammad kinachopendekeza kwamba watu hawa wataishi na majuto baada ya kuingia Peponi kutokana na adhabu waliyopata katika Jahannamu. Hii inaonekana wazi kwa furaha ya mtu huyo alipojikuta katika nafasi kati ya Peponi na Jahannamu. Anaonekana kuwa amepona mara moja na tayari anaangalia upande wa siku zijazo. Katika hadeeth zingine kutoka kwa Mtume Muhammad tunajua kwamba Pepo itawasahaulisha Waislamu shida zote walizozipata duniani, kwa hivyo tunaweza kusema kwamba hii pia inajumuisha shida zilizopitiwa katika Jahannamu kabla ya kuingia Peponi. Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehema za Mwenyezi Mungu na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alisema:

“Mtu aliyekuwa tajiri zaidi duniani, miongoni mwa watakao ingia Jahannamu, atahudhurishwa Siku ya Kiyama, na kutiwa Motoni mara moja. Kisha ataulizwa: Ewe mwana wa Adamu, Je! uliwahi ona kheri yoyote? Je! Umewahi kuwa na furaha yoyote? Atasema: Hapana, naapa kwa Mwenyezi Mungu, ewe Mola. Kisha aliyekuwa masikini zaidi duniani, miongoni mwa wanaoingia Peponi, ataletwa na atawekwa Peponi, na ataambiwa: Ewe mwana wa Adam! Je, umewahi kupata shida yoyote? Atasema: Hapana, naapa kwa Mwenyezi Mungu, ewe Mola. Sijawahi kuona chochote kibaya na sijawahi kupata shida yoyote."[2]

Dalili nyingine ya kuonyesha kwamba mtu kuzama katika neema ya Pepo itaondoa shida zote zilizotangulia, hata shida ya kuadhibiwa Jahannamu, ni kauli ya Mtume: “Anayeingia Peponi atafurahia neema na hatakuwa na huzuni, nguo zake hazitaisha na ujana wake hautapotea.”[3]

Baraka hii inaonyesha kwamba taabu itafutwa kwa yule anayeingia Peponi, na inajumuisha kila mtu anayeingia humo, awe ameipitia Jahannamu au la.

Na rehema ya Mwenyezi Mungu haina mipaka. Mtume Muhammad pia alisema:

"Mwenyezi Mungu ana sehemu mia za rehema, ambazo katika hizo ameteremsha moja baina ya majini, watu, wanyama na wadudu, na kwa hiyo sehemu wanahurumiana kati yao, na ni kwa hiyo sehemu wanyama wa pori wanahurumia watoto wao. Na Mwenyezi Mungu amewawekea waja wake sehemu tisini na tisa za rehema ambazo atawahurumia nazo Siku ya Kiyama."[4]



Vielezi-chini:

[1] Saheeh Muslim

[2] Ibid

[3] Ibid

[4] Ibid

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.